Ukuta wangu umepatwa na Ugonjwa huu, naomba msaada

Ukuta wangu umepatwa na Ugonjwa huu, naomba msaada

Mwambie afanye Skiming na white cement then apake Silk vinyl kuta za ndani na Weather guard kuta za nje
Vile aondoe kama kuna mti jirani unaosababisha eneo hilo lisipata mwanga wa jua
 
Kabla ya kutatua tatizo, kwanza unatakiwe ujue chanzo cha tatizo "Root cause" ama sivyo utatatua tatizo ila tatizo litarudi kujitokeza tena.

Fuatilia procedure za upigaji rangi, huo ukuta unaonekana ulipigwa rangi ukiwa wet "Unyevunyevu wa maji"

Piga rangi ya primary ukuta ukiwa mkavu kisha fuata maelekezo yaliyoandikwa kwenye rangi na manufacturer halafu ndio upige rangi, usitafute njia ya kusolve problem bali tafuta njia ya kueliminate the problem.
 
Hili janga lipo sana tabora maeneo ya kanyeye nyumba zinachakazwa sana na chumvi naweza kujifunza kitu hapa
 
Mkuu, utakuwa umejenga kwenye chemchem ya volkano....kimbia fastaaaa !!
 
1 maandalizi mabovu kabla ya rangi
2. Tofauli ulizojengea nazo zaweza kuwa sababu
4. Ame skim ukuta kwa kutumia nini na layer kubwa kiasi gani
Naomba unielimishe hapo kwenye skimming! Upande wa tofali ni za kuchoma
 
Hiyo ni fungus ya kuta inasababishwa na chumvi au unyevu nyevu.

Ni vizuri kutumia terrazzo kwenye vyoo na pia kuweka karatasi ya kuzuia unyevu kwenye kuta kabla ya kujenga.

Nadhani na contents ya rangi inasababisha reaction zaidi
 
Maji yanavujia au kunyonywa kwa ndani.. Tiba yake kuna cement plasta maalum kwa maeneo hayo maranyingi huwa chumba kinachopakana na choo au sink la maji linalovujisha maji
Upo sawa mimi wangu unatoa maji nadhani kwasababu umepakana ni chemba ila sina uakika coz nashindwa kuelewa chanzo cha hayo maji yanatoka wapi
 
Maji yanavujia au kunyonywa kwa ndani.. Tiba yake kuna cement plasta maalum kwa maeneo hayo maranyingi huwa chumba kinachopakana na choo au sink la maji linalovujisha maji
Then hiyo sio tiba maana tatizo liko palepale, tiba ni kutindua na kuondoa hizo bomba au kufix hilo sinki

Kuna nyumba nzuri nimeona hilo tatizo, ukuta unalika vibaya mno, bomba(piping system) zinavujia ndani kwa ndani, bili ya maji Tsh 25,000 kwa mwezi ila around 19,000 unalipia Leakage

Kibanda changu bomba zinapita nje, kuchimbia bomba za maji inacost sana baadae
 
Hapo tatizo ni kuta zinanyonya maji, sasa chanzo ni nini inaweza kuwa eneo hilo eidha
1. water table ipo juu, au
2. Eneo ni damp (linatuamisha maji) kama maeneo ya mabonde
Au pia
3. Inaweza kuwa ni mifumo ya maji ya nyumba (kama tatizo linatokea upande wenye vyoo pekee)

Kama ishu ni tatizo namba 1 au mbili basi kulikua na umuhimu wa kuweka dpc (damp proof coarse) na dpm (damp proof membrane) baada ya msingi wakati wa ujenzi na matumizi ya white cement wakati wa skimming
na kama tatizo ni namba mbili basi kuna umuhimu wa kucheki mifumo ya maji au kutumia white cement na rangi zenye uwezo wa kuhimili maji kama alivyoeleza mdau mwingine hapo
 
Kutibu bila kujua kinachosababisha ni kazi bure. KusKim na White cement Haiwezi kuzuia ascending water au rain splash. Utaalamu zaidi unahitajika
Kabisa Mkuu, Watu wengi wameshatumia gharama kwa ushauri wa Fundi rangi lakini baada ya muda ishu inarudi palepale.
 
Hili janga lipo sana tabora maeneo ya kanyeye nyumba zinachakazwa sana na chumvi naweza kujifunza kitu hapa
Tumia hiyo njia ya kutibu kwa Ultra flex 2 niliyotoa post ya nyuma ndio solution ya uhakika nimefanya kazi hiyo huko huko Tabora.
 
Huo ugonjwa ulikwisha kosewa toka awali kabla ya jamvi.IKiukweli dawa ya kuuponya haipo labda ya kuutuliza kwa muda tu.!Mkuu, i
Yeah nilikuwa natafuta hili jina la white cement.. Hiyo ndio tiba yake
lipaswa baada ya fundi kuona Hali ya ardhi ya hapo kuwa kuna chumvi nyingi na maji mengi eneo hilo,angekushauri kununua DAMP PROOF MEMBRANE (DPM) Ikatandikwa Kisha BAADA ya jamvi ndo ukaweka DAMP PROOF COURSE (DPC).huo unyevu na chumvi visinge panda ukuta asilani!
Sasa hapo hata ukarabati vipi au uskim vipi huo unyevu au chumvi hiyo haizuliki bali kila baada ya mwaka au miaka 2 lazima ukarabati TU.
 
Back
Top Bottom