Ukubwa haupigi hodi, Mvi zimeanza kunitoka kwa wingi

Ukubwa haupigi hodi, Mvi zimeanza kunitoka kwa wingi

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Wasalaam.
Leo nimeamka mapema najiandaa kwenye kwenye mihangaiko. Sasa nimetoka kuoga nachana nywele, nikasema nisogee kwenye kioo, japo binafsi sina huo utamaduni wa kupenda vioo. Ile kujiangalia vizuri nakutana na mvi kibao sana huku kichwani, nikajua tu labda ni nyuzi ya Blanketi lakini kuangalia nakuta mvi kabisa kabisaa.

Nkaishia kutabasamu nakujisemea kwamba ninaanza kuzeeka sasa na siwezi kurudisha tena muda nyuma, kujiangalia vizuri nakuta hadi makunyanzi yameanza usoni. Nimeondoka nacheka tu maana juzi tu nilikuwa na kichwa cheusii na uso usio na makunyanzi mengi.

Leo nimewaza kwamba unaweza ukajihisi una muda mwingi sana na bado kijana, lakini uzee huwa haupigi hodi jamani....
 
Halafu ukubwa unakuja kirahisi sn
Kirahisi sana, mara ya mwisho nimekuja kule shuleni kwenu nilikuwa na kichwa cheusi balaa. Lakini leo hii nimebadilika sana sanaaa hadi najishangaa.
 
Back
Top Bottom