Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
UKUMBI WA ARNAUTOGLO SAFARI NDEFU YA MWALIMU NYERERE ILIPOANZIA
George Arnautoglo alikuwa Mgiriki tajiri na ndiye aliyejenga jumba hilo akalitoa kwa matumizi ya Waafrika wa Tanganyika.
George Arnautoglo alikuwa hawapendi Waingereza kwa kuwa walikuwa wameikalia nchi yake Greece ambako Padri Makarios alikuwa akiongoza mapambano ya kudai uhuru.
Arnautoglo alipata kutoa fedha kwa siri kuwapa TANU zisaidie harakati za kudai uhuru na fedha hizi alimpa Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa mmoja wa viongozi wa juu wa TANU.
Kwenye Ukumbi huu wa Arnautoglo tarehe 17 April 1953 ulifanyika uchaguzi wa mwaka wa TAA kumchagua Rais na viongozi wengine.
Julius Kambarage Nyerere, mwalimu wa shule asiyefahamika sana kutoka Pugu alikuwa anagombea nafasi hiyo dhidi ya kijana maarufu wa Dar es Salaam na Kaimu Rais wa TAA na Katibu wake, mtoto wa mwanasiasa na mfanya biashara maarufu wakati wake, Kleist Sykes, Abdul akiwa Market Master Kariakoo Market.
Nyerere alishinda uchaguzi huu kwa kura chache sana.
Vipi Nyerere aliweza kumshinda Abdul Sykes siku ile ni kisa cha kusisimua katika historia ya Tanganyika na historia ya Mwalimu Nyerere.
Hapa kwenye jengo hili na siku ile ndipo Julius Nyerere alipoanza safari yake ndefu ya siasa na uongozi.
Hapa Nyerere alikuwa siku ile kavuka kiunzi kikubwa katika maisha yake ya siasa.
Meneja wa Ukumbi huu wa Arnautoglo ambae na yeye alishiriki katika kupiga kura ya kunyoosha mikono alikuwa kijana wa Kinyasa kutoka Nyasaland (Malawi) Dennis Pombeah.
Phombeah akiendesha pikipiki yake aina ya BSA alizunguka mji mzima kumfanyia Nyerere kampeni.
Abdul na wenzake katika TAA hawakufanya kampeni yoyote kwani walitaka Nyerere ashinde.
Imenichukua zaidi ya miaka 10 kutafuta picha ya Dennis Phombeah na mwisho nimeipata picha yake.
Dennis PhombeahPhombeah kama meneja wa Arnautoglo Hall kafanya mengi katika kuisaidia TAA hadi TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika historia ambayo si wengi wanaifahamu.
Lakini Dennis Pombeah alikuwa rafiki kipenzi wa Oscar Kambona...
Picha: Ukumbi wa Arnautoglo, Dennis Phomeah Menaja wa Arnautoglo na picha ya tatu kulia Nangwanda Lawi Sijaona, Abdulwahid Kleist Sykes, Julius Kambarage Nyerere na Waziri Dossa Aziz katika Ukumbi wa Arnautoglo kwenye dhifa ya kumuaga Rais wa TANU Julius Nyerere safari ya pili UNO 1957
George Arnautoglo alikuwa Mgiriki tajiri na ndiye aliyejenga jumba hilo akalitoa kwa matumizi ya Waafrika wa Tanganyika.
George Arnautoglo alikuwa hawapendi Waingereza kwa kuwa walikuwa wameikalia nchi yake Greece ambako Padri Makarios alikuwa akiongoza mapambano ya kudai uhuru.
Arnautoglo alipata kutoa fedha kwa siri kuwapa TANU zisaidie harakati za kudai uhuru na fedha hizi alimpa Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa mmoja wa viongozi wa juu wa TANU.
Kwenye Ukumbi huu wa Arnautoglo tarehe 17 April 1953 ulifanyika uchaguzi wa mwaka wa TAA kumchagua Rais na viongozi wengine.
Julius Kambarage Nyerere, mwalimu wa shule asiyefahamika sana kutoka Pugu alikuwa anagombea nafasi hiyo dhidi ya kijana maarufu wa Dar es Salaam na Kaimu Rais wa TAA na Katibu wake, mtoto wa mwanasiasa na mfanya biashara maarufu wakati wake, Kleist Sykes, Abdul akiwa Market Master Kariakoo Market.
Nyerere alishinda uchaguzi huu kwa kura chache sana.
Vipi Nyerere aliweza kumshinda Abdul Sykes siku ile ni kisa cha kusisimua katika historia ya Tanganyika na historia ya Mwalimu Nyerere.
Hapa kwenye jengo hili na siku ile ndipo Julius Nyerere alipoanza safari yake ndefu ya siasa na uongozi.
Hapa Nyerere alikuwa siku ile kavuka kiunzi kikubwa katika maisha yake ya siasa.
Meneja wa Ukumbi huu wa Arnautoglo ambae na yeye alishiriki katika kupiga kura ya kunyoosha mikono alikuwa kijana wa Kinyasa kutoka Nyasaland (Malawi) Dennis Pombeah.
Phombeah akiendesha pikipiki yake aina ya BSA alizunguka mji mzima kumfanyia Nyerere kampeni.
Abdul na wenzake katika TAA hawakufanya kampeni yoyote kwani walitaka Nyerere ashinde.
Imenichukua zaidi ya miaka 10 kutafuta picha ya Dennis Phombeah na mwisho nimeipata picha yake.
Dennis Phombeah