Kashaulo
JF-Expert Member
- Jun 14, 2019
- 2,936
- 4,947
Uko sahaihi, ni kweli kuwa hawa viumbe wamewahi kuwepo lakini kwa bahati mbaya wakawa extinct kabla ya binadamu wa kizazi chetu hiki cha sasa, kuanza kuishi. Kuna mmoja mifupa yake iliwahi kupatikana huko Tengaduruna Tanzania na watafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Idara ya Jiolojia, na sasa mifupa hiyo iko Ujerumani imehifadhiwa kwenye museum ya Berlin, kama sikosei.
Tukirudi kwenye Maandiko Matakatifu Biblia, ni kwamba Biblia inasema tangu Adam na Eva kuumbwa ni takribani miaka 6000 hadi leo, lakini Biblia hiyo hiyo ndiyo inayokiri kuwa Mungu hakuumba Ulimwengu siku ile ile alipowaumba Adam na Eva bali alikuwa tayari ameshaaumba kipindi kirefu huko nyuma, kama vile udong na miamba, katika muda ambao Biblia haitaji urefu wake. Alichofanya kipindi kile cha siku saba ambamo aliwaumba pia Adam na Eva, ni marekebisho ya kile alichokuwa tayari ameumba huko nyuma kama vile:
1. Kutenganisha maji na nchi kavu (maji na nchi kavu vilikuwepo tayari, hakuviumba siku hiyo
2. Kutenganisha anga na mbingu---hivi navyo vilikuwepo kipindi kirefu nyuma
Kwa hiyo ni sahihi kuwa kuna ulimwengu ulikuwepo kabla ya Adam na Hawa, na wana-Sayansi wanaofanya utafiti na kupata matokeo ya umri wa vitu ambavyo ni zaidi ya miaka 6000 wako sahihi na hawapingani na maandiko matakatifu ya kwenye Biblia
Asante sana mkuu kwa kushare nasi elimu hii, kwa sehemu kubwa umenyoosha vizuri ila naomba uweke sawa kipande kile cha “mabaki ya mifupa kuhifadhiwa Berlin”.
Ninavyofahamu mimi yale ni mabaki ya Dinosaur [mjusi mkubwa], sina nijuacho zaidi hata kuhusu alipatikana wapi... hebu nitoe shaka au rekebisha kumbukumbu zako kama yule ni Dragon au ni Dinosaur.?