Ukumbi wa Arnautoglo safari ndefu ya Mwalimu Nyerere ilipoanzia

Ukumbi wa Arnautoglo safari ndefu ya Mwalimu Nyerere ilipoanzia

Mwanzi1,

Suala la dini lilikuwapo lakini udini haukuwapo.

Katika majadiliano ya Nansio Mwapachu alimwambia Abdul kuwa Nyerere
mbali ya sifa nyingine zilizomfanya yeye awe anafaa zaidi kuongoza harakati
za uhuru, yeye kama Mkristo hii itaondoa hofu kwa Waingereza.

Wakoloni hawataingalia TANU kama chama cha Waislam kinachotaka kuleta
vita kama ile ya Maji Maji mwaka wa 1905.
Really? Where is the friggin' evidence for this? He said/She said isn't objective and credible enough as you would like it, Mr. MS. Anybody, including yourself, can put words into people's mouths, so to speak. How are we to trust that these claims are the truth, and nothing but?
 
Kwa hiyo hapa unataka kusema huyo Abdul Sykes, al-wataan wa Kariakoo alishindwa sababu hakufanya kampeni, na Nyerere, Mwalimu fulani tu wa Pugu, alishinda sababu alifanya kampeni? Halafu hapohapo unadai Abdul Sykes alikuwa anataka Nyerere ashinde? Kwanza tuambie vote tally ilikuwaje, siyo kutuletea hadithi za "alishinda kwa kura chache sana". Ni dhahiri jinsi ambavyo una pindisha mambo kwa kuipendelea hiyo famila tukufu kwako wewe ya SYKES.
Ndjabu...
Ndugu yangu nakueleza siku zote kuwa ukiwa na ghadabu akili haiwezi kufanya
kazi vyema.

Hebu jaribu kunisoma upya hakuna mahali niliposema kuwa Abdul alishindwa
uchaguzi kwa kuwa hakufanya kampeni wala hakuna popote niliposema kuwa
Mwalimu alifanya kampeni.

Inawezekana hujasoma kuhusu mkutano uliofanyika nyumbani kwa Mwapachu
mwaka wa 1953 kati ya Mwapachu, Abdul na Ali Mwinyi Tambwe.

Msome Juma Mwapachu hapo chini ili ujue Nyerere vipi alikuja kuingia katika uongozi
wa TAA 1953:

''Juma Mwapachu alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Nansio, Ukerewe wakati
Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walipokwenda Nansio mwaka wa 1953 kumuona
baba yake, Hamza Kibwana Mwapachu kuhusu uchaguzi wa TAA wa mwaka huo
uliokuwa ufanyike miezi michache mbele.

Abdul Sykes alikuwa anataka kauli ya mwisho kutoka kwa Mwapachu kuhusu Nyerere
kuwa ndiyo Hamza hajabadili fikra yake na anamtaka Abdul ampishe Nyerere katika nafasi
ya urais wa TAA?

Hamza Mwapachu alirejea katika fikra yake na akamueleza Abdul kuwa Nyerere achukue
nafasi ya urais na mwaka ujao, 1954 iundwe TANU.''

Juma Mwapachu kashuhudia haya kwa macho yake hakuhadithiwa.

Juma Mwapachu kasoma niliyoandika kuhusu historia ya TANU na hayo hapo chini ndiyo maneno aliyoniandikia:

''Mohamed naafiki kabisa na maelezo yako.''

Uchaguzi huu ulikuwa wa kunyoosha mikono na nimeueleza vizuri katika kitabu cha Sykes
kuwa hakuna ''tallying,'' wala Nyerere hajaeleza kuwa aligombea nafasi ya urais wa TAA na
Abdul wala kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni hakikueleza uchaguzi huu achilia mbali kule
kulitaja jina la Abdul.

Ningetegemea ungehangaishwa na haya si kuhangaishwa na mie ninapokuandikia ukweli.
Listowel kaeleza uchaguzi huu na kasema Nyerere alishinda kwa tabu.

'
 
Ndjabu...
Ndugu yangu nakueleza siku zote kuwa ukiwa na ghadabu akili haiwezi kufanya
kazi vyema.

Hebu jaribu kunisoma upya hakuna mahali niliposema kuwa Abdul alishindwa
uchaguzi kwa kuwa hakufanya kampeni wala hakuna popote niliposema kuwa
Mwalimu alifanya kampeni.

Inawezekana hujasoma kuhusu mkutano wa uliofanyika nyumbani kwa Mwapachu
mwaka wa 1953 kati ya Mwapachu, Abdul na Ali Mwinyi Tambwe.

Msome Juma Mwapachu hapo chini ili ujue Nyerere vipi alikuja kuingia katika uongozi
wa TAA 1953:

''Juma Mwapachu alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Nansio, Ukerewe wakati
Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe walipokwenda Nansio mwaka wa 1953 kumuona
baba yake, Hamza Kibwana Mwapachu kuhusu uchaguzi wa TAA wa mwaka huo
uliokuwa ufanyike miezi michache mbele.

Abdul Sykes alikuwa anataka kauli ya mwisho kutoka kwa Mwapachu kuhusu Nyerere
kuwa ndiyo Hamza hajabadili fikra yake na anamtaka Abdul ampishe Nyerere katika nafasi
ya urais wa TAA?

Hamza Mwapachu alirejea katika fikra yake na akamueleza Abdul kuwa Nyerere achukue
nafasi ya urais na mwaka ujao, 1954 iundwe TANU.

Juma Mwapachu kashuhudia haya kwa macho yake hakuhadithiwa.

Juma Mwapachu kasoma niliyoandika kuhusu historia ya TANU na hayo hapo chini ndiyo maneno aliyoniandikia:

''Mohamed naafiki kabisa na maelezo yako.

Uchaguzi huu ulikuwa wa kunyoosha mikono na nimeueleza vizuri katika kitabu cha Sykes
kuwa hakuna ''tallying,'' wala Nyerere hajaeleza kuwa aligombea nafasi ya urais wa TAA na
Abdul wala kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni hakikueleza uchaguzi huu achilia mbali kule
kulitaja jina la Abdul.

Ningetegemea ungehangaishwa na haya si kuhangaishwa na mie ninapokuandikia ukweli.
Listowel kaeleza uchaguzi huu na kasema Nyerere alishinda kwa tabu.

'
Kama ulikuwa ni uchaguzi wa kunyoosha mikono, hizo kura chache zilizomwezesha Nyerere kushinda, zilipatikana kwa ukaguzi wa macho tu? Vilevile, implicit kwenye bandiko lako ni kwamba Nyerere alishinda kwa taabu sababu kuna watu walimfanyia kampeni, lakini Sykes kama na yeye angefanya kampeni ili kweli washindane basi angeshinda ushindi wa tsunami, lakini ni kwa vile tu hakutaka kushinda.
 
Really? Where is the friggin' evidence for this? He said/She said isn't objective and credible enough as you would like it, Mr. MS. Anybody, including yourself, can put words into people's mouths, so to speak. How are we to trust that these claims are the truth, and nothing but?
Ndjabu...
Hii ndiyo moja ya maajabu ya historia hii kuwa inaghadhibisha baadhi ya watu
na inawafurahisha baadhi.

Chuo Cha CCM Kivukoni kimeandika historia hii na hakuna aliyeghadhibika mimi
nimekisoma kitabu wala sikughadhibika.

Niliamua kuandika historia hiyo hiyo ya TANU kama ninavyoifahamu kwa bahati
mbaya wako wanaoghadhibika sasa mwaka wa 20.

Ndjabu sasa ananimwagia Kizungu.

Hapa namkumbuka Maalim wangu Sheikh Haruna aliyenifunza ilm ya mnakasha
akanifunza adabu za majadiliano na dalili za mtu anaishindwa.

Akanifunza pia na jinsi ya kukabiliana na kila aina ya vitimbi vya mshindwaji.

Sasa Ndjabu anamwaga Kimombo anadai ushahidi kwa Kiingereza.

Hamwamini Juma Mwapachu wala Judith Listowel wala haamini Nyaraka za
Sykes.

Lakini kwa faida ya wale wanaofuatilia mjadala nitaweka hapa rejea ya Listowel
''The Making of Tanganyika,'' Chatto and Windus, London,1965, uk wa 221 kasema,
''...Nyerere won by a very small margin.''

Uchaguzi huu wa 1953 wa TAA uko katika Tanganyika Standard la 19 June, 1953
katika gazeti hili viongozi wa uchaguzi ule uliofanyika Arnautoglo wote wametajwa.

Lakini mimi nataka kumtua mzigo Ndjabu...
Si lazima kuiamini historia hii katika kitabu cha Sykes.

Anaweza kuamini kuwa mimi ni ''mrongo.''

Anaweza pia kuamini hapakuwa na uchaguzi wa TAA wa 1953 baina ya Abdul na
Nyerere.

Anaweza pia akaamini kuwa yote niliyosema kuhusu Hamza Mwapachu ni ''urongo.''

Ana haki zote kuamini kuwa historia ya TANU ya kuaminika ni ile ya Chuo Cha CCM
Kivukoni.
 
Kwa hiyo hapa unataka kusema huyo Abdul Sykes, al-wataan wa Kariakoo alishindwa sababu hakufanya kampeni, na Nyerere, Mwalimu fulani tu wa Pugu, alishinda sababu alifanya kampeni? Halafu hapohapo unadai Abdul Sykwes alikuwa anataka Nyerere ashinde? Kwanza tuambie vote tally ilikuwaje, siyo kutuletea hadithi za "alishinda kwa kura chache sana". Ni dhahiri jinsi ambavyo una pindisha mambo kwa kuipendelea hiyo famila tukufu kwako wewe ya SYKES.
Tujikumbeshe ili tuwaelewe vyema hawa tunaowasoma katika historia hii:

Nimesoma kila kitabu kinachohusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nimesoma kila kitabu kilichoandikwa kuhusu Mwalimu Nyerere.

Ikiwa kuna vilivyonipita vitakuwa vichache sana.

Katika vitabu vya historia vilivyoandika historia inayokaribia ukweli ni cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika,'' (1965).

Vitabu vyote vilivyobakia hakuna kitu.

Lady Judith Listowel alikuwa mke wa Lord Listowel aliyekuwa Gavana wa Gold Coast kutoka 1957 - 1960.

Huyu mama alitaka kuandika kitabu kuhusu Tanganyika kwa hiyo akamwomba Peter Colmore amuunganishe na wapigania uhuru wa Tanganyika wamsaidie katika utafiti wake.

Peter Colmore na Ally Sykes walikuwa marafiki wakubwa sana na mapatna katika biashara na walifahamiana Nairobi toka mwaka wa 1942 wakati wa WWII wote wawili wakiwa wanajeshi vijana katika KAR.

Siku zile Waingereza wote walikuwa wakitaka kufanya jambo Afrika ya Mashariki mtu wao wa kuwafagilia njia na kuwafungulia milango alikuwa Peter Colmore.

Colmore alikuwa anaushawishi mkubwa sana kwa viongozi wa Afrika ya Mashariki na alikuwa rafiki wa karibu sana wa Kabaka Edward Mutesa.

Colmore alikuwa na urafiki na viongozi wengi wa Afrika ya Mashariki ila Mwalimu Nyerere licha ya juhudi ya Ally Sykes kumkutanisha Colmore kwa kumpeleka nyumbani kwa Mwalimu, Magomeni.

Colmore alipata mwaliko wa kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika December 1961 kupitia mgongo wa Ally Sykes.

Kabaka Mutesa alisoma darasa moja na Abbas Sykes, King's College Budo.

Nimeuleta huu mukadama, yaani utangulizi mrefu ili uweze kujua ilikuwaje Listowel aliweza kuingia Tanganyika na kufanya mazungumzo na wapigania uhuru wengi na kupata ukweli wa historia ya TANU.

Hapa Tanganyika Colmore mwenyeji wake alikuwa Ally Sykes na ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuzungumzanae kuhusu harakati za uhuru wa Tanganyika.

Hii ndiyo sababu kwenye kitabu chake Dossa Aziz katajwa pamoja na wazalendo wengi kama Dr. Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Sheikh Suleiman Takadir, Schneider Plantan kwa kuwataja wachache.
 
Bibi yangu aliniambia kuwa Anatoglo ilikuwa ni mahali pa matembezi kama night club vile pakipigwa miziki
 
Bibi yangu aliniambia kuwa Anatoglo ilikuwa ni mahali pa matembezi kama night club vile pakipigwa miziki
Akilinjema,
Hapana haikuwa night club ilikuwa Community Centre.

Kulikuwa na ukumbi ambao Waafrika wakiutumia kwa shughuli nyingi za kijamii kama harusi, mikutano nk. na pakipigwa dansi vilevile.

Kulikuwa na sehemu vijana wakifanya michezo ya masumbwi na karate.

Kwa ufupi Arnautoglo palikuwa sehemu ya mambo mengi ila haikupata kuwa night club.
 
Tujikumbeshe ili tuwaelewe vyema hawa tunaowasoma katika historia hii:

Nimesoma kila kitabu kinachohusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Nimesoma kila kitabu kilichoandikwa kuhusu Mwalimu Nyerere.

Ikiwa kuna vilivyonipita vitakuwa vichache sana.

Katika vitabu vya historia vilivyoandika historia inayokaribia ukweli ni cha Judith Listowel, ''The Making of Tanganyika,'' (1965).

Vitabu vyote vilivyobakia hakuna kitu.

Lady Judith Listowel alikuwa mke wa Lord Listowel aliyekuwa Gavana wa Gold Coast kutoka 1957 - 1960.

Huyu mama alitaka kuandika kitabu kuhusu Tanganyika kwa hiyo akamwomba Peter Colmore amuunganishe na wapigania uhuru wa Tanganyika wamsaidie katika utafiti wake.

Peter Colmore na Ally Sykes walikuwa marafiki wakubwa sana na mapatna katika biashara na walifahamiana Nairobi toka mwaka wa 1942 wakati wa WWII wote wawili wakiwa wanajeshi vijana katika KAR.

Siku zile Waingereza wote walikuwa wakitaka kufanya jambo Afrika ya Mashariki mtu wao wa kuwafagilia njia na kuwafungulia milango alikuwa Peter Colmore.

Colmore alikuwa anaushawishi mkubwa sana kwa viongozi wa Afrika ya Mashariki na alikuwa rafiki wa karibu sana wa Kabaka Edward Mutesa.

Colmore alikuwa na urafiki na viongozi wengi wa Afrika ya Mashariki ila Mwalimu Nyerere licha ya juhudi ya Ally Sykes kumkutanisha Colmore kwa kumpeleka nyumbani kwa Mwalimu, Magomeni.

Colmore alipata mwaliko wa kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika December 1961 kupitia mgongo wa Ally Sykes.

Kabaka Edward Mutesa udogoni kwake alisoma darasa moja na Abbas Sykes, King's College Budo .

Nimeuleta huu mukadama, yaani utangulizi mrefu ili uweze kujua ilikuwaje Listowel aliweza kuingia Tanganyika na kufanya mazungumzo na wapigania uhuru wengi na kupata ukweli wa historia ya TANU.

Hapa Tanganyika Colmore mwenyeji wake alikuwa Ally Sykes na ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuzungumzanae kuhusu harakati za uhuru wa Tanganyika.

Hii ndiyo sababu kwenye kitabu chake Dossa Aziz katajwa pamoja na wazalendo wengi kama Dr. Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Sheikh Suleiman Takadir, Schneider Plantan kwa kuwataja wachache.
 
Arnautoglo Hall ndo ukumbi gani huo maana sijawahi sikia jina hilo bado upo kwa jina hilo ....
 
Historia nzuri ila kama imeishia pazuri,hakuna mwendelezo mkuu?
 
Historia nzuri ila kama imeishia pazuri,hakuna mwendelezo mkuu?
Ndumbula,
Tukisema tuandike yote tutakaa hapa jamvini hata miaka 3 hatujainuka.

Historia yote ipo ndani ya kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.
 
Sasa kama walitaka Nyerere ashinde uchaguzi ule kwannn alishindana naye sasa?
Vempire,
Swali hili nimelijibu huko nyuma juma lililopita na limezua mjadala mkali.

Pitia post za nyuma.
 
UKUMBI WA ARNAUTOGLO SAFARI NDEFU YA MWALIMU NYERERE ILIPOANZIA

George Arnautoglo alikuwa Mgiriki tajiri na ndiye aliyejenga jumba hilo akalitoa kwa matumizi ya Waafrika wa Tanganyika.

George Arnautoglo alikuwa hawapendi Waingereza kwa kuwa walikuwa wameikalia nchi yake Greece ambako Padri Makarios alikuwa akiongoza mapambano ya kudai uhuru.

Arnautoglo alipata kutoa fedha kwa siri kuwapa TANU zisaidie harakati za kudai uhuru na fedha hizi alimpa Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa mmoja wa viongozi wa juu wa TANU.

Kwenye Ukumbi huu wa Arnautoglo tarehe 17 April 1953 ulifanyika uchaguzi wa mwaka wa TAA kumchagua Rais na viongozi wengine.

Julius Kambarage Nyerere, mwalimu wa shule asiyefahamika sana kutoka Pugu alikuwa anagombea nafasi hiyo dhidi ya kijana maarufu wa Dar es Salaam na Kaimu Rais wa TAA na Katibu wake, mtoto wa mwanasiasa na mfanya biashara maarufu wakati wake, Kleist Sykes, Abdul akiwa Market Master Kariakoo Market.

Nyerere alishinda uchaguzi huu kwa kura chache sana.

Vipi Nyerere aliweza kumshinda Abdul Sykes siku ile ni kisa cha kusisimua katika historia ya Tanganyika na historia ya Mwalimu Nyerere.

Hapa kwenye jengo hili na siku ile ndipo Julius Nyerere alipoanza safari yake ndefu ya siasa na uongozi.

Hapa Nyerere alikuwa siku ile kavuka kiunzi kikubwa katika maisha yake ya siasa.

Meneja wa Ukumbi huu wa Arnautoglo ambae na yeye alishiriki katika kupiga kura ya kunyoosha mikono alikuwa kijana wa Kinyasa kutoka Nyasaland (Malawi) Dennis Pombeah.

Phombeah akiendesha pikipiki yake aina ya BSA alizunguka mji mzima kumfanyia Nyerere kampeni.

Abdul na wenzake katika TAA hawakufanya kampeni yoyote kwani walitaka Nyerere ashinde.

Imenichukua zaidi ya miaka 10 kutafuta picha ya Dennis Phombeah na mwisho nimeipata picha yake.

Phombeah kama meneja wa Arnautoglo Hall kafanya mengi katika kuisaidia TAA hadi TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika historia ambayo si wengi wanaifahamu.

Lakini Dennis Pombeah alikuwa rafiki kipenzi wa Oscar Kambona...
cc Mzee Said
 
Mwanzi1,

Suala la dini lilikuwapo lakini udini haukuwapo.

Katika majadiliano ya Nansio Mwapachu alimwambia Abdul kuwa Nyerere
mbali ya sifa nyingine zilizomfanya yeye awe anafaa zaidi kuongoza harakati
za uhuru, yeye kama Mkristo hii itaondoa hofu kwa Waingereza.

Wakoloni hawataiangalia TANU kama chama cha Waislam kinachotaka kuleta
vita kama ile ya Maji Maji mwaka wa 1905.
Khee, vita ya majimaji ilikuwa na uhusiano na uislam?! Au nimesoma vibaya hiyo sentensi!
 
Khee, vita ya majimaji ilikuwa na uhusiano na uislam?! Au nimesoma vibaya hiyo sentensi!
Gagnija,
Umesoma sawasawa.
Naingia Maktaba In Shaa Allah itakuwekea historia hiyo.

1148337

Kwa miaka mingi sana na hadi leo jina la Sultani wa Wangoni Abdulrauf Songea Mbano Jemedari wa Wangoni katika Vita ya Majimaji, jina lake la ‘’Abdulrauf’’ moja ya sifa za Allah ikiwa na maana ‘’Mwenye Huruma,’’ lilikuwa halifahamiki kwa wengi na wanahistoria kwa sababu zao hawakutaka kulisema lijulikane kama vile wengi hawajui kuwa Sultani Mkwawa jina lake ni ''Abdallah.''

Tukija katika historia ya miaka ya karibuni zaidi si wengi wenye kujua kuwa Kleist Sykes jina lake ni Abdallah, au Schneider Plantan jina lake ni ''Abdillah.''

Tunaweza tukasema kuwa haya yote ni matatizo ya ukoloni. Lakini swali linakuja iweje hata baada ya ukoloni kutoweka ikabakia historia yetu hatuiweki sawa?

Leo gazeti la ''Habari Leo,'' (28 Februari, 2018) ukurasa wa mbele imetoka picha ya kaburi la Sultani Abdulrauf Songea Mbano jina linalosomeka katika kaburi hilo ambalo ni la Kiislam ni ‘’Songea Mbano,’’ na jina lake halisi ''Abdulrauf,'' halipo.

Laiti kama Sultani Abdulrauf asingezikwa katika kaburi la Kiislam mengi katika historia ya Majimaji yasingelipata ushahidi madhubuti ukizingatia kuwa katika wale majemedari walionyongwa na Wajerumani, majina yao ya Kiislam yalifutwa yakawekwa mengine.

Atakae kusoma zaidi kuhusu historia hii aingie hapo chini:
  1. http://www.mohammedsaid.com/2016/06/chief-abdul-rauf-bin-songea-mmoja-wa.html
  2. http://www.mohammedsaid.com/2015/03/kutoka-jf-majemadari-wa-vita-vya-maji.html
  3. http://www.mohammedsaid.com/2015/03/kutoka-jf-uchakachuaji-wa-majina-ya.html
  4. http://www.mohammedsaid.com/2015/02/marehemu-sheikh-ilunga-hassan-kapungu.html
1148338
 
Gagnija,
Umesoma sawasawa.
Naingia Maktaba In Shaa Allah itakuwekea historia hiyo.

Tukija katika historia ya miaka ya karibuni zaidi si wengi wenye kujua kuwa Kleist Sykes jina lake ni Abdallah, au Schneider Plantan jina lake ni ''Abdillah.''
Unamuongelea huyu aliyekuwa Meya Dar, au babu yake! Na huyu Schneider waweza weka historia yake kidogo?
 
Back
Top Bottom