Siwezi kusema kama ni biashara nzuri au la sababu kuna watu wanazifanya na maisha yankwenda mbele
My take
Kama unataka kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye malengo makubwa basi biashara hii haikufai sababu utatumia nguvu nyingi sana kufaidisha wengine kuliko wewe ila pesa ya kula na kununua tecno huwezi kosa kama unabidii sana ya kupiga longolongo
Tatizo la biashara hii ipo limited sana sio kama kufungua duka lako au kunzisha biashara yako binafsi unaweza kuwa flexible kuliko hawa jamaa
Ila kama unataka kutafuta uzoefu na chaneli basi ingia kwa malengo then baada ya muda unaitema
Kiujumla ni biashara moja ya kishenzi ila ukiipatia inakuweka mjini kimtindo
Biashara yoyote nzuri huitaji kupewa semina na watu wanaojifanya wmefanikiwa nayo kukuconvice uifanye, biashara nzuri hujitangaza yenyewe, watu wanatumia maneno mazito kukushawishi ooh uoga wako sijiu nini mara wanaofanikiwa blah blah..... Asili ya biashara ni kutokuwa na washindani inanoga sasa hii wuzaji wanauza na kusaka wauzaji kwa udi na uvumba
Ushenzi wa hii makitu ni mfumo unaitwa pyramid scheme ingiza wengi kwenye network yako ili upate zaidi, hapo unaweza kuta unatumia muda mwingi kushawishi watu waingie kwenye chaneli yako kuliko kuuza bidhaa, na moja ya sifa ya pyramid scheme lazima itafika sehemu ita corrupt
Bila kujali bidhaa zinauzika au la lakini mkiletena wenyewe basi wale jamaa wanauhakika wa kuuza sh laki saba ndio maana wanakushawishi uingize watu zaidi kuliko hata kuuza bidhaa zao , so mleta mada najua jamaa watakua wamekufata na pm za kutosha na ukienda tu jamaa wameingiza laki saba zao na interest inagawiwa kwenye chaneli uliyoingilia
Utashangaa unakutana na mtu badala ya kukuuzia anakushawishi na wewe uwe muuzaji..... Hushangai? Anakujali sana au?
Nenda sasa kwenye semina zao kuna washenzi wanatoa ushuhuda wa kitoto utacheka, wengine wanakuja theory hata billy gate mtoto nafuu hata ya semina za Shigongo
Angalia post ya
Mr II hayo ndio maneno yao matamu na yakutia moyo lakini ukweli hizo ni theory tu
Naamini biashara zipo nyingi sana mkuu kuna kichwa utatoka tu ukiwa hata na milioni moja, nakuhakikishia kama unatafuta biashara serious kwa maisha yako don't go there