Pole sana waziri mkubwa...Tunapozungumzia watu billion 3.9, tunazungumzia nusu ya dunia...tuko zama za ulimwengu wa mawasiliano 'information technology' kwa lugha ya kimanyema... Habari huenea kwa kasi zaidi kuliko sauti na kuliko mwanga.. Yaani ni zaidi ya mwendokasi wa supersonic...!!
Dunia imekuwa kama kijiji...lakini kinachofanya iwe kama kijiji ni mitandao ya mawasiliano na vyombo vya habari... Na kwasasa mitandao maarufu na vyombo maarufu kidunia ni TWITTER, FACEBOOK, INSTAGRAM YOUTUBE WHATSAPP , CNN, ALJAZEERA BBC, RT, CCTV, DW, pamoja na redio na tv mbalimbali za Kimataifa
Hawa wote kwa ujumla wao wakitangaza jambo moja kwa wakati mmoja 24/7 ndio walau wanaweza kuifikia robo ya dunia yenye wakazi wasiozidi bilion nane(8,000,000,000,000)
Kwa kumbukumbu ambazo si za kitambo sana na si za karibu sana watu waliosababisha dunia ikasimama na mitandao ya kijamii ika jam ni vifo vya
Princess Diana
Michael Jackson
Kobe Briat
Hawa karibia vituo vyote vya luninga vilikuwa live 24/7 kwenye live coverage.. Mitandao niliyotaja ya kijamii ilizidiwa na wachangiaji na wasomaji...lakini hakuna kati yao aliyefikisha wafuatiliaji billion 3.9..labda pengine Michael Jackson
Waziri mkuu kapata wapi hii hesabu ya 3.9 billion? Sikuona popote mitandao ikijam kwa habari za mwendazake wetu.. Sikuona live coverage world wide...huwezi kuwafikia watu billion 3.9 duniani bila kutumia vyombo vya habari vya kimataifa na mitandao yake
Wenzetu ulaya huwa na rekodi ya kila kituo na kila mtandao kwa idadi ya watazamaji (viewers) je pm anaweza kuweka hizo rekodi?
Vyombo na mitandao ya kijamii ya ndani ya Afrika havikuwa na live coverage...hii hesabu ya 3.9 billion waziri mkubwa kaipata wapi?
Ni wazi pm wetu kadanganya kisha akadanganyika kama vile alivyoaminishwa kuwa boss wake ni mzima wa afya na anachapa kazi.... Kama alikuwa anajua ukweli kisha akaamua kupotosha basi kuna tatizo kubwa pahala...
Mungu ibariki Tanganyika..!!!