Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Sheria nyingi zimetungwa kulinda hadhi za viongozi kama kinga hususan hata wakiwa wapuuzi na majizi yanajitwika heshima na staha wasiyo stahili. Mnataka tuwaite waheshimiwa lakini hakuna hata heshima moja mnayostahili. Mnatumia mamlaka vibaya kukandamiza wananchi wanaohoji na kukosoa.
Kuhusu mkataba wa DP World ni wazi viongozi wamefanya upuuzi usiovumilika. Kugenisha misitu na mbuga zetu ni usaliti wa kipumbavu kabisa dhidi ya taifa letu
Mtasema natukana lakini hakuna jina zuri kwa mtu au watu wanaotuweka watanzania utumwani kwa tamaa za matumbo yao.
Yaani unalipwa mshahara kwa kodi zetu halafu ufanye madudu nikuheshimu?
Nyie polisi na wanadola mnaotumika kufanya ukandamizaji mjitafakari kwa sababu kila linalofanyika kinyume.cha Katiba na sheria dhidi ya taifa mtalipwa sawa sawa na kipimo mnachowajazia wanyonge.
Habari zenu bana