Ukweli Kuhusu Idadi ya watu 3.9B kuangalia msiba wa Rais Dkt. Magufuli

Wewe jamaa ni mweupe sana kichwani, yani unamuonea wivu hata marehemu??.

Haya lete wewe takwimuzako tuziamini.
 
Mpaka Waziri mkuu anatamka hili ni jambo la kidunia, huwezi liacha hivi hivi.
 
Wachawi sikuzote huwezi watenganisha na husuda plus nongwa.
Ukitaka umuweze chura mpe maji ya moto... ! Chura angekuwa na faida waganga wangemtumia sana lakini hana hana faida kimwili wala kiroho zaidi ya kelele zinazokera
 
Yaani kama rais huyu mpya akiamua japo ni ngumu kufanya ukaguzi wa kina kwenye miradi yote toka 2015 -2020, juu ya matumizi yote ya pesa za serikali, watu watashika vichwa kwa kutoamini watakachokisikia!!
 
Huu mjadala ni mzito na watanzania wakitaka kuuvalia njuga utaleta tafrani Kubwa tuvumilie azikwe kwa Amani kwanza baadae huko mbeleni vyama vya upinzani vitahoji mapungufu yote tokea kuumwa kwa kificho mpaka kufariki kwa kificho
Kwa hiyo tukubali lile libaba liendelee kutudanganya tu?
 
mihemko tu na majisifu kuna watu hawaamini kama amekufa ndio maana wanaendelea na propaganda zao hiyo link fake imetengenezwa na msemaji mkuu wa watanzania nagalieni twitter yake yaani ni aibu, huyu jamaa kimsingi ni kanjanja nilishawahi kusema , sasa kwakua mchawi mchawi na kijazi alimkumbatia kwa ukabila akapewa sijui usemaji sijui ukatibu kaona yeye ndio second to none ,kila kitu anachosema ni habari hata kama kaharisha, nchi ndio imefika hapa tuvumiliane tu
 
Television ngapi zilirusha mpaka kufikia idadi hiyo?? Aligusa mataifa mangapi wakati anaongoza mpaka kukubalika hivyo? Alitikisa mikutano ipi kimataifa akajenga ilojina? Tusimkuuuuze mtu kupitiliza alijitahidi kujengajenga lkn maajaaabu hakuna kaangaliwa sana bongo maana pia watu hawanakazi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…