Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 586
- 590
- Thread starter
- #21
Mkuu msikilize vizuri Mhe. Mwigulu Nchemba ni bilioni 1 kwa kila jimboPoint of correction
Kuhusu barabara kila jimbo litapata millioni 500
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu msikilize vizuri Mhe. Mwigulu Nchemba ni bilioni 1 kwa kila jimboPoint of correction
Kuhusu barabara kila jimbo litapata millioni 500
Kilimo kinachangia kwa sehemu kubwa maendeleo ya nchi yetu. Bajeti yake ipoBila kilimo,hata aje Malaika hatutoboi
TARURA wanahusika kwa kushirikiana na wabunge.Ambazo watawekewa TARURA wajenge barabara au zitaingizwa kwenye ac ya mbunge?kama mbowe alivyokuwa anapigania.
Historia mpya itaandikwa kwa wino wa chuma. Serikali imedhamiria kwa dhati kuleta maendeleo jumuishi kwa wananchi wa Tanzania.Kila mwaka , ngojera hizo zimekuwa zikiimbwa sana!!cha ajabu waziri anasema itabidi tufunge mikanda, huku wazee wa kusifu na kuabudu(wabunge wa ccm) wanatwambia sasa hii ni bajeti ya kurudisha pesa kwa mwananchi, vyuma vimepatiwa grisi wakiongozwa na nape!
Sasa hadi hapo kuna nini!!?huo ubabaishaji utaisha vipi wakati pesa nyingi inaliwa na wajanja!!eti mashine za efd za makusanyo zimepotea! unaingiza 50, zinapotea 70 hapo utegemee maendeleo?ndio maana marais wengi wa Africa wameamua kuwatesa wanyonge ili wapate pesa za bure za IMF/WB kwa kisingizio cha COVID 19!
Suala la Msingi ni kwamba wapo Bungeni na sauti zao zinatakiwa kusikika wakishauri kwa hoja.hivyo vyama vingine ulivyo vitaja je vina wabunge silimia %ngapi humo buni mpaka waweze kupinga yanayopitishwa na wabunge wachama tawala
Usisahau tu In Shaa Allah tarehe kama ya leo mwakani uje utupe tathmini ya utekelezaji wa hii bajeti...imekuwa ni kawaida miaka nenda miaka rudi kutenga mipesa lakini miradi haitekelezeki!...kabla sijasahau katika hizo trilion 36 asilimia ngapi tutategemea misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo wa nje ya nchi..zamani kidoogo wakiitwa "mabeberu"Historia mpya itaandikwa kwa wino wa chuma. Serikali imedhamiria kwa dhati kuleta maendeleo jumuishi kwa wananchi wa Tanzania.
Hatutakiwi kuruhusu matatizo yatawale, tunatakiwa kuyatatua.
Wahenga walisema "Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha", baada ya mjadala mrefu juzi Juni 22, 2021 Bunge la Tanzania lilipitisha na kuidhinisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania shilingi trilioni 36.68 (36,681,897,765,000) kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo wabunge 361 sawa na 94% walipiga kura ya ndiyo, wabunge 23 sawa na 6% walipiga kura isiyo ya maamuzi (hawajakataa wala kukubali) na wabunge 5 hawakuwepo wakati wa zoezi hilo la upigaji kura. Ikumbukwe kwamba bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 ina ongezeko la 4% ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2020/2021 iliyokuwa ni shilingi trilioni 34.8.
Nilimsikiliza kwa makini Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) wakati akijibu hoja kwa ajili ya kuhitimisha mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali kabla ya Bunge kuidhinisha Bajeti hiyo Bungeni jijini Dodoma, kwa hakika Serikali inahitaji kupewa pongezi za dhati kwa jinsi ilivyojipambanua namna ambavyo itaenda kuitekeleza bajeti hii na kuhakikisha inaleta maendeleo jumuishi na endelevu.
Kuna baadhi ya hoja (mambo) wengi wetu tulizielewa vibaya kutokana na tafsiri tofauti zilizoenea sambamba na kukosa taarifa sahihi na huu hapa chini ndiyo ukweli kuhusu bajeti hii.
KODI YA MAJENGO KUPITIA MITA ZA LUKU
Kodi hii haitatozwa kwa kila mwenye umeme na wala kwa matumizi ya umeme bali maeneo ambayo yatatozwa ni yale yaliyoainishwa yenye sifa kisheria, hivyo namba za mita za luku za wananchi ambao hawatakiwi kulipa zitaondolewa katika mfumo (blacklisted). Sambamba na hilo kodi hii italipwa na mmiliki wa nyumba na sio ya mpangaji. Kama ilivyokuwa inakusanywa kwa njia ya kawaida (physical) ukusanyaji uleule unapelekwa katika njia ya kielektroniki kwa sababu teknolojia imekuja ili kurahisisha kazi.Makato hayatafanyika kila siku bali ni pale tu mtu anapoweka muda wa maongezi. Makato yataanzia shilingi 5 kwa wanaotumia shilingi 1000/= kwenda chini mpaka shilingi 222 kwa wanaotumia 100,000/= na kuendelea.
Serikali imeeleza kuwa kodi hii haitatozwa kwa kila mwenye umeme na wala kwa matumizi ya umeme kwa sababu kodi ingetozwa kwa matumizi ya umeme gharama za uzalishaji wa umeme zingeongezeka na hivyo kuleta adha kwa wananchi.
MAKATO YA SIMU KWENYE MUDA WA MAONGEZI
Mhe. Mwigulu Nchemba alisisitiza kuwa nchi hii (Tanzania) itajengwa na watanzania wenyewe, ni lazima tubebe majukumu hayo (ulipaji wa kodi) kama watanzania kwa sababu majukumu hayo ni yetu na nchi yetu ina matatizo pamoja na jitihada kubwa ambazo zimefanyika. Kila hatua ya maendeleo tunayoifanya inatuletea changamoto zaidi; ndivyo utaratibu wa maendeleo ulivyo.
WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI
Serikali imetenga nyongeza ya bilioni 322 kwa ajili ya kufungua maeneo ambayo hayapitiki (hayana barabara) katika maeneo ya mijini na vijijini. Kila jimbo la uchaguzi litapata si chini ya bilioni 1 kwa ajili ya barabara hizi.
Barabara za vijijini zimekuwa ni kilio kikubwa kwa muda mrefu. Kutengwa kwa fedha hizi ambazo zitatumika kujenga barabara za vijijini ili zikae muda mrefu kutasaidia usafiri wa uhakika kwa wananchi, usafirishaji wa bidhaa na kuanza kusogeza huduma karibu na wananchi sambamba na kuiwezesha TARURA kifedha na kiutaalamu ili ifanye kazi kwa ufanisi zaidi.
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Serikali imetenga nyongeza ya bilioni 70 ili kuwapeleka chuo wanafunzi 11,000 waliokosa mkopo mwaka 2020 na wanafunzi 10,000 wanaokadiriwa kuwa wangekosa mkopo mwaka 2021. Kutengwa kwa fedha hizi kutawezesha wanafunzi wote waliodahiliwa katika vyuo vikuu nchini na kuomba mkopo katika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuweza kupata mikopo na kutimiza azma yao ya kupata elimu ya juu na kuongeza wasomi wa kada mbalimbali nchini.
Pia Serikali imetenga nyongeza ya bilioni 125 kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya vyumba vya madarasa (maboma) 10,000 kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza, kila halmashauri itapata maboma yasiyopungua 10. Wanafunzi wengi waliofaulu wamekuwa wanashindwa kwenda kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za Serikali kwa sababu hakuna nafasi au miundombinu haitoshi.
Ikumbukwe kuwa mwaka kesho (2022) taifa linaenda kupata toleo la kwanza la wanafunzi wanaoenda kumaliza darasa la saba na kuanza kidato cha kwanza ambao waliandikishwa kupitia elimu bila malipo kwa shule ya msingi. Fedha hizi ni sehemu ya hatua nzuri kukabiliana na uhitaji wa vyumba vya madarasa nchini.
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Serikali imetenga nyongeza ya bilioni 100 kwa ajili ya zahanati kwenye vijiji na kata (maboma ya afya). Fedha hizi zitahakikisha ujenzi ulioanza na ujenzi mpya unakamilika katika maeneo husika na wananchi hususan maeneo ya vijijini wanapata huduma bora za afya.
Pia Serikali imetenga nyongeza ya bilioni 50 kwa ajili ya vifaa tiba pamoja na dawa. Utekelezaji huu utaenda sambamba na suala la bima kwa wote.
WIZARA YA MAJI
Serikali imetenga nyongeza ya bilioni 207 kwa ajili ya shughuli za maji na utaratibu wa visima na mabwawa. Kwa sasa Serikali inajielekeza katika utaratibu wa kisima kwa kila kijiji kama ilivyo kwa umeme.
Pia fedha hizi zinatarajia kufanya ununuzi wa magari ya kujimba visima na greda za kuchimba mabwawa.
Mbali na hoja hizo hapo juu, Serikali imesisitiza kuwa inazingatia mambo yote yanayoikabili nchi yetu sambamba na miradi ya kimkakati ambayo ni lazima ipate fedha; Serikali imeona vyema ikafanya utaratibu wa kupata fedha kiasi (fedha za ndani) lakini kwa wakati huohuo itafute mikopo yenye masharti nafuu ambayo haitaipa mzigo mkubwa wa deni kwa taifa letu.
Ndugu watanzania wenzangu kazi ya kujenga nchi yetu lazima ifanywe na sisi sote.
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Wizara ya Fedha na Mipango imeweka mapendekezo mbalimbali yanayolenga kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi kama vile; kuzingatia maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 9% hadi 8%, kufanya marekebisho ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kupunguza kiwango cha mchango kutoka asilimia1.0% hadi 0.6%, pamoja na kuzingatia maslahi ya wakulima wa mbogamboga na wengineo.bajeti yoyote ambayo kila mwaka inakuja na mbinu mpya ya kumkamua na kumtoa pesa mwananchi hadi yule wa chini kabisa hiyo ni bajeti mufilisi, bajeti bora ni ile inayompa mwananchi wa kawaida hauweni kwenye kodi...
Amen, Mwenyezi Mungu atujalie uzima.Usisahau tu In Shaa Allah tarehe kama ya leo mwakani uje utupe tathmini ya utekelezaji wa hii bajeti...imekuwa ni kawaida miaka nenda miaka rudi kutenga mipesa lakini miradi haitekelezeki!...kabla sijasahau katika hizo trilion 36 asilimia ngapi tutategemea misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo wa nje ya nchi..zamani kidoogo wakiitwa "mabeberu"