Ukurasa wa Twitter wa Nape Nnauye nani anausimamia?

Ukurasa wa Twitter wa Nape Nnauye nani anausimamia?

Najua wazi viongozi wengi wa kisiasa wana vijembe sana. Wapo niliowahi kukutana nao na kushuhudia mwenyewe majibu yao yasiyo na staha. Lakini linapokuja suala la maadili, ifike mahali tuambiane ukweli.

Kwa majibu haya ya kejeli nina wasiwasi na anayetoa majibu hayo. Ni yeye kweli au kuna mtu anamjibia?View attachment 2584893View attachment 2584894
Mambo ya tweeter yamesababisha Rais wa Taifa kubwa duniani kuhudumu kwa mhula mmoja.

Niliwahi kutahadharisha siku nyingi kabla wakati akiwa bado yupo madarakani kwamba Rais huyo angehudumu mhula mmoja kutokana na tweets zake nilizokuwa nazisoma mtanadaoni

Mimi sioni haja sana ya viongozi wakubwa kuanzia ngazi ya Katibu Mkuu/ Wakuu wa Mikoa, kuwemo kwenye mitandao hii.

Sina shida na watu kama Jeshi la Polisi au IGP au Usalama wa Taifa, kuwemo kwemye mitandoa hii kwa sababu wao wapo kazini masaa 24, siku 7 kwa wiki; na kwa hiyo the best catch yao wakati mwingine inakuwa ni humu kwenye mitandao hii.

Tuseme kwa mfano, mtu kama Waziri mitandao kama hii inamsaidiaje kwenye majukumu yake? Labda kwa kusoma jumbe tu, ila siyo kwa kujibizana na watu au kutoa majibu kupitia mitandaaoni
 
Tatizo la Sisi watanzania (hasa wanyonge) tunapenda kuongea Kwa Lugha ngumu Mbele ya viongozi, sasa wakijibu Kwa kiwango kilekile tunaona ni tatizo.

Wananchi wanapenda viongozi wanaowanyenyekea😀😀🤣🤣.
Yaani mwananchi aongee atakavyo lakini amlimit kiongozi atakayemjibu.
Kwa nini wasione hivyo ikiwa uchaguzi ukifika hao hao viongozi hawaishi kuwapigia magoti watanzania ili wawapigie kura. Kiongozi sio mtawala. Anatakiwa awanyenyekee wale waliomuweka pale hata pale wanapotumia lugha zisizopendeza.

Aidha, si busara kutumia account yako binafsi kwa ajili ya mambo ya serikali. Mambo hayo ayaongelee kwenye account yake ya kiwazara ambayo inapaswa kusimamiwa na mtaalam wa mawasiliano. Huku kujibu ovyo kunaleta picha mbaya kwa serikali nzima na sio yeye peke yake.

Amandla...
 
FB_IMG_1681293149769.jpg
 
Back
Top Bottom