"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

Kwani kutembea na hawala au mke wa mtu kama unavyojaribu kutaka kuaminisha umma kuna halalisha mauaji! Mbona unaleta chuki binafsi mkuu........?!!!
 
Da inanikumbusha wimbo wa bahati bukuku Dunia haina huruma,Mke wake sijui alikuwa anamdanganya nini kila mara anarudi kesho yake home.

Anasema shughuli za kikazi
 
Kwani kutembea na hawala au mke wa mtu kama unavyojaribu kutaka kuaminisha umma kuna halalisha mauaji! Mbona unaleta chuki binafsi mkuu........?!!!

Issue ya mke wa mtu ogopa. Ikijulikana mwenyewe anaona bora akuondoe duniani so mleta mada amegusa kwenyewe make taarifa za polisi ndo zinachanganya, kwaki hao majambazi walipora hiyo gari, au ni watu waliondoka na roho ya m2
 
Kweli kabisa ina onekana kabisa hii ishu ili pangwa kabisa na mwenye mke!

Mke wa mtu ni sumuuu
yaaayaayaaa,yaayaayaayaaaah
usijribu chombezaaaaaaaaaaaaaaa
yatakuja ya kukutee, yaaaaaaaaa
yaliyo mkuta kamandaaaaa!
Yayayayaayaaah.

Samahani nahitaji mke wa mtu leo ucku maana kuna panya wananisumbua thana. Nackia 'MKE WA MTU NI THUMU'
 
Jembe Barlow! Lala na matumaini ya kuja kwa Yesu Kristo! Amen....
 
Walimu watoboa mahusiano ya mwenzao, RPC Barlow (Nipashe 16 October, 2012)


Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Nyamagana wamevunja ukimya na kueleza kile kinachodaiwa ni mahusiano kati ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow, na mwalimu mwenzao, Dororth Moses.

Wakizungumza na NIPASHE shuleni hapo jana, pia walielezea kusikitishwa kwao na jinsi tukio hilo la mauaji ya RPC lilivyotokea mbele ya mwalimu mwenzao, Doroth Moses aliyeuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia Jumamosi eneo la Kitangiri, jijini Mwanza.

Mwalimu Doroth ndiye aliyekuwa na RPC Barlow ndani ya gari wakati watu wanaosadikiwa kuwa majambazi walipowavamia na kumuua kwa kumpiga risasi Kamanda huyo.

Katika mahojiano hayo Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule hiyo, Mary Ngalula, alisema wanamuonea huruma mwalimu mwenzao kutokana na kushuhudia tukio hilo la kutisha.

Alisema wanamsikitikia kwa sababu jamii imeanza kumfikiria vibaya kwa kudhani anahusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.

“Tunamuonea huruma mwalimu mwenzetu kutokana na maneno tunayoyasikia, lakini sisi tuko pamoja naye kwa sababu tunamfahamu ni mtu safi, na hivi tunajiandaa kwenda kumuona na kumtia moyo ili amudu kuilea familia yake kwani ni mjane,” alisema.

Mwalimu Baraka Magafu alisema tofauti na hisia za baadhi ya watu kuhusu uhusiano wa Mwalimu Doroth na Kamanda Barlow, wao (walimu) wanafahamu kuwa ni watu wa kabila moja wanaotoka kijiji kimoja huko Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Alibainisha kuwa Mwalimu Doroth amekuwa ni mtu anayejihusisha sana na shughuli mbalimbali za watu wa kabila lake (Wachaga), hivyo hakuna sababu ya kumfikiria vibaya kwa sababu tu mtu aliyekuwa amemsindikiza nyumbani wakitokea kwenye kikao cha maandalizi ya harusi aliuawa kwa kupigwa risasi.

“Ukifuatilia mwenendo wa tukio lote, utaona kwamba kilichotokea ni bahati mbaya na kingeweza kumtokea yeyote, kwani Barlow alikuwa akimsindikiza Mwalimu Doroth nyumbani kwake, na hata baada ya tukio, alipowapigia simu wenzao waliokuwa nao kwenye kikao walikuwa ndipo na wao wanafika majumbani mwao,” alisema.

Aliongeza kwamba katika mazingira kama hayo ni makosa kuwa na mtazamo hasi dhidi ya Mwalimu Doroth kama ambavyo baadhi ya watu wameanza kuvumisha kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Wakati huo huo, majonzi, simanzi na kauli za kulipa kisasi ni miongoni mwa mambo yaliyogubika shughuli ya kuuaga mwili wa Barlow.

Mwili wa Barlow uliagwa na wakazi wa Jiji la Mwanza wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, katika shughuli iliyofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana jana.

Baada ya shughuli ya kuagwa mwili wa Barlow, ulisafirishwa baadaye jana jioni kwa ndege kuelekea jijini Dar es Salaam kabla ya leo kusafirishwa kwenda kijijini kwake Vunjo, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
 
POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU ILA SIO KWA JESHI LA POLISI. NAO WAONE MAUMIVU YA WATANZANIA WENGI WANAOUWA BILA HATIA TENA NA POLISI
Manumba keshasema polisi walipe kisasi sasa subiri uone watakavyoua watu kila siku utasikia majambazi yameuawa kwa kutaka kufanya uporaji baada ya majibizano ya risasi...Polisi wataua sana utafikiri risasi zina macho
 
walimu watoboa mahusiano ya mwenzao, rpc barlow (nipashe 16 october, 2012)


alibainisha kuwa mwalimu doroth amekuwa ni mtu anayejihusisha sana na shughuli mbalimbali za watu wa kabila lake (wachaga), hivyo hakuna sababu ya kumfikiria vibaya kwa sababu tu mtu aliyekuwa amemsindikiza nyumbani wakitokea kwenye kikao cha maandalizi ya harusi aliuawa kwa kupigwa risasi.


saa nane za ucku?
 
Manumba keshasema polisi walipe kisasi sasa subiri uone watakavyoua watu kila siku utasikia majambazi yameuawa kwa kutaka kufanya uporaji baada ya majibizano ya risasi...Polisi wataua sana utafikiri risasi zina macho

Subiri tuone
 
Sukari ya Mungu ina madhara yake,unamsindikiza mke wa mtu usiku?
Polisi mje na fukia fukia ripoti kama kawaida yenu.
 
jaman marehemu si anasifiwa baada ya kufa,mbona apa hali ya ewa imechafuka
 
Wakuu, mimi nasubiria kwa hamu mtu mwenye taarifa kutoka kwa ndugu waliokuwa nao kwenye "HICHO KIKAO CHA HARUSI" ili waeleze jinsi walivyoondoka baada ya kikao na kikao kilimalizikaje saa hizo za usiku wamanane. Pia tungetamani kusikia harusi hiyo ni ya nani na ana mahusiano gani na huyu kamanda pamoja na huyu binti.
 
Wana JF,naamini mambo mengi yameshakuwa wazi hadi sasa kuhusu kifo cha Barlow na kesho anazikwa.Naomba tujuzane ukweli tupu kuhusu haya maswali machache.
1. Ukweli wa udada na kaka wa RPC na yule mwalimu-Ndugu au mke au mashoga zao tujuzeni.
2. Je yaweza kuwa ni Kisasi cha Kundi fulani?
3. Kijana mwenye ile Harusi amewekwa ndani pia?
4. Account ya Mwl Doroth imechekiwa na ina Tsh Ngapi?-Mchaga huyo aweza kuwa alipewa mzigo mzuri na RPC wa rushwa kutoka sehemu fulani then bila hiana mama kaamua kusuka deal hata kama ni kaka yake kabisa.
5. Mke wa RPC hana wivu wa mapenzi kweli hadi kasuka deal hiyo?Ni mchaga wa wapi mke wa Barlow?Chunguzeni account zao wachaga hao wanataka kula life may be
6. Bunduki ya RPC ipo?inawezekana walitumia hiyo kumuua jamaa maana alikuwa amekunywa creti tatu za urabu?
7.Hakuna kesi yoyoye ya hatari mezani mwa RPC iliyofika hadi sasa?Angalieni mafaili aliyoyaacha kama kuna kesi yaweza kusababisha watu wamtoe roho huyu jamaa.

N.B:Naomba tupeane updates halisi baada ya mengi kusemwa,najua akizikwa vitu kibao vitaletwa na serikali ikiwa ni pamoja na kuwaziba midomO kwa posho kama kwa ulimboka!

Pendekezo:Naomba asichukue mtu huyu mama wa RPC najua akaunti yake iko vizuri na mimi nipumzike na maisha,najua ana majonzi makubwa ila by next week na mimi nianze kumpoza Dar,mwanza watanipiga nondo!Nafanya kama Barlow kwa Mwl Doroth baada ya kufiwa na mumewe hahhahahahahaahhh just a joke
.
 
Kamanda Barlow sasa tumuombee apumzike kwa amani,Mwenyezi Mungu ampe kuona pepo yake.
Mambo mengine ya Mwl.Doroth alikuwa na uhusiano gani na kamanda haiwezi kutusaidia kumrejesha duniani.
R.I.P Kamanda Barlow!
 
Back
Top Bottom