Ukumbi wa Papa: Ndiyo Utambulisho wa yule Nyoka wa Eden?

Hizi dini nizaidi ya tuzijuavyo, kunamambo mengi sana tunafichwa inaelekea
Sio tunafichwa mkuu, yan in short hatuyajui. Na sidhani kama kuna mtu ali-master dini yoyote kusema ukimuuliza swali la dini atakujibu kwa usahihi.
 
Umenikumbusha Kuna documentary moja Inaitwa SECRET OF SYMBOL mpak lile duara la nyuma katika picha ya yesu nilivyojua maana yake nilichoka..!
Sio ulivyojua,sema ulivyoambiwa! Hata hao waambiaji huwa wanaangalia mtu wa kumwambia!
 
Mkuu mi pia sina dini ila kwenye hizi dini za abrahmic ( hususani ukristo) dhana ya nyoka imetajwa katika pande zote mbili (kimungu/kishetani)

Ukisoma habari za nyoka katika bible utakuja kuona kwamba nyoka mwenye vinasaba vya ushetani ametajwa mara chache sana kuliko nyoka mwema

Mfano katika historia na habari za kiroho nyoka huwakilisha uzazi au maisha ya kibunifu, nyoka wanapojivua gamba huashiria kuzaliwa upya (immortality) na uponyaji.

Nyoka ameonekana kutumiwa na mungu katika missions za mitume wake

Ukisoma NUMBERS 21:8 mungu alikuwa anampa maelekezo musa kuwa atatengeneza nyoka ambaye yeyote atakaye mtazama atapona ( hapa nyoka kaonekana kama mponyaji)

Ukiendelea kusoma kisa cha mussa utaona kupitia mussa, Mungu amefanya miujiza mingi ya nyoka. Aliweza kufanya fimbo ya musa kuigeuza kuwa nyoka kisha huyo nyoka kuwameza nyoka (wa kishetani) wa farao

Swali langu ni kwanini swala la jengo kuwa na alama ya nyoka litazamwe kwa upande mmoja wa dhana ya ushetani na sio kinyume chake?
 
Nakuongezea na hii inayozungumzia positive side ya nyoka:

Mathayo 10:16
16 Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.
 
Mimi ya kwangu paa ni mfano wa eagle
 
Nadhani wewe umemaliza kila kitu
 
Ni nyoka anayemeza nyoka nyomi wa shetani[emoji23]
 
Ukumbi ni huu, tuonyeshe nyoka, achaneni na picha za wasabato zilizojazwa Google
 
Hapo kuna kichwa cha nyoka kweli? Maana dirisha liko kwa chini kabisa na sehemu ya juu ndiko mbele
 
Reptilian Race ni Hypothesis na hicho ulicho propose hapo pia ni Hypothesis.....

Hypothesis nzuri ni ile inayoweza kuelezea various observations....

Hypothesis yako inaweza kuelezea observations nitakazozitoa?
Mimi sijapinga kwamba hilo jengo halina muonekano wa nyoka (naomba unielewe vyema point hii)

Ila nahoji kutaka kujua kwanini conclusion yenu kwa muonekano wa jengo hilo liashirie ni ishara ya ushetani na sio kinyume chake?
 
Kwamba hayo umeyatoa kichwani kwako??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…