Ukristo ni dini ya kipagani, ni dini ya kuabudu jua

Ukristo ni dini ya kipagani, ni dini ya kuabudu jua

Unasema hivyo kwa sababu una ushahidi au kwa sababu watu wengine wanasema hivyo? Kama Ukristo ni dini ya uongo isingechukua miaka zaidi 2000. Ingekuwa imeshakufa. Hakuna dini ya uongo inayowafundisha wanadamu kumrudia Mwenyezi Mungu, kutenda haki, kupendana (upendo wa kweli), kuwaonea huruma wanaoteseka, kusameheana na kuwasaidia wenye shida. Hakuna dini ya uongo ya aina hiyo. Kuna madhehebu ya uongo yanaibuka na huyasemi hayo: yanafundisha watu ufuska etc. Labda kama ukisema aina hii ya madhehebu hapo naweza kukubali.
Jibu hoja je siku ya j2 ni siku ya kuadu jua?
 
Kuhusu kuabudu Jua ni kweli madhehebu ya jumapili yote yanaabudu Mungu jua , na master mind wa hii kitu ni Roman Catholic , na kilele cha sherehe za ibada za jua ni Desember 25

Madhehebu yanayoabudu jumapili ndo yamejaa kero na vurugu tupu , humo ndo kuna mitume , manabii , wanenaji wa Lugha , mara sadaka ya kujimaliza yaani ni vurugu

Hata hvyo bado ukristo ni dini ya kweli
 
Umeandika conspiracy theories kwa kujiamini kabisa yani. Wakristu walikuwa wanaabudu siku ya jumapili kabla ata ya huyo Constantine.
Wakristo hawajawahi kuabudu Jumapili kabla ya constantine mwaka 325BK...weka ushahidi
Costantine hakiwahi kuwa sehemu ya maamuzi ya kanisa ata kidogo. Huu upotoshaji ni ujinga.
Aliyeitisha kikao kikuu cha wakuu wa makanisa yote duniani kwa kipindi hiko alikuwa nani kama sio Constantine?
Kupitia hicho kikao ni mambo mengi yaliingizwa kwenye ukristo ikiwemo siku ya kusali, Utatu mtakatifu, vitabu vya kwenye biblia nk. Nk.

Google tu hata neno council of naicea uone nani aliitisha hicho kikao na nani alikuwa mwenyekiti kwenye hicho kikao kama sio huyo constantine

Wakatoliki kimsingi ambao ndio wakristo wa mwanzo hawaabudu sanamu. Ogopa sana ujinga. Mungu hakukataza sanamu, ndio maana alimuamuru ata Musa akatengeneze sanamu ya nyoka, suleiman pia. Issue ni kuipa sanamu uhai. Kitu ambacho hakuna mkatoliki anafanya. Kama hujui utulie.
Uzuri hizi amri kumi ziko agano la kale kwahyo wakatoliki pamoja na kuifuta hii amri bado tunaweza kuangalia biblia ya kiyahudi na kuujua ukweli uko wapi.
Biblia ambayo haijachakachuliwa inasema:
Kutoka 20:4
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia

Sasa hiyo mifano ya Musa na nyoka, ile hakujifanyia bali aliamrishwa na mungu kutengeneza, kwahyo yeyote aliyeangalia yule nyoka aliamini kuwa ametengenezwa kwa maagizo ya mungu na akimuangalia basi anamtii mungu.
ila wakatoliki kila kanisa lina masanamu kibao, watu wanaenda kuyaabudu... rozali yenyewe ni sanamu na mbaya zaidi ni sanamu ya uongo maana Yehoshuwa hakusulubiwa msalabani kama rozali zilivyomchora.

Alafu unadiriki kusema eti kuna amri wakatoliki wamefuta, ya pili eti, wewe ni juha mkuu. Amri zinafundishwa zote na kufafanuliwa ipasavyo. Nyie wa nje ndio kazi kubwabwaja tu.

Amri ya pili kwenye biblia yenu ya kikatoliki inasemaje?? Je ni sawa na biblia zingine ikiwemo ya kiyahudi??
 
Ni kweli baada ya mfungo sasa mmefungulia kazi iendelee
 
Kuhusu kuabudu Jua ni kweli madhehebu ya jumapili yote yanaabudu Mungu jua , na master mind wa hii kitu ni Roman Catholic , na kilele cha sherehe za ibada za jua ni Desember 25

Madhehebu yanayoabudu jumapili ndo yamejaa kero na vurugu tupu , humo ndo kuna mitume , manabii , wanenaji wa Lugha , mara sadaka ya kujimaliza yaani ni vurugu

Hata hvyo bado ukristo ni dini ya kweli
Tueleze tuelewe,kuabudu maana yake nini?
 
Unazo hoja. Hoja hujibiwa kwa hoja. Subiri wafia dini waje kupangua hoja.

Swali kwako. Owner wa bibilia ni nani? Nani alikuwa na mamlaka ya kuweka na kutoa baadhi ya vitabu kama tunavyosikia kuwa kuna baadhi ya vitabu vimeondolewa kwenye bibilia? Ref. Injili ya Enoch na Barnaba.
Yote hayo yalifanyika chini ya mtawala wa dola la kirumi Constantine, yeye ndo alikuwa na mamlaka ya kubadili chochote kwenye biblia na ndiye aliita baraza la wazee wa makanisa yote duniani na kupitisha hivyo vitabu.
Biblia kupitia Daniel ilimtabiri ujio wake miaka 600 kabla

Daniel 7 23: Akiutabiria ufalme wa dola ya kirumi utakaokuja
24:Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.
24 Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.(constantine)
25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
Atabadili majira na sheria...na kweli constantine alikuja akabadili majira kutoka jumamosi kwenda jumapili na sheria nyingi tu alibadili
 
Yote hayo yalifanyika chini ya mtawala wa dola la kirumi Constantine, yeye ndo alikuwa na mamlaka ya kubadili chochote kwenye biblia na ndiye aliita baraza la wazee wa makanisa yote duniani na kupitisha hivyo vitabu.
Biblia kupitia Daniel ilimtabiri ujio wake miaka 600 kabla

Daniel 7 23: Akiutabiria ufalme wa dola ya kirumi utakaokuja
Atabadili majira na sheria...na kweli constantine alikuja akabadili majira kutoka jumamosi kwenda jumapili na sheria nyingi tu alibadili
Unaseama biblia imebadilishwa alafu mda huo huo unai-quote tena hivi ndo vitimbi na vibweka
 
Wewe unaamini hadith zipi? Ulizoambiwa na mchungaji wako au padri?
Hiyo hadithi uliyoileta ni kutoka kwa wasabato ambao hao hao wanatumia biblia ambayo wanasema imechakachuliwa na wanatumia calender ya warumi ambayo nawewe unaifuata
 
Unaseama biblia imebadilishwa alafu mda huo huo unai-quote tena hivi ndo vitimbi na vibweka
Fatilia naquote nini...biblia ya wakristo ndiyo ilibadilishwa.
Mi ninaquote biblia ya kiyahudi kupitia agano la kale.
 
Back
Top Bottom