Ukuta wangu umepatwa na Ugonjwa huu, naomba msaada

Ukuta wangu umepatwa na Ugonjwa huu, naomba msaada

Then hiyo sio tiba maana tatizo liko palepale, tiba ni kutindua na kuondoa hizo bomba au kufix hilo sinki

Kuna nyumba nzuri nimeona hilo tatizo, ukuta unalika vibaya mno, bomba(piping system) zinavujia ndani kwa ndani, bili ya maji Tsh 25,000 kwa mwezi ila around 19,000 unalipia Leakage

Kibanda changu bomba zinapita nje, kuchimbia bomba za maji inacost sana baadae
[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji817][emoji736]
 
Kutibu bila kujua kinachosababisha ni kazi bure. KusKim na White cement Haiwezi kuzuia ascending water au rain splash. Utaalamu zaidi unahitajika
Yaah nadhani uko sahihi, hayo ni maji toka ardhini yanapanda na kuharibu hiyo rangi au lipu na kama ni hapa Dar basi chumvi chumvi iliyoko kwenye maji yetu ndiyo inafanya uharibifu huo. Suluhisho sahihi ni kuweka plastiki chini ya huo ukuta, yaani unakatwa kwa chini na kuzungushia hiyo plastiki ili kuzuia hayo maji kupanda juu. Baada ya TIBA hiyo, then hayo mengine yanafuata na utakuwa umemaliza tatizo hilo.
 
Then hiyo sio tiba maana tatizo liko palepale, tiba ni kutindua na kuondoa hizo bomba au kufix hilo sinki

Kuna nyumba nzuri nimeona hilo tatizo, ukuta unalika vibaya mno, bomba(piping system) zinavujia ndani kwa ndani, bili ya maji Tsh 25,000 kwa mwezi ila around 19,000 unalipia Leakage

Kibanda changu bomba zinapita nje, kuchimbia bomba za maji inacost sana baadae
Duh bomba zinapita nje! Itakuwa nyumba ya ajabu.
 
Hapo tatizo ni kuta zinanyonya maji, sasa chanzo ni nini inaweza kuwa eneo hilo eidha
1. water table ipo juu, au
2. Eneo ni damp (linatuamisha maji) kama maeneo ya mabonde
Au pia
3. Inaweza kuwa ni mifumo ya maji ya nyumba (kama tatizo linatokea upande wenye vyoo pekee)

Kama ishu ni tatizo namba 1 au mbili basi kulikua na umuhimu wa kuweka dpc (damp proof coarse) na dpm (damp proof membrane) baada ya msingi wakati wa ujenzi na matumizi ya white cement wakati wa skimming
na kama tatizo ni namba mbili basi kuna umuhimu wa kucheki mifumo ya maji au kutumia white cement na rangi zenye uwezo wa kuhimili maji kama alivyoeleza mdau mwingine hapo
Well said mkuu.
 
Back
Top Bottom