Ukurupukaji wa Hayati Magufuli unavyozidi kuligharimu taifa hata baada ya kifo chake

Ukurupukaji wa Hayati Magufuli unavyozidi kuligharimu taifa hata baada ya kifo chake

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Tangu akiwa Waziri Magufuli alifahamika kama mtu mkurupukaji mwenye kufanya maamuzi ya pupa kwa hasira na kukomoa.

Hii sio iliumiza watu wengi tu bali pia kuitia hasara serikali pale ambapo aliyechezewa rafu na mwendazake ni wa kimataifa na anaishtaki Serikali.

Leo tena tumeona ndege ya Tanzania kukamatwa nje ya nchi baada ya serikali ya Magufuli kuvunja mkataba bila kuzingatia sheria mwaka 2016.

Na bado mengine mengi yanakuja, soma hapa.

 
Kwani huyo Magufuli ndie anayeendelea kuwafanya hawa wa sasa washindwe kulipa hicho tunachodaiwa?

Magufuli alikuwa sehemu ya tatizo ambaye alishapita, CCM kiini cha tatizo bado tunayo, badala ya kuhangaika na kiini cha tatizo, mnahangaika na sehemu ya tatizo ambayo ilishapita, ajabu kutwa kujiita GT wa JF!.

Pesa nyingi za walipa kodi huwa zinachezewa na serikali ya CCM, hasa ripoti za CAG hutuonesha na wahusika hawachukuliwi hatua zozote, mpo kimya...

Kwanini wasitoe sehemu ya hizo pesa wanazochezea wakalipe hayo madeni, badala ya kuacha pesa nyingi ziishie kwenye matumbo ya wachache kila mwaka?

Kama wewe na wenzio mnamuona Magufuli alikuwa ni tatizo, kwangu CCM na serikali yake inayowalinda wezi ni tatizo kubwa zaidi.
 
Ugumu wa maisha unaendelea mtaani kwa wengi yeye ndie chanzo kwa kupeleka pesa nyingi Sana kwenye miradi. Na miradi yote imepeleka pesa nje kwenye nchi zao kununua vifaa vya miradi.

Pesa zote zile zingebakia nchini kuchochea uzalishaji kupitia nguvu Kazi ya ndani, maisha yasingekuwa magumu kiasi hiki.
 
Ugumu wa maisha unaendelea mtaani kwa wengi yeye ndie chanzo kwa kupeleka pesa nyingi Sana kwenye miradi. Na miradi yote imepeleka pesa nje kwenye nchi zao kununua vifaa vya miradi.
Pesa zote zile zingebakia nchini kuchochea uzalishaji kupitia nguvu Kazi ya ndani, maisha yasingekuwa magumu kiasi hiki.
Wewe tafuta hela acha kulia lia hapa! Lini serkali inagawa hela! Sema tu serkali ya bibi yenu haijui inachofanya!
 
Bila hivyo nchi ilikuwa inaelekea kuzimu kwa kasi ya ajabu sana
Ila nyinyi vyeti feki mna shida sana! Sasa Samia akaingia vipi siku hizi mnaokota pesa? Maana nijuavyo mimi hakuna mwekezaji makini anaweza kuja kwenye nchi isiyo na umeme! Mnajificha kweney kivuli cha JPM huku watu wanajua uwezo wenu kuongoza nchi ni zero!
 
Ujui chochote kuhusu uchumi pita kushoto.Hata nchi zenye unafuu hazigawi hela kwa watu wao
Wewe unayejua uchumi na kwa akili yako uchumi chini ya Samia na Mwigulu ni mzuri? Naomba maoni yako mbobevu wa uchumi!?
 
Back
Top Bottom