Tajiri mpole
JF-Expert Member
- Apr 15, 2018
- 2,890
- 5,632
Mzee tuwekee nasisi hiyo picha ya Mzee Pombe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ally ni marehemu, alikuwa jirani pale mbezi beach, nyumbani yake ipo ufukweni kabisa.Kingsmann,
Historia ya TANU ni tamu sana na inasisimua.
Namshukuru siku zote Bwana Ally Sykes kwa kunifungulia nyaraka
zake na kunipa mimi fursa ya kuzisoma na pia kumhoji.
Inasikitisha sana kuwa wenye nyaraka hizi wamezuia zisisomwe na
umma.
Hivi mbezi beach inaanzia wapi na kuishia wapi!Ally ni marehemu, alikuwa jirani pale mbezi beach, nyumbani yake ipo ufukweni kabisa.
Alipenda kuandaa sherehe za mwisho wa mwaka, mtu mmoja mchangamfu na asiyejikweza.
Alikuwa na spirit kama ya Bakhresa, kama usipotambulishwa na anayemfahamu usingeweza kumjua.
Inaanzia pale maringo ukikata kona inayoelekea rainbow, inaishia pale kwenye kipita shoto cha kuelekea afrikana. .Hivi mbezi beach inaanzia wapi na kuishia wapi!
Hotel Africana, zamani jioni tukimsikia simba akiunguruma hapo.Inaanzia pale maringo ukikata kona inayoelekea rainbow, inaishia pale kwenye kipita shoto cha kuelekea afrikana. .
Eneo lote kutoka pale darajani lugalo upande wako wa kulia kuelekea baharini ni mbezi beach, mpaka unapokutana na ile barabaraba inayotoka katika kile kipita shoto nilichokitaja hapo juu.
Tanu ndio ccm mfumo ni uleule. Nyumba mbovu juu ya msingi mbovu....Kituko kingine hichi yani mshindani hakupiga kampeni makusudi ili mtu mwingine ashinde [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Phillipo,Ally ni marehemu, alikuwa jirani pale mbezi beach, nyumbani yake ipo ufukweni kabisa.
Alipenda kuandaa sherehe za mwisho wa mwaka, mtu mmoja mchangamfu na asiyejikweza.
Alikuwa na spirit kama ya Bakhresa, kama usipotambulishwa na anayemfahamu usingeweza kumjua.
Mjukuu wa Ally ni mdogo wetu pale Mbezi Beach, amekua tunamuona. Mwanae ndio mwenye ile travel agency iliyopo katika huu mtaa unaoanzia round about ya iliyokuwepo bilicanas unakuja kumalizia ile round about ya karibu na ule msikiti ulio karibu na hindu mandal (nadhani unaitwa Idrissa).Phillipo,
Mzee Ally alikutana na Tito Mbuwane katika mkutano Afrika ya Kusini.
Tito Mbuwane alikuwa waziri katika serikali ya Mandela.
Ally Sykes akamwambia Tito Mbuwane kuwa na yeye ni Mbuwane akamtajia majina yake yote - Ally Kleist Sykes Mbuwane akamweleza historia ya babu yake Sykes Mbuwane.
Tito Mbuwane akawa na mashaka na historia ile akihofu labda ni mbinu za Watanzania kutaka kumptapeli kwa hiyo akafanya check ya haraka na mtu mmoja anaemwamini.
Tito akaelezwa kuwa yote aliyoambiwa ni kweli kisha yule mpashaji habari akamwambia, "Ally Sykes hapo aliposimama anaweza kununua nyumba zote za huu mtaa."
Sebago,Sikuwahi kufahamu Kua uwanja wa Nangwanda Sijaona ni jina la mtu
shukrani Sana Kiongozi, madini haya tunayapata JF pekee, ipo haja ya haya mambo kuingizwa kwenye mitaala ya elimu wanafunzi wapate kuyajuaSebago,
Lawi Nangwanda Sijaona ni katika wapigania uhuru wa Tanganyika toka
wakati wa TAA hadi TANU.
Unaweza kusoma historia yake katika siasa ndani ya kitabu cha Abdul
Sykes (1998):
View attachment 1164624
Kulia ni Lawi Nangwanda Sijaona, Abdulwahid Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz
katika hafka ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1957 Ukumbi wa Arnautoglo
Sebago historia hii inatia hofu kwa hiyo inaonekana bora isifahamike kwa hiyo haiwezi kuitwa katika mtaala.shukrani Sana Kiongozi, madini haya tunayapata JF pekee, ipo haja ya haya mambo kuingizwa kwenye mitaala ya elimu wanafunzi wapate kuyajua
shukrani Sana Kiongozi, madini haya tunayapata JF pekee, ipo haja ya haya mambo kuingizwa kwenye mitaala ya elimu wanafunzi wapate kuyajua
upload mzeeMohamed Said yupo sahihi kuhusu uchaguzi. Nimemsikiliza marehemu Ally Kleist Sykes amefafanua vizuri sana katika kipindi cha Maktaba yetu TBC. Amepita mle mle Ninayo crip yake ntaiupload