Ukwel kuhusu biashara na bidhaa za forever living

Ukwel kuhusu biashara na bidhaa za forever living

Ni kampuni ya network marketing inayodili na uuzaji WA dawa za binadamu ambazo Ni nzuri Sana kiukweli hii Ina tofauti na forever living na gnld kwanza kiingilio Ni 34000 Tu na unahitaji kuunganisha watu watano Tu PIA product zao Ni bei rahis

Mkuu nitapateje details za hiyo bf
 
wakati ukifika utakulazimu utajiunga tu. hizi networking market ni nyingi mno hasa kwa wenzetu hivyo ni kuwa makini tu kampuni nyingine ni kongwe na nyingine zinaibuka kwa sasa as the best so akili mkichwa . ni ushauri tu kama mmeamua kufuata digital kutoka analog basi hata kwa mfumo huu ipo siku mtawatafuta tu
 
Ushauri unaopewa hapa juu utakuchanganya. Nakushauri tafuta watu wanayoifanya ambao unawaamini na kuwaheshimu wakushauri vizuri.pia soma vitabu, na ingia kwa interntet (mitandao) duniani utapata ukweli pia. Wataalamu wakubwa dunia wanasema kuwa watu wengi huwa hawafanikiwi kwa vile wanasilikiza opionion (mawazo) ya watu wengine na sio facts(kweli kuhusu jambo Fulani). Na ukweli ni kwamba ukitaka kufanikiwa lazima ufanye vitu au mambo tofauti na watu wengine. ukifanya sawa sawa na wengine huwezi fanikiwa kwa vile utakuwa huna jipya. kudhihilisha hilo ebu jiulize watu wengi wanasomea mambo gani?, wanafanya biashara za aina gani? wanaisho maeneo gani? nk. Fanya utafiti wako mwenyewe na chukua maamuzi mwenyewe na sio kwa kufuata wanayosema wengi hapa. Kwa hakika wengi wanaokushauri hapa hawajui na pengine hawaja wahi kufanya biashara hiyo na wengine walifanya na wameferi. swali ungependa kupata ushauri kwa asiyefanya biashara hiyo au aliyeferi biashara hiyo? mimi nashauri pia tafuta waliyo fanikiwa na watakueleza walifanikiwaje. Watalamu pia wanashauri acha kuandamana na 'negative people'maana wao kila kitu kwao hakiwezekani.Pia usiogope kukosea kwani kukosea ni dalili kuwa una jalibu na ukikosea jifunze kutoka na makosa! tafiti zinaonyesha pia kuwa watu wote waliofanikiwa walikosea mara nyingi sana na wakajifunza mengi sana. kuna usemi huu 'You don't need to be perfect to start, but you need to start to be perfect' sijui unauchukulia.
 
Mi huwa najiuliza ukikosa wa kumuulizia hizo bidhaa inakuwaje? Unarudishiwa hela yako?
 
Mi huwa najiuliza ukikosa wa kumuulizia hizo bidhaa inakuwaje? Unarudishiwa hela yako?

actually hawawez kukurudishia na suala la kukosa mtu WA kumuuzia mi nasema Ni vigum Sana kukosa mtu WA kumuuzia kwa mfano mi nipo kwny network marketing ya madawa ya binadam magonjwa kama kisukari,pumu, presha na joint sasa kwa magonjwa hayo utakosa VP mtu WA kumuuzia? ...ninachowasihi vijana wenzangu tafuten information sahihi msisikilize watu wengi humu,wengi wao hawajawah kufanya hii biashara na km washafanya walishindwa kukabiliana na changamoto
 
Ningependa tu share ujuzi juu ya hii biashara ya uuzaji wa bidhaa na kampuni tajwa apo juu, Je! kuna ukweli wowote na sio utapeli jamani???

Mwenye kitu tafadhali usisite kudondosha apo chini

avatra_mok ushapata solution
 
Last edited by a moderator:
ila hawa jamaa dawa zao ni chenga tu hamna lolote m nlitumia dawa za hela ndefu lakin hata matokeo sijayaona
 
Inalipa ndugu Yangu...kulko ata wenye pharmacy. Ukibahatika kubali tu ndugu Yangu.
 
Hawa jamaa wajanja sana,hapo biashara siyo products bali ni collection ya entry fee.Ndiyo maana wanaencourage new recruitment.
 
Hivi seriously nani anaweza kununua dawa ya meno kwa 15k? Uanze kumconvince mtu awe ananunua ni kazi nzito sana.
Si kila mtu lazima afanye hii biashara wengine tutakuwa watazamaji tu. Siwezi kusugua soli kila siku nimnenepeshe mwingine.
Wizi tu hakuna lingine.

Cwezi fanya biashara ya For ever aisee heri nifanye biashara ya kuuza maji ya kandoro tu njiani inalipa,mchana jua likiwaka maskini wenzangu lazima wanywe.Lkn For ever aaah hapana aiseee.Tuwaachie wanaosema inalipa.Nadhani wakiwa wachache ndo itawalipa zaidi maana wateja watakuwa wengi na wauzaji wachache.Ila kuwa tuingie wote bidhaa tutamuuzia nani?
 
Kuna wengne wanaitwa 4life wapo pale Nakiete mwenge,wana dawa mpaka za ebola na ukimwi
 
living aah sikushauri kiingilio ni laki saba sasa huu si mtaji tosha niwape ya nini?
 
Siwezi kusema kama ni biashara nzuri au la sababu kuna watu wanazifanya na maisha yankwenda mbele

My take
Kama unataka kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye malengo makubwa basi biashara hii haikufai sababu utatumia nguvu nyingi sana kufaidisha wengine kuliko wewe ila pesa ya kula na kununua tecno huwezi kosa kama unabidii sana ya kupiga longolongo
Tatizo la biashara hii ipo limited sana sio kama kufungua duka lako au kunzisha biashara yako binafsi unaweza kuwa flexible kuliko hawa jamaa

Ila kama unataka kutafuta uzoefu na chaneli basi ingia kwa malengo then baada ya muda unaitema

Kiujumla ni biashara moja ya kishenzi ila ukiipatia inakuweka mjini kimtindo
Biashara yoyote nzuri huitaji kupewa semina na watu wanaojifanya wmefanikiwa nayo kukuconvice uifanye, biashara nzuri hujitangaza yenyewe, watu wanatumia maneno mazito kukushawishi ooh uoga wako sijiu nini mara wanaofanikiwa blah blah..... Asili ya biashara ni kutokuwa na washindani inanoga sasa hii wuzaji wanauza na kusaka wauzaji kwa udi na uvumba

Ushenzi wa hii makitu ni mfumo unaitwa pyramid scheme ingiza wengi kwenye network yako ili upate zaidi, hapo unaweza kuta unatumia muda mwingi kushawishi watu waingie kwenye chaneli yako kuliko kuuza bidhaa, na moja ya sifa ya pyramid scheme lazima itafika sehemu ita corrupt
Bila kujali bidhaa zinauzika au la lakini mkiletena wenyewe basi wale jamaa wanauhakika wa kuuza sh laki saba ndio maana wanakushawishi uingize watu zaidi kuliko hata kuuza bidhaa zao , so mleta mada najua jamaa watakua wamekufata na pm za kutosha na ukienda tu jamaa wameingiza laki saba zao na interest inagawiwa kwenye chaneli uliyoingilia

Utashangaa unakutana na mtu badala ya kukuuzia anakushawishi na wewe uwe muuzaji..... Hushangai? Anakujali sana au?
Nenda sasa kwenye semina zao kuna washenzi wanatoa ushuhuda wa kitoto utacheka, wengine wanakuja theory hata billy gate mtoto nafuu hata ya semina za Shigongo
Angalia post ya Mr II hayo ndio maneno yao matamu na yakutia moyo lakini ukweli hizo ni theory tu

Naamini biashara zipo nyingi sana mkuu kuna kichwa utatoka tu ukiwa hata na milioni moja, nakuhakikishia kama unatafuta biashara serious kwa maisha yako don't go there
 
Last edited by a moderator:
The end should not be used to justify the means. Sababu wapo waluofanikiwa isitumike kama ndo njia ya kuwapumbaza wengine. Na pia kufananisha biashara yenu na Barkhesa ni matusi. Kuuza biashara ya Barkhesa huitaji kumlipa Barkresa kiingilio. Hebu achenii uhuni. Hizi njia zote ni shortcut. Utapata pesa sawa. Lakini sustainability ipoje? .Tanzania bado bikra. Tuzalishe mali tuache shortcut
 
Back
Top Bottom