Ukweli kuhusu biashara ya Vanilla

Ukweli kuhusu biashara ya Vanilla

ngongoti2000

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2017
Posts
2,236
Reaction score
2,142
Wadau

Naomba kujua ukweli kuhusu biashara ya Vanilla ambayo inatangazwa sana na jamaa wa Vanilla International wa Vanilla Village wa kule Njombe.

Kwa mahesabu ambayo wamenipa naona faida yake ni mamilioni ya shilingi kwa mfanio ukiwekeza 10m faida yake kwa mwaka huo uikshavuna na kuuza iliyochakatwa ni kama 720m

Sasa hapa nataka kujua kwa nia nzuri tuu kama humu jamvini kuna mtu alishawahi kuwekeza kwenye mradi huu na matokeo yake yakawaje?

Seriously , nataka kujua kabla sijaimimina hela yangu humo!

Pia ukweli wa soko lake la dunia likoje?

Natanguliza shukrani ,karibuni.
 
Niliwahi kusoma mahal hichi kilimo, kinachukua zaidi ya mwaka mmoja kuanzia kupanda, kuvuna, kuanika na kuhifadhi ndani ili ile chemical ya Vanilin ambayo hasa ndo inayolipa hili zao thaman iweze kujitengeneza.

Hii vanilin inatumika sana kwenye kutengeneza manukato, kwan hata ukiwa umeihifadhi tu ndan baada ya kuanika kwa muda mrefu basi hayo maeneo yatakua yananukia sana
 
Niliwahi kusoma mahal hichi kilimo, kinachukua zaidi ya mwaka mmoja kuanzia kupanda, kuvuna, kuanika na kuhifadhi ndani ili ile chemical ya Vanilin ambayo hasa ndo inayolipa hili zao thaman iweze kujitengeneza. Hii vanilin inatumika sana kwenye kutengeneza manukato, kwan hata ukiwa umeihifadhi tu ndan baada ya kuanika kwa muda mrefu basi hayo maeneo yatakua yananukia sana
kuanika tu inachukua karibia miezi sita, anika anua
 
Kinacho fanya kilimo hiki kisiwe rahisi ni kuwa zao hili linahitaji Tender Love and Care TLC kuanzia kwenye kitalu hadi kuanika na kuhifadhi. Ukikosea step moja tu umepoteza ubora.

And must be pollinated by hand
Ndio maana Madagascar wanalima vanilla bora sana
Nasubiri sample toka Tz ili niijaribu kama Ina kiwango
 
duh kwa hiyo hawa jamaa wa Vanilla International ni wapigaji au?....sasa nashangaa kama hivyo wanathubutu kutangaza biashara hii kwenye ITV tena primetime katikati ya taarifa ya habari....halafu wanakuwa wapigaji duh!
 
Iyo 10m iweke kwenye betting... Utakuja kunishukuru siku vannila n scum [emoji56]
Are you sure? Leo kuna mdau amekuja na mizuka kibao anataka kwensa Njombe kwa ajili ya kilimo cha vanilla.
 
Sio rahisi ni long term but reward yake ni uhakika.Kwa Kanda ya kule Njombe ambako watu wamezoea vipato vya kusubiria kwenye miti hadi miaka 7 kwao hili ni zao zuri baada ya miaka 3 kama parachichi inawezekana kusubiria.

Kwa kweli kama una pesa wekeza utakuja kunishukuru maana sioni tofauti na korosho au hayo Mazao mengine ya mda mrefu.
 
Mr.Kuku nae alikuja hivi hivi ila raia walishasahau yaliyotokea wakati wa DECI. Tufanye kazi kwa bidii.
Kuna wale wanaojutangaza ambao wako kwenye soko la hisa jatu sijui jatu
 
Wadau

Naomba kujua ukweli kuhusu biashara ya Vanilla ambayo inatangazwa sana na jamaa wa Vanilla International wa Vanilla Village wa kule Njombe.

Kwa mahesabu ambayo wamenipa naona faida yake ni mamilioni ya shilingi kwa mfanio ukiwekeza 10m faida yake kwa mwaka huo uikshavuna na kuuza iliyochakatwa ni kama 720m

Sasa hapa nataka kujua kwa nia nzuri tuu kama humu jamvini kuna mtu alishawahi kuwekeza kwenye mradi huu na matokeo yake yakawaje?

Seriously , nataka kujua kabla sijaimimina hela yangu humo!

Pia ukweli wa soko lake la dunia likoje?

Natanguliza shukrani ,karibuni.
Usipende kuambiwa kila kitu mkuu fatilia hata mashamba darasa ujionee,nna jirani kalima mwaka wa pili huu hajavuna sio kilimo faida ya haraka tafuta kampuni ya Ney ltd moshi ndio wanadili na hii kitu
 
Vanilla ipo kwenye kundi la viungo ( spice) Shida ya vanilla ipo kwenye uchavushaji wake pia inataka kimvuli na miti ya pembeni ili iweze kutambaa kwenda juu
Kuhusu thamani yake kwenye upande wa viungo ni yapili ukiachana na Saffron
 
Hii saffron kwa Tz inalimwa wapi?

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom