Avatar
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 11,128
- 11,921
- Thread starter
- #101
Ushauri unaopewa hapa juu utakuchanganya. Nakushauri tafuta watu wanayoifanya ambao unawaamini na kuwaheshimu wakushauri vizuri.pia soma vitabu, na ingia kwa interntet (mitandao) duniani utapata ukweli pia. Wataalamu wakubwa dunia wanasema kuwa watu wengi huwa hawafanikiwi kwa vile wanasilikiza opionion (mawazo) ya watu wengine na sio facts(kweli kuhusu jambo Fulani). Na ukweli ni kwamba ukitaka kufanikiwa lazima ufanye vitu au mambo tofauti na watu wengine. ukifanya sawa sawa na wengine huwezi fanikiwa kwa vile utakuwa huna jipya. kudhihilisha hilo ebu jiulize watu wengi wanasomea mambo gani?, wanafanya biashara za aina gani? wanaisho maeneo gani? nk. Fanya utafiti wako mwenyewe na chukua maamuzi mwenyewe na sio kwa kufuata wanayosema wengi hapa. Kwa hakika wengi wanaokushauri hapa hawajui na pengine hawaja wahi kufanya biashara hiyo na wengine walifanya na wameferi. swali ungependa kupata ushauri kwa asiyefanya biashara hiyo au aliyeferi biashara hiyo? mimi nashauri pia tafuta waliyo fanikiwa na watakueleza walifanikiwaje. Watalamu pia wanashauri acha kuandamana na 'negative people'maana wao kila kitu kwao hakiwezekani.Pia usiogope kukosea kwani kukosea ni dalili kuwa una jalibu na ukikosea jifunze kutoka na makosa! tafiti zinaonyesha pia kuwa watu wote waliofanikiwa walikosea mara nyingi sana na wakajifunza mengi sana. kuna usemi huu 'You don't need to be perfect to start, but you need to start to be perfect' sijui unauchukulia.
mkuu imeningia akilini ... shukrañ