Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Tanguj vita vianze baina ya Ukraine na Urusi kumekuwepo na lawama kutoka Ukraine kuwa kutofanikiwa kwa zoezi la kurudisha mapigo ya Urusi kikamilifu ni kutokana na kutopatiwa silaha muhimu walizokuwa wakiziomba.
Hali sasa imebadilika ambapo afisa mmoja na mshauri wa karibu wa raisi Zelensky wa nchi hiyo amesema kuna upungufu mkubwa wa wapiganaji kiasi kwamba vifaa vipya walivyopokea havina wa kuvitumia kikamilifu.
Katika muda huu wa vita watu wanaume wote wenye umri wa miaka 18 mpaka 60 wamezuiliwa kusafiri kutoka nje ya nchi.Hata hivyo Andriy Demchenko ambaye ni afisa wa uhamiaji ameliambia shirika la habai la AFP kuwa jumla ya watu 6100 wamekamatwa wakiwa wameghushi nyaraka zao ili wapate kukimbia kutoka nchi hiyo.