TATIBU SALUM
New Member
- Jul 6, 2015
- 3
- 12
UKWELI KUHUSU KAMARI
Habari yako mwana jf unaesoma uzi huu, leo nataka nizungumze na wewe, uwe mkamali au sio mkamalia huu ni ujumbe muhimu kwako
KAMARI NI NINI
Kamari ni mchezo wa kukusanya pesa kwa washiriki na kumpatia mmliki, kisha mmiliki kutoa kiasi kidogo kwa baadhi ya washiriki ili kuwatia moyo muendelee kucheza mzunguko ujao, pesa nyingi inayobaki inaingia kwenye mfuko wake,
mfano wachezaji 100 jumla ya pesa zote walizostake ni MILIONI 30, mmiliki hutoa milioni 10 kwa baadhi ya washiriki watakaosadikika ni washindi, kisha MILIONI 20 iliyobaki inaingia mfukoni mwake, washiriki wengine waliopoteza watatafuta pesa ili wastake tena wakihisi wanaweza kuwa washindi kwa mzunguko ujao, na wale washindi wa awali wakicheza tena wanapoteza pesa zote, wanatafuta pesa nje ili wajaribu kucheza tena wakihisi watapata ushindi mkubwa, jambo ambalo si kweli, hakuna mafanikio yanayopatikana kwa kamari, hata ikitokea kwenye mzunguko ukapata Milioni 100, kaa ukijua kwamba wakati ujao utaliwa zaidi ya hiyo pesa hata kama hauna uliitumia utajua pa kuipata ili lazima tu irudi ikiwa na zaidi,
PESA YA KAMARI UKILA UTAHITAJI KUENDELEA KUCHEZA ILI ULE ZAIDI UPATE MAFANIKIO UKIHISI KUNA PESA ZA BURE, UKILIWA UTAHITAJI KUWEKA PESA NYINGINE ILI URUDISHE PESA ULIZOLIWA, MWISHO WA YOTE UTAKUA NA MAISHA MAGUMU NA PESA UNAZOZIFUKUZIA KAA UKIJUA HUTOWEZA KUZIPATA
URAIBU WA KAMARI NA HASARA ZAKE
Kamari ina athari kubwa kuanzia kwenye maisha binafsi ya mkamalia, familia, ndugu, marafiki, na jamii yote inayomzunguka
1) Mkamalia hawezi kukaa na akiba kuna wakati hata anaweza akalala na njaa japokua kazi anafanya na pesa anapata ila zote zinapotelea kwenye kamari
2) Kuingia kwenye madeni makubwa na yasiyo na ulazima na mengine ambayo hauna hata uwezo wa kuyamudu mwisho wake ni kuwa mwizi, tapeli ili upate pesa nyingi kwa haraka uweze kulipa mwisho wake ni mbaya zaidi
3) Kutengwa na ndugu jamaa na marafiki, na kuna muda utahisi watu ni wabaya, hawakupendi, kumbe tatizo ni kamari pia inaweza kusababisha hata migogoro kazini, kunawakati unaweza kufikiria hata kutoweka Duniani kwa changamoto unazopitia kutokana na uraibu huo
4) Kupata magonjwa kama magonjwa ya moyo, afya ya akili, n.k, waliowahi kucheza wakapoteza kiasi kikubwa cha pesa wanaelewa hali inavyokuwa,
KUJINASUA KWENYE URAIBU WA KAMARI
kitu kikishakuwa ni uraibu ni ngumu kuacha kwa sababu nafsi na mwili wako vyote vimeshindwa kujizuia hata watu wakuseme, wakulaumu wakiondoka tu, unarudi kwenye uraibu wako, unaweza ukajilaumu na kuapa kutorudia tena lakni mwisho wa siku ukishika pesa unarudi kule kule ulipotoka, unaweza ukapoteza pesa nyingi na yenye umuhimu ukaumia, ukaingia matatizoni, ukakiri kujizuia lakini mwisho wa siku pia narudia,
SULUHISHO
Leo nataka nitoe tiba kwa wenye uraibu huo tu na wenye nia ya dhati ya kutaka kutoka kwenye hiyo changamoto, kama umeshaathirika umepoteza pesa, au kila ukipata pesa zinapotelea huko tuwasiliane,,,, ila kama wewe ni muhanga umeshaathirika kila ukipata pesa unawaza kuendelea kubeti na hutak kuacha ukidhani siku 1 utafanikiwa kupata pesa nyingi au kurudisha pesa ulizopoteza endelea kupambana usinitafute, sina tiba ya kukufanya ushinde, ila ninauwezo wa kukutoa kwenye hiyo changamoto tu
MUHIMU: UZI HUU HAUNA LENGO LA KUHARIBU BIASHARA AU KAMPUNI YA MTU, NI KWAAJILI YA KUWEZESHA VIJANA KUTOKA KWENYE WIMBI LA MATESO NA KUTOKUFANYA KAZI