Ukristo: Mungu hajakataza kuoa mke zaidi ya moja, dhana ya mwili moja si kuwa na mke moja, hata ukilala na malaya ninyi tayari ni mwili moja

Ukristo: Mungu hajakataza kuoa mke zaidi ya moja, dhana ya mwili moja si kuwa na mke moja, hata ukilala na malaya ninyi tayari ni mwili moja

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Tatizo kubwa ni kwamba wakristo wanafata wanachoambiwa na viongozi wa kidini na sio maandiko yanavyosema. Hakuna sehemu imeandika mwanaume aoe mke moja tu.

Kuna huu mstari wa "Nao wawili watakuwa mwili mmoja." i hutafsiriwa vibaya kwa kudhani kwamba mwanaume inabidi awe na mke moja, La hasha!

Mwili moja ni mahusiano halali kwa ndoa ama batili nje ya ndoa yanayowakutanisha kimwili mwanaume na mwanamke kimwili. mwanaume akikutana kimwili hata na malaya tayarini mwili mmoja hapo.


1 Wakorintho 6:16
Maana, kama mjuavyo, anayeungana na kahaba huwa mwili mmoja naye--kama ilivyoandikwa: "Nao wawili watakuwa mwili mmoja.


pia ni dhana ya wingi wa kilicho chini kujikusanya kwa chenye ukuu kuwa kimoja, hata kiroho watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu wako wengi ila wanatengeneza kwa vile wapo chini ya Bwana wanatengeneza roho moja tu,


1 Wakorintho 6:16
Lakini aliyejiunga na Bwana huwa roho moja naye.


basi hivi ndivyo ilivyo kwa mwanaume mwenye wake wengi, licha ya kuwa na wanawake wengi bado itakuwa ni mwili moja.

..............................


Matokeo ya kuafiki maandiko haya

-kuna kesi kibao za wanawake kuwanyima unyumba wanaume zao (njia pekee ni mwanaume kuchepuka)
-Mwanamke anampangia mwanaume wawe na watoto wangapi (anaweza kuzaa mtoto moja shughuli imeisha)
-Mwanaume anaweza asiwe na watoto kama mwanamke ni tasa.
 
Mleta mada ukitaka olewa mke wa pili au oa mke wa pili na zaidi ni hiari yako suala la ukristo achana nalo,unapigia mbuzi gitaa.
 
Uchaguzi ni wako oa au olewa zaidi na zaidi.
sawa, endeleeni na ibada njema..

Mtatandikwa hadi viboko kuondoa mapepo, hakuna namna.

1651409482248.png
 
Back
Top Bottom