Ukubwa wa Singapore ni kama Wilaya ya Kigamboni tu lakini ina uchumi mkubwa sana

ward41

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2022
Posts
749
Reaction score
2,533


Ni jambo LA kusimitisha Sana kuona nchi ndogo kama Singapore ikiwa na uchumi mkubwa kuliko taifa lolote ndani ya bara LA Africa

Ukubwa wa Singapore ni kama tu wilaya ya kigamboni. Ina raia karibia million Sita

Uchumi wake ni gdp karibia 500 billion usd. Kwanini tunazidiwa na nchi ndogo kiasi hiki? Hii sasa ni too much
 
Jibu hoja why uchumi wa Singapore ni bora kuliko wa Tanzania?
 
kwaiyo unawashauri viongozi wetu wakuu waende wakajifunze Singapore
 
Hapo zenji muungano ukivunjika watatuzidi kiuchumi stay tuned...
 
Na tulipata uhuru kipindi kimoja.. . Tukaungana na znz kipindi ambacho wao waliungana na Malaysia
 

Kwani mtu mwenye pua kubwa anatoa kamasi nyingi?
 
Wametumia vizuri rasilimali yao ya bandari. Sisi tuna Tanzanite, Almasi, chuma, dhahabu, ardhi, mito, maziwa, wanyama, bahari, misitu, gesi, watu na zingine nyingi lakini tumeshindwa kuzitumia vizuri. Tungekuwa bado tupo chini ya mkoloni tungekuwa tumeendelea kuliko tulivyo sasa.
 
Nadharia za Mwl. Nyerere alituambia ili nchi iendelee inahitaji vitu vinne - ardhi, watu, siasa safi, na uongozi bora.

I think ilitakiwa iwe ardhi, watu, elimu bora, na uzalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…