Ukurasa wa Hayati Magufuli umefungwa kama zilivyofungwa za wengine

Watatu kiaje sasa?

Mbona mnaanzisha nyuzi kwà papala?
 
Siyo kwamba hatuamini kwamba Magufuli (Rip) ameshafariki, tunalijua hili na tunaamini hivyo. Tunachofanya hapa ni kupambana na wafuasi ya yule mshikishwa ukuta, (aka dish limeyumba, au chizi, kamanda msaliti/mtundulisu).

ambao pamoja na yeye mwenyewe wamekuwa wakifanya juhudi kuwa sana za makusudi kumtukana, kulichafua jina lake na ku-paint picha isiyoendana na uhalisia wake. Hao tutakula nao sahani moja mpaka kieleweke.

Pili, wewe ni nani mpaka uwapangie watu cha kusema? Watu wana uhuru wa kujinafasi bhana, acha hizo.
 
Kwa orodha yako ya marais waliokwisha fariki ukianza na Karume, basi umewasahau akina Idris Abdul Wakil na Aboud Jumbe, ingawa Mkapa ambaye ni wa juzi tu kutangulia hukumweka kwenye hiyo list.
 
Wawe watatu wanne au sita ,cha kuzingatiwa ndio wameshatoweka na tukubali yao yamesita,jamhuri ipo na inaendelea,kuna ulazimishaji eti ni lazima mikakati na misimamo yake ifuatwe ,mnaobakia hapo hamna tofauti na wale askari wanaopiga marktime,Sasa yupo Raisi mupya na kile anachokisema yeye ndio hicho kinachotakiwa kusikilizwa. Magu is gone.

Na kiuhalisia Magufuli alishindwa kuwa mweledi katika baadhi ya mambo hasa kwenye kusimamia haki au amani pale panapotokea tukio kuu katika nchi ,kama mabarabara na madaraja mbona yalijengwa tokea na kabla ya Uhuru ? Kwa hayo alichokifanya ni kule kunakoitwa kuboresha.

Mepya ambayo yalitingisha Taifa na kupotea kwa watu maarufu,kupigwa risasi,kuokotwa watu baharini ndani ya vipolo,raia kupigwa viboko hadharani ,sikuwahi kumsikia Magu akilikemea au hata angalau kulitaja na kumtaka mhusika japo ababaishe,kwa sababu za kiccm,hamna.

Tuseme ukweli na sio kutetea mambo maovu au kwa vile halikukuta wewe mwana kuliafuta? Sio mlazimishe tuendelee na tabia zake ndio nikasema ,yeye ameshafariki na nyie mnaotaka tuendelee na mambo yake ndio msiomtakia kheri mnafukua na kusababisha makaburi yachunguzwe upya.

umemzika Magufuli na tuzike na mambo yake mnapoambiwa kazi iendelee,basi jiongezeni kwa akili zenu.magu sasa yupo kaburini peke yake nyinyi mliobakia ambao pengine mkinufaika kwa kukingiwa kifua na yeye na kujiona au mlijiona kama ndio maraisi sasa mpo peke yenu, kama ulikuwa ni mtenda maovu na kuruka hukumu, ile ngao yako ujue sasa haipo, kuendelea kumshobokea Magu ni kama vile huelewi au hukubali jamaa hatunae na unataka kuendeleza siasa zake. Utaishia jela achana nae na kuwa mtii na mfuata sheria kwa waliokuwepo.
 
Mheshimiwa Magufuli amefariki na kuzikwa Rasmi, kwao Chato ni rais wa tatu kuzikwa wakwanza akiwa Karume, wapili Nyerere na Magufuli anaifanya idadi iwe ya watatu.
Duh...!.
Haya ndugu yangu, Benjamin William Mkapa, anakusalimu!.
P
 
Duh umenikumbusha na Luteni Mkapa ,hawa wanaokufa kwa gafla wanaroo ngumu kuingia kwenye kundi la maiti. Ni wanne karume,Nyerere.Mkapa na Mheshimiwa Magufuli.
Kumbe hao wote walikufa ghafla?
 
Karume yupi au Mkapa?
 
mbona unasisitiza nawewe umewaamini hao watu,ambao hata hawajulikani ni akina nani na ni wapi waliyasema hayo!...
Dr. Ali Juma alikuwa makamu wa Rais 1995-2001 akafariki 4 July 2001 nafasi yake ilichukuliwa na Dr Sheni, weka kumbukumbu vizuri.
 
Dr. Ali Juma alikuwa makamu wa Rais 1995-2001 akafariki 4 July 2001 nafasi yake ilichukuliwa na Dr Sheni, weka kumbukumbu vizuri.
Wala sijaandika bahati mbaya mkuu,msiba wa makamu ni msiba wa rais hata jeshini ni hivyo.
 
Wala sijaandika bahati mbaya mkuu,msiba wa makamu ni msiba wa rais hata jeshini ni hivyo.
Historia hiyo ya makamu kupewa rank sawa na Rais ndio naisikia kwako... any way baki na unavyo amini mkuu.
 
Mkuu shida gani? Kwanini unahangaika na kivuli cha waliolala?
MAGUFULI AMELALA Na wewe laza akili yako kuhusu yeye, Kama umesahahu Mkapa naye kama Rais wa Awamu ya 3 Ya uchaguzi naye alilala.
Funga huo ukurasa akilini mwako achana na watu wengine.
 
Duh umenikumbusha na Luteni Mkapa ,hawa wanaokufa kwa gafla wanaroo ngumu kuingia kwenye kundi la maiti. Ni wanne karume,Nyerere.Mkapa na Mheshimiwa Magufuli.
Hao wote hawakuwa waheshimiwa na magufuli tuu ndio alikuwa mheshimiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…