Ukurasa wa Twitter wa Nape Nnauye nani anausimamia?

Mambo ya tweeter yamesababisha Rais wa Taifa kubwa duniani kuhudumu kwa mhula mmoja.

Niliwahi kutahadharisha siku nyingi kabla wakati akiwa bado yupo madarakani kwamba Rais huyo angehudumu mhula mmoja kutokana na tweets zake nilizokuwa nazisoma mtanadaoni

Mimi sioni haja sana ya viongozi wakubwa kuanzia ngazi ya Katibu Mkuu/ Wakuu wa Mikoa, kuwemo kwenye mitandao hii.

Sina shida na watu kama Jeshi la Polisi au IGP au Usalama wa Taifa, kuwemo kwemye mitandoa hii kwa sababu wao wapo kazini masaa 24, siku 7 kwa wiki; na kwa hiyo the best catch yao wakati mwingine inakuwa ni humu kwenye mitandao hii.

Tuseme kwa mfano, mtu kama Waziri mitandao kama hii inamsaidiaje kwenye majukumu yake? Labda kwa kusoma jumbe tu, ila siyo kwa kujibizana na watu au kutoa majibu kupitia mitandaaoni
 
Kwa nini wasione hivyo ikiwa uchaguzi ukifika hao hao viongozi hawaishi kuwapigia magoti watanzania ili wawapigie kura. Kiongozi sio mtawala. Anatakiwa awanyenyekee wale waliomuweka pale hata pale wanapotumia lugha zisizopendeza.

Aidha, si busara kutumia account yako binafsi kwa ajili ya mambo ya serikali. Mambo hayo ayaongelee kwenye account yake ya kiwazara ambayo inapaswa kusimamiwa na mtaalam wa mawasiliano. Huku kujibu ovyo kunaleta picha mbaya kwa serikali nzima na sio yeye peke yake.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…