Ukumbi wa Papa: Ndiyo Utambulisho wa yule Nyoka wa Eden?

Tunapozungumzia kuruhusu ubongo ujifunze kitu kipya tuna maana kuna possibility kubwa kukutana na mambo ambayo yanakinzana na imani yako?
 
Nimekuelewa mkuu tatizo sisi binadamu wengi wao hatupendi kusoma kuchambua kwa nini hiki kiko hivi, kwa nini dunia moja na Mungu mmoja na dini zipo zaidi ya 10,000/= duniani kote, tunapenda kushikilia kile tukiaminicho na sio kutafuta tafuta na kujifunza kwa nini hii hiko hivi, hii ndiyo maana tunapenda kutafuniwa na sisi kazi yetu ni kumeza tu, ujiulizi ni nini hiki ninachomeza, Asante mkuu nilikuwa sijui na sasa nimejua nimegain kitu kutoka kwenye mada hii, mimi huwa ninapenda kufanya upembenuvi au kutafiti na kuelewa jambo siyo mtu wa kutafutiwa tu na kupewa halafu wewe unaitikia ndiyo mzee!!
Nasema tena asante mkuu mimi nimezaliwa katoliki na kukulia huko lakini leo nimejifunza kitu kutoka kwenye hekalu hili la Papa. Nasema asante sana na Mungu awe pamoja nawe ni raha sana jamiiforum!!
 
Jibu linapatikana katika Ufunuo 13:2, "yule Joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi."


Angalia ya kwamba MAMLAKA yake inatoka kwa JOKA. Lakini Joka huyu ni nani?

Ufunuo 12:7- 9: "Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule Joka, yule Joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye."


Joka ni Shetani mwenyewe hasa. Lakini ni lini Shetani alipoudanganya ulimwengu wote? Alipotupwa chini kutoka mbinguni palikuwa na watu wawili tu duniani, na hao ndio walioiwakilisha dunia yote. Kwa kuwadanganya Adamu na Hawa katika Bustani ile ya Edeni, Shetani aliifanya dunia yote ipotee, naye akaimiliki kwa muda. PAMBANO KUU kati ya mema na mabaya, ambalo lilianza kule mbinguni, sasa likawa limehamia katika sayari hii.
 
Kweli kabisa ,shukraani mkuu🤝
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…