Ukubwa gani wa madirisha ambao hupendezesha nyumba?

Futi 5 sio sawa na mita 1.7
Madirisha mazuri na yatayopendeza yawe na urefu wa futi 7(course 8) na yawe na upana wa futi 5(sawa na mita 1.5)
Uliza swali lolote la ujenzi nitakujibu kitaalamu zaidi.
Mimi ni contractor niliyeshindikana
Mkuu, msingi imara wa tofari unatakiwa ujengwe kwa kufuata kanuni zipi...!?
 
Fanya hivi
  • Ukishamaliza kuchimba msingi, mwaga zege chini
  • anza kujenga Msingi wako wa Tofali
  • Funga mkanda wa zege na nondo.


Fundi ramani yangu ni hii fundi kanambia tofari 4500. Ni hidden roof. Vipi hapa Countrywide sijapigwa??
 
Fanya hivi
  • Ukishamaliza kuchimba msingi, mwaga zege chini
  • anza kujenga Msingi wako wa Tofali
  • Funga mkanda wa zege na nondo.
Na vipi kama nikimwaga tu mchanga kwa kimo cha inchi 6-7 then nikaanza msingi?.

Malengo ni kupambana na nyufa zinazoanzia ardhini au kutokana na effect ya kutitia kwa udongo.
 
View attachment 1949366
Fundi ramani yangu ni hii fundi kanambia tofari 4500. Ni hidden roof. Vipi hapa Countrywide sijapigwa??
Hazitafika 4500
  • Msingi hapo zitaenda Tofali 1000(course 6)
  • Boma zitaenda Tofali 2700(course 17),
Za urembo tuweke 200 hivyo jumla ni Tofali 3900
Ila sikushauri utumie ramani hiyo. Ramani mbovu Sana hiyo.
Haiwezekani milango miwili ya chumbani ikawa na direct contact ya sitting room
Ilipaswa iwepo corridor kwa ajili ya kuficha vyumba
Hapohapo jiko nalo lina mlango wake ambao upo moja kwa moja na sebule
Narudia sikushauri utumie hiyo ramani, tafuta nyingine au mwambie aliyechora arekebishe
 
Futi 5 sio sawa na mita 1.7
Madirisha mazuri na yatayopendeza yawe na urefu wa futi 7(course 8) na yawe na upana wa futi 5(sawa na mita 1.5)
Uliza swali lolote la ujenzi nitakujibu kitaalamu zaidi.
Mimi ni contractor niliyeshindikana
Mkuu tunaomba utupatia picha ya ukuta wenye dirisha la futi 7 kwa 5.
 
Inategemea na mazingira uliyopo..
Maeneo ya baridi madirisha ni madoho na maeneo ya joto madirisha ni makubwa
 
Kwahiyo baada ya msingi, ukuta wa boma unakwenda kwa course 11 then linta, na baada ya linta zifuate course ngapi hadi kenchi kwa ramani ya paa la kawaida?.
 
Unatambua sana nini unakifanya, kwa hilo nakupa 5 Mkuu. Huku mtaani kuna mswahili kajenga ukuta umemega mipaka ya viwanja vinavyopakana, yaani kwa mtu smart lazima ujiulize, hivi hata mafundi wenyewe walikubali vipi kujenga ukuta ulio nje ya mipaka husika. Yaani ubavuni kamega si chini ya mita 2.5 ya eneo la mtu mwingine bila hata aibu.
 
Pia kadiri utakavyoweka madirisha makubwa ukumbuke kuwa wakati wa finishing gharama itakuwa kubwa pia!

Gharama za chuma (nondo, flat bars etc) zitakuwa kubwa, aluminum/PVC etc zitaongezeka pia , ufundi n.k.

Ni angalizo tu natoa kwa kila mhusika ajipange asijekuwa dis-appointed badae!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…