Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Joyce Meyer is a filthy rich celebrity preacher who made her millions through "Joyce Meyer Ministries". In 2005 Joyce Meyer Ministries received $109,000,000. So much for her ministry being a non for profit organization. She has her own private jet and lives in extreme luxury the likes of which most people couldn't even comprehend. Most mega church pastors are false teachers who have been overcome with greed and the desire for vain glory. So many churches today have become completely corrupted and they are run by greedy ministers.Namshukuru Mungu nimeshakaa huko amerika. Ukweli ni kwamba, sio kweli kwamba Ukristo Marekani umekosa mwelekeo. Never. ila Ukristo Afrika ndio umekosa mwelekeo kabisa. Marekani huwezi kukuta kina mwamposa wanauza maji na mafuta au wanasema watu waje wakanyage mafuta, huwezi kuona sarakasi hizi za kuseta watu walete nywele za utosi au kucha kidole kidogo au kidole gumba, haya ni kwa waafrika tu.
HATA HIVYO, haimaanishi kwamba Afrika hakuna waamini wa kweli. pamoja na kuwepo manabii wengi wa uongo, bado wapo waamini wa kweli wanaotembea na Mungu na wataurithi uzima wa milele. pamoja na kwamba shetani amepambana sana kudanganya watu, upande mwingine pia watu wa Mungu wamepambana sana kuhubiri injili ya kweli, na wapo wanaoishi katika injili ya kweli.
Na marekani nako hivyo hivo, kuna ushoga mwingi sana, na ubaguzi wa rangi pia, freemasonly, na mambo mengi ya kishetani, lakin bado wapo watu ambao wanamwendea Mungu kwa utakatifu, na ni wengi kuliko hata hawa waliopo bongo. bongo wengi ni wanafiki, hatujazaliwa na kukuzwa kwenye kuwa wakweli, mzungu akifanya dhambi anakuja kukuambia nimefanya dhambi, yupo huru, ila mbongo akifanya dhambi anaweza kufa nayo. wapo wengine waliokoka wakaanguka, hawataki kukiri kwamba walifanya dhambi wasije wakaaibika, mzungu hayupo hivyo, anakuambia kabisa nilidondoka, natubu naomba nisaidiwe kusimama tena kwasababu namuhitaji Mungu.
uwepo wa mashoga marekani haimaanishi kila mzungu anashabikia ushoga, kuna wazungu wengi sana nawajua hawataki hata kusikia icho kitu, na wanaongea waziwazi hata huko ulaya.
kwa habari ya ubaguzi wa rangi, huu ni udhaifu wa kibinadamu, na hii ni shida ya dunia nzima hata waafrika ni wabaguzi pia. leo hii mhindi akija kusali kanisani kwako, atanyooshewa vidole na kila mtu. "ona yule mhindi kaja kusali", ona yule mwarabu, ona yule mzungu, na hata sisi kwa sisi tunabaguana, utasikia, angalia mchaga asiwe kiongozi, angalia mchaga asiwe mtunza hazina, tumpigie kura fulani kwasababu anatoka ukanda wetu, ukabila umejaa, huo ukabila kwa lugha nyingine ni ubaguzi ule ule tu ila ni wa kabila badala ya wa rangi. na pia, wazungu waliookoka kwa kweli sio wabaguzi. nimeishi huko na mimi nimeokoka na walionisaidia maishani mwangu ni wazungu badala ya waamarekani weusi.
ni kweli kuna hadi makanisa ya wazungu wengi na waafrika wengi, ila utafanyaje sasa, Mungu anaonekana humohumo kama walivyoamua wao wenyewe kuishi na inatokana na desturi zao na historia yao waliyotoka nayo mbali. na hata hivyo, sio makanisa yote utaenda ukute ni weusi watupu hakuna mzungu, au wazungu watupu hakuna weusi. wamejitahidi kupambana na racism lakini kwasababu ni dhambi kama zilivyo nyingine tu, huwezi kuifuta, ni ya kupambana nayo for life, kama ambavyo hata ufanye maombi huwezi kufuta uzinzi, ulevi na dhambi zingine, ila utapambana kuhubiri watu waziache. atakayeziacha anapona asiyetaka ataangamia.
View: https://youtu.be/yNiCLz9IH-g