Ukristo unahubiri upendo, je huu ni upendo wa aina gani? Au huu ni Ukristo wa aina gani?

Ukristo unahubiri upendo, je huu ni upendo wa aina gani? Au huu ni Ukristo wa aina gani?

Ninadhani walikuwa wanabatizwa.
'he is not dead'... hajafa ili azikwe pamoja na Kristo ili baadae anyanyuke akiwa kiumbe kipya katika Kristo.
Acha kutetea ujinga. Ubatizo unazamishwa kwenye maji ndio maana Yohana alibatiza Yordani na sio hekaluni.

Waganga wa kienyeji ndio hufanya hizo mambo.
 
Ukiangalia kwa jicho la kibinadamu utaona pastor anachapa bakora waumini

Ila kwa jicho la kiroho ni pastor anachapa bakora mapepo yaliyowaingia waumini

Shalom
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Unaona kabisa mtu anapigwa bakora ila kwa kuwa umekuwa brain washed unaambiwa ni mapepo nawe unakubali
Endelea kumtumikia huyo mchapa bakora.
 
DHAMBI ISIYOSAMEHEKA.

“Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa KUMKUFURU ROHO HAWATASAMEHEWA.” 12:3Mathayo
yan kama ulikua kwenye kichwa changu nilitaka niseme hivi hivi.
The God of thuggery
The God of threats
[emoji117]Note:...he never existed.

Msipagaishwe na hayo matapeli yajipayo vyeo kama vile, wachungaji, manabii, wainjilisti, walimu wa Neno, mashekhe, mitume, haya yote ni matapeli yanayofanya kazi chini ya kiumbe mmoja anayemiliki dini zote, na huyu kiumbe ndye anayewapa wafuasi wa hizi imani, yale mafeelings(hisia) za kuhisi uwepo/uoga wa dini na kujazwa ujinga kichwani.

Hao wanaofanyia miujiza makanisan nao ni waganga tu, tofaut na hawa waganga wa mitaani na maporini, ni kuwa hao wamejipa majina mazuri na kuwaponda hawa waganga wenzao wasiotumia utapel wa majina na magenge ya jumapil,ijumaa&jmos.

AmkeniiiView attachment 2093288

lakini hiii mtu namuurumia na yule anayesema mungu hayupo

unasema mungu hayupo kwa kisa cha kulisha watu 5000 na ety saiv kuna watu maskini jua moja mungu hampi mtu mapito asiyo yaweza kamwe bora uamini mungu yupo kuliko kutoamini na kumkuta yupo utasaga meno alaaah

WE ENDELEA KUSEMA NOT EXIST TUMEPIGWA KUMBE UNEPIGWA NA SHETANI
 
Tukiachana na hiyo video ambayo sijaiona tuongelee kuchapa...hivi unapomchapa mwanao maana yake humpendi?
Ww nawe hujui tofauti ya kuchapa mtoto akikosea na kumchapa muumini? Muumini kakosea Nini au kaiba sadaka unataka asirudie Tena? Kuwa na maarifa ili usidhalilishwe na shetani hadharani.
 
Mafundisho ya dini ya Kikristo yamejikita zaidi kwenye upendo, kwani ndio amri iliyo kuu kama tulivyo agizwa na Bwana wetu Yesu Kristo.

Miongoni mwa mistari inayo onyesha kiwango cha hali ya juu cha upendo ni ule unaosema tusamehe saba mara sabini. Pia upo ule mstari unaosema ukipigwa shavu la kushoto, geuza na la pili.

Sasa hebu tazama hiyo video, kisha tujadili, ni nini kimetokea? Je huyu anayepiga wenzake na ni kiongozi wa kanisa anasimamia andiko kutoka mstari gani?

Je, huu ni upendo wa namna gani?
Mbona hukuwai kushangaa wakatoliki wakipigwa makofi wakati wa kipaimara? Ni mifumo tu ya ibada
 
Ww nawe hujui tofauti ya kuchapa mtoto akikosea na kumchapa muumini? Muumini kakosea Nini au kaiba sadaka unataka asirudie Tena? Kuwa na maarifa ili usidhalilishwe na shetani hadharani.
Wewe ndio unajidhalilisha, wapi nimetaja mtoto? Wapi nimetaja muumini. Hem ficha upumbavu wako
 
Mafundisho ya dini ya Kikristo yamejikita zaidi kwenye upendo, kwani ndio amri iliyo kuu kama tulivyo agizwa na Bwana wetu Yesu Kristo.

Miongoni mwa mistari inayo onyesha kiwango cha hali ya juu cha upendo ni ule unaosema tusamehe saba mara sabini. Pia upo ule mstari unaosema ukipigwa shavu la kushoto, geuza na la pili.

Sasa hebu tazama hiyo video, kisha tujadili, ni nini kimetokea? Je huyu anayepiga wenzake na ni kiongozi wa kanisa anasimamia andiko kutoka mstari gani?

Je, huu ni upendo wa namna gani?
Kwa ufupi Ukristo unafundisha USHIRIKINA. Kielimu hakuna atakae pinga hili.
 
Acha kutetea ujinga. Ubatizo unazamishwa kwenye maji ndio maana Yohana alibatiza Yordani na sio hekaluni.

Waganga wa kienyeji ndio hufanya hizo mambo.
Je, uliona neno 'ninadhani'.
Kutokana na mapokeo ya hao watumishi wa Mungu, batizo zishakuwa nyingi zaidi ya hiyo ya kuzamishwa katika maji mengi.
Watu wanabatizwa kwa kuchapwa viboko kama hao kwenye picha mjongeo, kwa kuruka moto, kwa barua, kwa kunyunyiziwa maji kichwani n.k.
Kwa kulisoma neno kwa ufahamu timilifu, muumini wa imani hiyo atafahamu kutenganisha mchele na chuya.
 
Kuweka neno kudhani haiondoi ukweli kuwa unajaribu kutetea ujinga. Nani kwenye Biblia alibatiza kwa viboko? Hata Neno ubatizo lina maana kuzamisha kwenye maji sio kuwachabanga watu mboko!

Waganga wa kienyeji ndio huchapa watu na mikia ya ng'ombe au mbuzi. Kwa hiyo anachokifanya kinafanana na uganga wa kienyeji na sio ubatizo
 
Unajua ukiwa mjinga ni mjinga huwezi kuelewa mkristo/christian maana yake anayokana na kristo/christ au mfuasi wa kristo/christ sasa jina la kristo asili yake ni mashariki ya kati?
Ngoja nikuache tu. Hujui unachokisema ila unajifanya unajua sana. Endelea kuogelea na kuruka ruka kwenye ujinga wako
 
Alafu watatezi wa haki za binadamu na unyanyasaji wanaangalia tu wapo kimya...
 
Ukiangalia kwa jicho la kibinadamu utaona pastor anachapa bakora waumini

Ila kwa jicho la kiroho ni pastor anachapa bakora mapepo yaliyowaingia waumini

Shalom
We bana wewe,
 
Back
Top Bottom