"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

Mwangos aliuliwa na askar saba tena kwa bomu mchana kweupe na picha zilionyesha waliohusika lakn uchunguz ulionyesha askar hawakuhusika moja kwa moja. Je uchunguz huu polis jamii sita wenye mikanda ya polis, saa nane usiku, wala hamna picha, je uchunguz si utaonyesha polis jamii hawajahusika kabisa.


Watasema ni majangili toka kenya yalikuwa yanaenda SAA NANE Island
 
Hii video naona wanasema ni toyota double cabin na wakati habari nyingine zinasema ni RAV4,yani vurugu tupu!bongo bana!Which one should be reliable?

Kama kuna RAV4 Double cabin,then ma bad!
 
Last edited by a moderator:
Hawa jamaa huku "site" wanachukiwa kishenzi. Tuendako si ajabu visasi vikawa nje nje!.. BILA HAKI KWA WOTE HAKUNA AMANI KWA WOTE!.
 
Mimi nadhani hii issue ni zaidi ya 'mke wa mtu'. Kama ilikuwa ni mke wa mtu basi mwenyewe/wenyewe wangeshamshughulikia siku nyingi maana kuna taarifa kwamba amekuwa na huyo mwanamama kwa muda. Hapa kunaweza kuwa na' mlundikano' wa mambo sasa wamepata nafasi kupitia kwa huyo mama. Sad!

Heshima yako mkuu, hata mimi nilikuwa nahisi hivyo, mume wa mtu hawezi kutekeleza kitu kama hicho wakati anajuwa wazi wazi kwamba yeye ndiye angekuwa first suspect - haingii akilini MKUU - naye hawezi kuwa mjinga kiasi HICHO.

Kwa mawazo yangu kuna kitu cha zaidi sio mke wa mtu i.e mlundikano wa mambo kama unavyo sema, watu wenye nia mbaya au bifu na jamaa wanaweza kuchukulia incident ya juzi kugilibu watu akili ili ionekane ni muendelezo wa mambo ya wanawake - wawatafute watu anao shirikiana nao kibiashara kama alikuwa ana shughuli za ziada za kumuongezea kipato na wala hiyo si dhambi. Lakini waki-dwell kwenye mambo ya kumuhoji mwanamke sijuhi nini, watakuwa wanapoteza muda.

Tukiwa wakweli POLISI wa TANZANIA wakiamua kuvalia njuga tukio fulani hawashindwi kitu mkuu (namaanisha katika nyanja za investigation sio vurugu za kupiga raia mikutanoni) ni kweli wako mahili sana katika mambo ya upelelezi, nina hakika wahusika watatiwa mbaroni - cha muhimu hapa waweke kila kitu adhalani ili liwe fundisho kwa vizazi vijavyo na kusafisha jina la TAIFA letu lililo tiwa dosari na kisa hiki cha kusikitisha.

Mimi katika maisha yangu yote hapa TANZANIA na nje ya Tanzania sijawahi kusikia Commander wa Polisi kauwawa eti na majabazi!!! - hii inaleta picha mbaya katika TAIFA letu, we unafikili RAIA na Wageni wanapo kisikia kwamba mlinzi mkuu wa Usalama wa mkoa kauwawa na majambazi si itaonekana TAIFA letu alina USALAMA tena - TAIFA linapaswa kufanya kazi ya ziada kurudisha imani ya usalama kwa RAIA na wageni wanao tembelea TANZANIA, tukilaza damu mahasimu wetu jambo hili watalikuza out of proportion kwa kutujengea jina BAYA.

R.I.P kamanda Barlow.
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Sasa ndio Maana wakatuwekea PICHA za NYUMBANI kwa huyo Mwanamama kama pia Ameuawa na aliyetoa habari ni NDUGU ya HUYO POLISI aliyekuwa kwenye KIKAO?

HUU NI UOZO; What GOES around COMES around!!! KIKWETE na MWEMA watasema nini? it is a CCM STYLE...
 
ninafarijika sana kuona polisi nao wakiuwawa kwani wao wamejifunza kutuuwa tu kumbe nao wanakufa. hii ni mkuki kwa nguruwe, hatufurahii misiba ila kuna mingine lazima turidhike nayo.
 
hakuna anaependa binadamu mwenzie afariki,lkn kwa hili polisi wajifunze kitu wanajisahau sana na kujiona miungu watu hapa duniani,haiingii akilini igp anakurupuka kutoa taarifa marehemu alimpelka dada yake kbl hajapata usahihi alikuwa na nani tayari ameshatia doa taarifa yoyote itakayotolewa na jeshi lake.pia uwezekano wa chanzo cha kifo kuwa ni mapenzi umechukua asilimia 75 ingawa huyo dada hakuwa na mme ila alikuwa na jamaa mwingine baada ya kumpata marehemu akaanza mbwembwe!rip kamanda
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow
APIGWA RISASI SHINGONI NA WATU WASIOJULIKANA
Frederick Katulanda, Mwanza
SIMANZI imegubika Jiji la Mwanza na vitongoji vyake baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (55), kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa manane wa kuamkia jana.Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Said Mwema alithibitisha tukio hilo akieleza kuwa amemwagiza Kamishna wa Makosa ya Jinai nchini, Robert Manumba kwenda kuchunguza mauaji hayo."Tunasikitishwa kwa mauaji hayo na ninawaomba Watanzania wawe watulivu wakati tukishughulikia kuwakamata watu waliohusika katika tukio hilo," alisema IGP Mwema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.


Mbali ya kumuua Kamanda Barlow, wauaji hao waliokuwa wamevalia makoti yanayovaliwa na watu wa ulinzi shirikishi (Polisi Jamii), walichukua na bastola ya kamanda huyo, simu mbili za mkononi pamoja na ‘radio call' ya Jeshi la Polisi.

Hili ni tukio la tatu kwa Ofisa wa juu wa Polisi kuuawa mkoani Mwanza. Tukio la awali lilitokea mwaka 2007, ambapo aliyekuwa Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Mwanza, ASP Mahende aliuawa kwa kupiga risasi eneo la Bugando saa 4:00 usiku wakati akifuatilia majambazi waliokuwa wakijitayarisha kuvamia.
Mwaka 1987, Inspekta Gamba aliuawa na majambazi katikati ya Jiji la Mwanza.
Kamanda Barlow aliuawa wakati akiendesha gari lake binafsi, aina ya Toyota Hilux Double Cabin na wakati wa tukio hilo hakuwa na mlinzi wake kwa kuwa kamanda huyo alikuwa katika shughuli binafsi.
Hata hivyo, mauaji hayo yamezua hisia tofauti huku wengine wakieleza kuwa ni kifo cha bahati mbaya na kwamba, wauaji walidhani ni mwananchi wa kawaida na wengine wakisema huenda ulikuwa mpango maalumu uliolenga kumwangamiza kwa kulipiza kisasi.
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa
Akizungumza na waandishi wa habari jana saa 2:57 asubuhi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kuwa kifo cha Kamanda Barlow kimetokea saa 8:00 usiku katika eneo la Kitangiri, Barabara ya Kona ya Bwiru karibu na Hoteli ya Tai Five.

Alisema kuwa kamanda huyo aliuawa alipokuwa akimrejesha mmoja wa wanawake waliokuwa nao katika kikao cha maandalizi ya harusi ya ndugu yake.
Mkuu huyo wa mkoa alimtaja mwanamke huyo aliyekuwa na marehemu kuwa ni Doroth Asasia Moses ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyamagana B.
"Marehemu alikuwa katika kikao cha harusi ya anayedaiwa kwamba ni mtoto wa dada yake, Semburi Moleto kilichofanyika katika Hoteli ya Florida, Mtaa wa Rufiji. Kikao kilipomalizika tunaambiwa majira ya kati ya saa 4 hadi 5 usiku, alimchukua mwanamke huyo kama ‘lift' ili kumsaidia kufika nyumbani kwake,"alieleza.
Alisema kuwa alipofika nyumbani kwa mwanamke huyo aliona watu waliokuwa wakimulika tochi waliokuwa wakilalamika kuwa wameumizwa na mwanga wa taa za gari lake.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema walipofika katika gari, aliwauliza iwapo wanamfahamu na waliposhindwa kumjibu Kamanda Barlow alichukua radio ya mawasiliano ya kipolisi ili kuwasiliana na askari wake, ndipo wauaji hao walimpiga risasi eneo la shingo na kufariki papohapo.
"Kamanda wetu inaonekana amefariki kutokana risasi hiyo, ambayo imemvunja shingo yake na imepigwa kutokea upande wa kiti cha abiria na kumpitia begani na kuingia shingoni," alisema Ndikilo na kufafanua:

"Baada ya kumuua, watu hao walipora bastola yake, ‘radio call' hiyo pamoja na simu zake mbili za mkononi na mwanamke huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano na kusaidia upelelezi."

Kilichomponza RPC
Habari za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinamkariri shuhuda wa tukio hilo (Dorah) akieleza kwamba, kilichomponza Kamanda Barlow ni kuwadharau wauaji hao baada ya kuona wamevalia vikoti vyenye rangi ya kijani vilivyokuwa na maandishi ya Polisi Jamii, alidhani kuwa na watu wa ulinzi shirikishi.

Baadhi ya maofisa wa polisi wameeleza kuamini kuwa watu hao walikuwa ni Polisi Jamii ndiko kulikomponza marehemu Barlow kwa kuwa aliamini kuwa alikuwa katika mikono salama, hali ambayo ilimfanya kutojiandaa kupambana nao.
Mwalimu Doroth
Mwalimu Doroth aliyekuwa na marehemu wakati wa tukio hilo, ambaye kwa sasa anashikiliwa kuhusiana na mauaji hayo ni mjane wa marehemu Modest Lyimo ambaye zamani alikuwa ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), aliyefariki mwaka 1997 wakati huo Kamanda Barlow akiwa na OCD wa Kituo cha Kati.

Lyimo alifariki na kumwacha Doroth akiwa na mtoto mmoja, lakini baadaye mwalimu huyo alizaa watoto wawili na mwanamume mwingine hivyo kuwa na watoto watatu (majina yanahifadhiwa kwa sasa).

Eneo la mauaji
Mwandishi wa gazeti hili alipofika nyumbani kwa Mwalimu Moses alikuta askari watatu wa jeshi la polisi wakilinda na kumkagua kila mtu aliyekuwa akiingia katika nyumba hiyo na kutoka.

Mauaji yalivyotokea
Mmoja wa watoto wa mwalimu huyo, Kenrogers Edwin, ambaye alishuhudia tukio hilo la kuuawa kwa Kamanda Barlow, aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa siku hiyo usiku kabla ya tukio, alipigiwa simu na mama yake aliyemwarifu kuwa alikuwa amefika na kumtaka amfungulie mlango.

Edwin alisema kuwa anakumbuka pia katika maongezi ya simu mama yake alimweleza kwamba alikuwa akija na mgeni kwa ajili ya kutambua nyumbani anapoishi.

Alisema kuwa wakati akifungua geti ili gari alilokuwamo mama yake (Doroth), pamoja na mgeni wao (Kamanda Barlow) liingie ndani, aliona watu wakiwa wamezunguka gari hilo.

"Ilikuwa saa 8 usiku, nilipofungua geti ili aingie, niliona watu watatu wakiwa upande wa dereva wa gari na wawili upande mwingine aliokaa," alisema na kuongeza:
"Niliona wakimnyang'anya mama mkoba na simu na nilisikia wakibishana, lakini baadaye nilisikia mlio wa risasi."
Alieleza kwamba anakumbuka kuwa baada ya mlio huo wa risasi alilazimika kulala chini kwa kuogopa na kwamba baada ya Kamanda Barlow kupigwa risasi, wauaji hao walikimbia walipoona pikipiki ikija eneo hilo kwa kasi.

Aliyemhudumia Baa
Mhudumu wa baa, Benard Kanyabukala, ambaye alimhudumia Kamanda Barlow katika kikao hicho alisema kuwa baada ya kikao hicho kumalizika, kamanda huyo aliagiza sanduku moja la bia kwa ajili ya wajumbe waliokuwapo katika kikao hicho na yeye (mhudumu) alinunuliwa kinywaji aina ya Alivaro.

"Aliomba bili na nilipompa alinifokea akidai nimemzidishia bei. Awali nilimweleza kuwa bei ya kreti ni Sh36,000, lakini kutokana na baadhi ya watu kutokunywa bia na kubadilisha vinywaji bei ilizidi na kuwa Sh40,700, ingawa baada ya kumwelewesha alilipa na kuongeza bia nyingine kwa raundi ya mwisho zenye thamani ya Sh 30,800," alisema Kanyabukala.
Alieleza kwamba, wakati wa kikao hicho Kamanda Barlow alikuwa akinywa bia aina ya Serengeti, lakini mara ya mwisho alipoagiza vinywaji alikunywa maji ya Kilimanjaro na waliondoka hapo saa 8:30 usiku akiwa na mwanamke mmoja.
Mmiliki wa baa
Mmiliki wa baa ya Florida, kilipofanyika kikao hicho, Ritha Mosha alielezea kuwa, Kamanda Barlow alifika katika baa hiyo kwa mwaliko wa Semburi Moleto, ambaye yeye na Kamanda Barlow wote ni Wachaga waliozaliwa Kijiji cha Kiyou, Tarafa ya Vunjo Marangu, mkoani Kilimanjaro.

"Mimi ilikuwa ni mara yangu ya pili kuonana naye siku hiyo. Kijana anayetarajia kuoa alinieleza kuwa, alimwomba Kamanda Barlow amsimamie kama mzazi wake katika arusi yake na ndiye aliyesimamia kikao hicho, ndiyo aliyeongoza sala ya kufungua kikao hicho," alieleza Ritha.
Alisema kuwa kikao hicho kilichelewa kuanza kutokana na wajumbe kuchelewa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini hapo.
Alifahamisha kuwa kikao hicho kilianza saa 2:21 usiku na kwamba kamanda huyo alikuwa msemaji wa familia.
Idadi ya wanawake
Ritha alifahamisha kuwa, kikao hicho kilitarajiwa kuwa na wajumbe 100, lakini walifika kati ya 55 hadi 60 na kati ya hao kulikuwa na wanawake wawili ambao aliwataja kwa majina ya Christina Mosha, mkazi wa Nyakato na Doroth ambaye alisindikizwa na kamanda huyo.
 
kuna wanawake wanatutia aibu sana!laiti wangejua thamani ya hii kitu!

sasa na huyo mama anapata zali la kumegwa na mkubwa the bado anaishi uswazi?
au alikuwa anafaidi kunywa bia na michemsho?
by the way so wale walomuua mwagosi ndo wamemuua bos wao au /
sielewi polisi jamii ndo wapi hao
 
angalizo polisi msijeanza kazi yenu ya kukusanya machinga wasiokuwa na hatia bila sababu kwa mambo wasioyajua au mambo ya kijinga kama ya mzinzi
 
Ritz leo umekuwa mkweli sana!! Nimekupa na like Mkuu!! Kumbe ukiamua unaweza!! Ha ha ha ha !!!Wameshikwa pabaya. Sasa sijui IGP atoakuja tena na Press Release nyingine au yataisha kimya kimya kama yale ya Ulimboka na Mwangosi?

tatizo la watz ni kuwa tuna mambo yetu tumeamua yatupofushe macho. Hapo kwa kuwa imeingizwa issue ya kuwa na nje wa mtu wote tutafumbia macho possibilities nyingine zote zinaweza kuelezea mauaji haya. Kwani huyu mama hawezi kuwa ni sehemu ya mpango maalum ulioandaliwa kummaliza huyu kamanda? Watu kama Ritz wanapotoa comments zinazotaka kutuaminisha kuwa chanzo cha mauaji ni nje wa mtu, hatushtuki hata kidogo. It is time watz tuache kuendeshwa kwa hisia tu, kwa kuwa mtu angetembe na nje wangu ningewish afe, isinifanye nishindwe kuchambua matukio kwa umakini unaotakiwa.
 
Mod Tafadhali usiunganishe thread hii. Najua iko inayoripoti kifo, iko ya maswali.

Hii inahusu majibu na revelations zilizoingia kwenye dish langu.
===========

-Kamanda Barlow alikuwa na mwanamke ndani ya gari wakiwa peke yao wawili
-Mwanamke si dada yake wala ndugu yake
-Lilikuwa gari la binafsi na Kamanda aliendesha mwenyewe.
-Walitoka kwenye kikao La Kairo Hotel na siyo Florida Hotel kama IGP alivyosema katika taarifa yake
-Walipofika Kitangiri, Kamanda aliamua kumpeleka yule mama ndani kwnye uchochoro badala ya kumwacha barabarani
-Si mara ya kwanza Kamanda kumpeleka mama yule eneo lile
-Walipoingia uchochoroni, waliwakuta the so called "polisi jamii" wakiwa kwenye doria
-Kamanda alishusha kioo na kuwauliza ni kina nani, na wao walimjibu kuwa ni polisi jamii.
-Aliwahoji kwa nini wamevaa mikanda ya polisi wakati waliishazuiwa
-Ulitokea ubishi kidogo
-Kamanda akainua redio call kuwaita vijana wake waje kuwakamata
-Polisi jamii wakamdaka kumnyanganya redio call hiyo na kumpiga risasi ya shingoni
-Wakamvuta na kumlaza chini ya uvungu wa gari
-Yule mama ndiye aliyemwita mlinzi wa RPC na kumwambia aje kumchukua "mzee" maana ameuawawa
-Mama anaisaidia polisi hata sasa.

MY Take:

-Jeshi la polisi linajaribu kusafisha hali ya hewa kwa kufanya damage control
-Mme wa mama yule amekuwa akilalamika kuwa analiwa mali yake
-Kuna uwezekano, polisi jamii walijua kamanda anakuja saa ile na yule mama, na walitekeleza maagizo waliyopewa
-Kuna other underlying issues ndani ya jeshi la polisi Mwanza
-Uchunguzi hautapata ushirikiano wa kutosha kwa sababu ya chuki kubwa kati ya jamii na jeshi hilo.



Wakuu!

Yale yale ya Delila na Samsoni.
 
Kwa mawazo yangu kuna kitu cha zaidi sio mke wa mtu i.e mlundikano wa mambo kama unavyo sema, watu wenye nia mbaya au bifu na jamaa wanaweza kuchukulia incident ya juzi kugilibu watu akili ili ionekane ni muendelezo wa mambo ya wanawake - wawatafute watu anao shirikiana nao kibiashara kama alikuwa ana shughuli za ziada za kumuongezea kipato na wala hiyo si dhambi. Lakini waki-dwell kwenye mambo ya kumuhoji mwanamke sijuhi nini, watakuwa wanapoteza muda.

Tukiwa wakweli POLISI wa TANZANIA wakiamua kuvalia njuga tukio fulani hawashindwi kitu mkuu (namaanisha katika nyanja za investigation sio vurugu za kupiga raia mikutanoni) ni kweli wako mahili sana katika mambo ya upelelezi, nina hakika wahusika watatiwa mbaroni -


hapo kwenye red uko serious kweli ndugu..tafadhali bana
 
mod tafadhali usiunganishe thread hii. Najua iko inayoripoti kifo, iko ya maswali.

Hii inahusu majibu na revelations zilizoingia kwenye dish langu.
===========

-kamanda barlow alikuwa na mwanamke ndani ya gari wakiwa peke yao wawili
-mwanamke si dada yake wala ndugu yake
-lilikuwa gari la binafsi na kamanda aliendesha mwenyewe.
-walitoka kwenye kikao la kairo hotel na siyo florida hotel kama igp alivyosema katika taarifa yake
-walipofika kitangiri, kamanda aliamua kumpeleka yule mama ndani kwnye uchochoro badala ya kumwacha barabarani
-si mara ya kwanza kamanda kumpeleka mama yule eneo lile
-walipoingia uchochoroni, waliwakuta the so called "polisi jamii" wakiwa kwenye doria
-kamanda alishusha kioo na kuwauliza ni kina nani, na wao walimjibu kuwa ni polisi jamii.
-aliwahoji kwa nini wamevaa mikanda ya polisi wakati waliishazuiwa
-ulitokea ubishi kidogo
-kamanda akainua redio call kuwaita vijana wake waje kuwakamata
-polisi jamii wakamdaka kumnyanganya redio call hiyo na kumpiga risasi ya shingoni
-wakamvuta na kumlaza chini ya uvungu wa gari
-yule mama ndiye aliyemwita mlinzi wa rpc na kumwambia aje kumchukua "mzee" maana ameuawawa
-mama anaisaidia polisi hata sasa.

my take:

-jeshi la polisi linajaribu kusafisha hali ya hewa kwa kufanya damage control
-mme wa mama yule amekuwa akilalamika kuwa analiwa mali yake
-kuna uwezekano, polisi jamii walijua kamanda anakuja saa ile na yule mama, na walitekeleza maagizo waliyopewa
-kuna other underlying issues ndani ya jeshi la polisi mwanza
-uchunguzi hautapata ushirikiano wa kutosha kwa sababu ya chuki kubwa kati ya jamii na jeshi hilo.


kaka hebu tupe ushahidi nasi turidhike kwenye hizo red na pili polisi jamii kwa tafsiri ipi maana nijuavyo mimi polisi jamii ni sungusungu na huwa silaha yao ni marungu na mapanga, na kwanini wampige risasi
 
Mengi yatasemwa ngoja tusubili na bwana Manumba naye anakuja na lipi?
 
huyo mwenye mke si aingie humu JF atuweke wazi! au ndo watamdaka akawasaidie pamoja na mke wake?
 
tunasikitika kwa kila roho inayopotea kwa ukatiri, tunaposema haki za msingi za raia,haiondoi maaskari wetu, poleni sana

vile vile tusikitike kwa watu kutumia MADARAKA WALIOPEWA NA MAMLAKA ZA NCHI au NPESA ZAOo kuiba WAKE WA WATU wengine wasio na madaraka au pesa.

Siku zote Mola yu pamoja na wenye kudhulumiwa.


lakin tujiulize JE HUKO TANZANIA KUNA VIKAO GANI VYA HARUSI VYA SAA NANE USIKU?
 
"Dada yake" kumbe mke wa mtu?,Jamani!juzi kati askari uhamiaji alikoswa kwenye mtego wa polisi,Na sasa Bosi wa Polisi Kanasa.Sijui nani atabaki.
 
Back
Top Bottom