Watu wengi wamekuwa wakipenda sana kuwatisha waliochaguliwa hasa first year kwamba SUA chungu
Si kweli kwamba SUA ni chungu but ni kweli kwamba SUA pana ugumu wake, Kudisco SUA ni kazi na pia ni rahisi
NI RAHISI kwasababu SUA ili ufaulu kwenda mwaka unaofuata according to sheri 13.2 na 13.3 ni lazima uwe na credit hours 16 na kuendelea na GPA ya 2 na kupanda, hivyo unakuta wengi wanashindwa kufikisha credit hours 16 na kudisco na kwa mwaka huu wengi wamedisco wamedisco unakuta wana credit hours 15.5.
NI KAZI KUDISCO SUA kwasababu SUA huwezi kudisco semister ya kwanza mpaka usome zote mbili, na kwa mwaka huu ulioisha kimasomo imeonekana mwaka wa kwanza wengi semister ya kwanza waliharibu but semister ya pili walijitahidi na kujiokoa.
Ki ujumla SUA ni kazi kudisco kama ukifuata sheria zake na kuhudhuria vipindi, sema ni ngumu maana vipindi huwa ni masaa karibia matatu na muda mwingi mnajikuta mpo mnasoma lakini ukiweza kujipanga SUA utaiona rahisi na utakula bata kama kawa. Hivyo first year naomba msiogope na karibuni sana SUA na kwa wale wa MAZIMBU CAMPUS karibuni sana na mtaenjoy sana kuja SUA kama mtakuwa committed, ila naomba ujue kama unapenda mzaha basi SUA sio mahala pake maana hapa sheria inafuatwa hivyo utajikuta umedisco kwa kosa la kijinga sana.
KARIBUNI SANA HOME OF AGRICULTURE