Really? Where is the friggin' evidence for this? He said/She said isn't objective and credible enough as you would like it, Mr. MS. Anybody, including yourself, can put words into people's mouths, so to speak. How are we to trust that these claims are the truth, and nothing but?
Ndjabu...
Hii ndiyo moja ya maajabu ya historia hii kuwa inaghadhibisha baadhi ya watu
na inawafurahisha baadhi.
Chuo Cha CCM Kivukoni kimeandika historia hii na hakuna aliyeghadhibika mimi
nimekisoma kitabu wala sikughadhibika.
Niliamua kuandika historia hiyo hiyo ya TANU kama ninavyoifahamu kwa bahati
mbaya wako wanaoghadhibika sasa mwaka wa 20.
Ndjabu sasa ananimwagia Kizungu.
Hapa namkumbuka Maalim wangu
Sheikh Haruna aliyenifunza ilm ya mnakasha
akanifunza adabu za majadiliano na dalili za mtu anaishindwa.
Akanifunza pia na jinsi ya kukabiliana na kila aina ya vitimbi vya mshindwaji.
Sasa
Ndjabu anamwaga Kimombo anadai ushahidi kwa Kiingereza.
Hamwamini
Juma Mwapachu wala
Judith Listowel wala haamini
Nyaraka za
Sykes.
Lakini kwa faida ya wale wanaofuatilia mjadala nitaweka hapa rejea ya
Listowel
''The Making of Tanganyika,'' Chatto and Windus, London,1965, uk wa 221 kasema,
''..
.Nyerere won by a very small margin.''
Uchaguzi huu wa 1953 wa TAA uko katika
Tanganyika Standard la 19 June, 1953
katika gazeti hili viongozi wa uchaguzi ule uliofanyika Arnautoglo wote wametajwa.
Lakini mimi nataka kumtua mzigo
Ndjabu...
Si lazima kuiamini historia hii katika kitabu cha
Sykes.
Anaweza kuamini kuwa mimi ni ''mrongo.''
Anaweza pia kuamini hapakuwa na uchaguzi wa TAA wa 1953 baina ya
Abdul na
Nyerere.
Anaweza pia akaamini kuwa yote niliyosema kuhusu
Hamza Mwapachu ni ''urongo.''
Ana haki zote kuamini kuwa historia ya TANU ya kuaminika ni ile ya Chuo Cha CCM
Kivukoni.