Ingawa wakristu wanajieneza kwa kupinga sana uislamu, ni wazi kwa nini uislamu umekuwa unasambaa sana Marekani siku za hivi karibuni huku ukiristo ukisinyaa.
Mim ni nilikuwa nasali kanisa la kikatoliki kwa muda mrefu sana kwani ndilo nililoona lilikuwa karibu na nyumbani kwani na ibada zake zianendeshwa kama zile za Kiluteri nilikotokea. Isipokuwa niliacha tena kwenda kanisani kwani kila mara sehemu kubwa ya mahubiri yao ni kuhimiza watu kuchagua republican tu.
Baada ya kuhudhuria kwa muda mrefu kanisa hilo, niliggundua kuwa hata mapadri walikuwa na ubaguzi fulani dhidi ya watu weusi. Sasa ukienda kwenye hao Evangelicals, ndiko utakuta wanalofahamu ni kuwa Marekani ni nchi ya weupe tu, wengine wote ni haramu.
Jana nimekutana na website hii ndipo nikagundua kweli imani yangu kuhusu ukristo kukosa mweleko ni ya kweli kabisa.
Welcome to the official home of the God Bless The USA Bible, the only Bible endorsed by President Donald J. Trump and Lee Greenwood.
Namshukuru Mungu nimeshakaa huko amerika. Ukweli ni kwamba, sio kweli kwamba Ukristo Marekani umekosa mwelekeo. Never. ila Ukristo Afrika ndio umekosa mwelekeo kabisa. Marekani huwezi kukuta kina mwamposa wanauza maji na mafuta au wanasema watu waje wakanyage mafuta, huwezi kuona sarakasi hizi za kuseta watu walete nywele za utosi au kucha kidole kidogo au kidole gumba, haya ni kwa waafrika tu.
HATA HIVYO, haimaanishi kwamba Afrika hakuna waamini wa kweli. pamoja na kuwepo manabii wengi wa uongo, bado wapo waamini wa kweli wanaotembea na Mungu na wataurithi uzima wa milele. pamoja na kwamba shetani amepambana sana kudanganya watu, upande mwingine pia watu wa Mungu wamepambana sana kuhubiri injili ya kweli, na wapo wanaoishi katika injili ya kweli.
Na marekani nako hivyo hivo, kuna ushoga mwingi sana, na ubaguzi wa rangi pia, freemasonly, na mambo mengi ya kishetani, lakin bado wapo watu ambao wanamwendea Mungu kwa utakatifu, na ni wengi kuliko hata hawa waliopo bongo. bongo wengi ni wanafiki, hatujazaliwa na kukuzwa kwenye kuwa wakweli, mzungu akifanya dhambi anakuja kukuambia nimefanya dhambi, yupo huru, ila mbongo akifanya dhambi anaweza kufa nayo. wapo wengine waliokoka wakaanguka, hawataki kukiri kwamba walifanya dhambi wasije wakaaibika, mzungu hayupo hivyo, anakuambia kabisa nilidondoka, natubu naomba nisaidiwe kusimama tena kwasababu namuhitaji Mungu.
uwepo wa mashoga marekani haimaanishi kila mzungu anashabikia ushoga, kuna wazungu wengi sana nawajua hawataki hata kusikia icho kitu, na wanaongea waziwazi hata huko ulaya.
kwa habari ya ubaguzi wa rangi, huu ni udhaifu wa kibinadamu, na hii ni shida ya dunia nzima hata waafrika ni wabaguzi pia. leo hii mhindi akija kusali kanisani kwako, atanyooshewa vidole na kila mtu. "ona yule mhindi kaja kusali", ona yule mwarabu, ona yule mzungu, na hata sisi kwa sisi tunabaguana, utasikia, angalia mchaga asiwe kiongozi, angalia mchaga asiwe mtunza hazina, tumpigie kura fulani kwasababu anatoka ukanda wetu, ukabila umejaa, huo ukabila kwa lugha nyingine ni ubaguzi ule ule tu ila ni wa kabila badala ya wa rangi. na pia, wazungu waliookoka kwa kweli sio wabaguzi. nimeishi huko na mimi nimeokoka na walionisaidia maishani mwangu ni wazungu badala ya waamarekani weusi.
ni kweli kuna hadi makanisa ya wazungu wengi na waafrika wengi, ila utafanyaje sasa, Mungu anaonekana humohumo kama walivyoamua wao wenyewe kuishi na inatokana na desturi zao na historia yao waliyotoka nayo mbali. na hata hivyo, sio makanisa yote utaenda ukute ni weusi watupu hakuna mzungu, au wazungu watupu hakuna weusi. wamejitahidi kupambana na racism lakini kwasababu ni dhambi kama zilivyo nyingine tu, huwezi kuifuta, ni ya kupambana nayo for life, kama ambavyo hata ufanye maombi huwezi kufuta uzinzi, ulevi na dhambi zingine, ila utapambana kuhubiri watu waziache. atakayeziacha anapona asiyetaka ataangamia.