Ukweli kuhusu bajeti ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania 2021/ 2022

hivyo vyama vingine ulivyo vitaja je vina wabunge silimia %ngapi humo buni mpaka waweze kupinga yanayopitishwa na wabunge wachama tawala
 
Historia mpya itaandikwa kwa wino wa chuma. Serikali imedhamiria kwa dhati kuleta maendeleo jumuishi kwa wananchi wa Tanzania.
Hatutakiwi kuruhusu matatizo yatawale, tunatakiwa kuyatatua.
 
hivyo vyama vingine ulivyo vitaja je vina wabunge silimia %ngapi humo buni mpaka waweze kupinga yanayopitishwa na wabunge wachama tawala
Suala la Msingi ni kwamba wapo Bungeni na sauti zao zinatakiwa kusikika wakishauri kwa hoja.
Bungeni mambo yanajadiliwa kwa maendeleo ya nchi na sio vyama.
 
Historia mpya itaandikwa kwa wino wa chuma. Serikali imedhamiria kwa dhati kuleta maendeleo jumuishi kwa wananchi wa Tanzania.
Hatutakiwi kuruhusu matatizo yatawale, tunatakiwa kuyatatua.
Usisahau tu In Shaa Allah tarehe kama ya leo mwakani uje utupe tathmini ya utekelezaji wa hii bajeti...imekuwa ni kawaida miaka nenda miaka rudi kutenga mipesa lakini miradi haitekelezeki!...kabla sijasahau katika hizo trilion 36 asilimia ngapi tutategemea misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo wa nje ya nchi..zamani kidoogo wakiitwa "mabeberu"
 
bajeti yoyote ambayo kila mwaka inakuja na mbinu mpya ya kumkamua na kumtoa pesa mwananchi hadi yule wa chini kabisa hiyo ni bajeti mufilisi, bajeti bora ni ile inayompa mwananchi wa kawaida hauweni kwenye kodi...
 
bajeti yoyote ambayo kila mwaka inakuja na mbinu mpya ya kumkamua na kumtoa pesa mwananchi hadi yule wa chini kabisa hiyo ni bajeti mufilisi, bajeti bora ni ile inayompa mwananchi wa kawaida hauweni kwenye kodi...
Wizara ya Fedha na Mipango imeweka mapendekezo mbalimbali yanayolenga kupunguza ugumu wa maisha kwa wananchi kama vile; kuzingatia maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 9% hadi 8%, kufanya marekebisho ya mfuko wa fidia kwa wafanyakazi kupunguza kiwango cha mchango kutoka asilimia1.0% hadi 0.6%, pamoja na kuzingatia maslahi ya wakulima wa mbogamboga na wengineo.
 
Amen, Mwenyezi Mungu atujalie uzima.
Mchanganuo ni huo hapa chini.

 
NADHANI SI VYEMA KUDANGANYANA KWENYE HAYA MAMBO KWA SABABU:

1. Kodi ya majengo kulipwa kupitia mita za LUKU;

å Kwa hakika kabisa kila mwenye LUKU atalipa kodi hii bila kujali uko wapi na umefunga LUKU yako kwenye nyumba au juu ya mti...!

å Tumuulize waziri na serikali ni lini wamefanya survey nchi nzima ili wajue huyu mwenye LUKU namba hii anastahili au hastahili kulipa na tuna siku 5 tu bajeti hii ianze kutekelezwa...?

å Je, si kwamba wataitaka tu TANESCO kupeleka orodha ya wateja wote wa LUKU - TANESCO wizara ya fedha/TRA na kuingizwa ktk mfumo wa kodi moja kwa moja...?

å For sure, katika nchi hii kusema/kuzungumza huwa ni jambo moja rahisi sana lakini utekelezaji huwa ni jambo jingine gumu mno kwake ambapo mara nyingi hukinzana na kauli zao...

å Mfano ulio bado mbichi kabisa, ni huu wa ni agizo la kisiasa la kupandisha madaraja watumishi umma. Kulinakishiwa kwa kila kauli nzuri na tamu kama asali toka kwa viongozi....

å Lakini matokeo yake ni almost zero na kuacha vilio vingi vya wanufaika waliostahili wakiwa hawana la kufanya...!

å Vivyo hivyo, kodi hii italipwa na wanyonge na masikini wachache tu na wengi wenye majengo wanaostahili kulipa kodi hii hawatailipa...

2. Kodi ya line za simu kwa kadiri ya matumizi ya mwenye line...

å Kama ilivyo ktk kodi ya majengo vivyo hivyo itakuwa kwenye kodi hii. Kila mwenye line ya simu atalipa kodi hii na usije ukapigwa butwaa ikawa ni FLAT RATE kwa kila mwenye line ya simu...

å Watu tusiwe wasahaulifu kiasi hiki. Hebu tukumbuke ule mpango wa TCRA na kutoa unafuu wa vifurushi kwa watumiaji wa huduma za simu na internet...

å Kauli za viongozi wa serikali zilikuwa tamu kama asali kwenye masikio ya wananchi...

å Wenye kuona mbele wakakosoa sana. Wasio ona mbele wakashabikia. Ulipokuja utekelezaji, kilio nchi nzima. Na tukarudi kulekule tulikokuwa kabla...!

## Haya mawili, tegemeeni kilio kikubwa zaidi maana LUKU/TANESCO na kampuni za mitandao ya simu wao hawajasema upande wao watakuwa na charge rate kiasi gani kama gharama za kuikusanyia serikali mapato yake...

NINI TATIZO NA SULUHISHO LAKE?

1. Ni udhaifu wa mifumo ya utambuzi ya walipa kodi stahili ktk kila eneo la kodi kunakosababishwa na unevenly distribution of the nation's population. Hii imepelekea wananchi kuwa na makazi yasiyo ktk mpangilio maalumu kiasi kufanya kukusanya kodi ya majengo kuwa ngumu....

2. Suluhisho ni kurekebisha hayo ambako kunahitajika investment kubwa na wakati huohuo kuacha na kuepukana kabisa na siasa zetu za kijinga na kipuuzi ambazo zimeathiri kila eneo la maisha ya watu kijamii na kiuchumi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…