"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

"Ukweli" kuhusu kifo cha RPC Barlow ni huu hapa...

Kamanda naye alikuwa analeta dharau unatafuna mali za watu halafu unakwenda kujiachia mpaka maeneo ya jamaa.

Mkuu mbona inasemekana hule mama ni mjane tangu 1997 alipofariki mume wake!
 

-Mme wa mama yule amekuwa akilalamika kuwa analiwa mali yake

Kuna thread humu umebeba gazeti la Nipashe ambapo walimu wenzie na Doroth [mwanamke aliyekuwa na marehemu Barlow] wanadai Doroth ni 'mjane'. Sijui hata niamini kipi.
 
haya bana hebu tuelezeni vyema maana hili jeshi letu ndo la kulinda mai zetu na usalama wetu, sasa hawa makamanda wake mbona hivyo?
Halafu hii taarifa ya Jeshi kukinzana na hali halisi ikoje?
au ndio Intelijensia hiyo?
 
dah ngoja tuone mwisho, kwani imekuwa kawaida kwa viongozi kuacha wake zao hivyo wawe huru.
 
Tatizo linalotukabili sasa ni kuzibwa macho na siasa za ushabiki........kukiwa na tatizo basi tunachagua majibu halafu tunaanza kujenga sababu zetu kufikia majibu yetu....
 
malipo ya uzinzi hayo kama ni kweli alikuwa na mke wa mtu

Kama hadithi hii ina ukweli,hata mimi nathubutu kusema sijapata kuona hukumu sahihi kwa 'washarati' kama hii! AIBU!!!!!!
 
Kuna thread humu umebeba gazeti la Nipashe ambapo walimu wenzie na Doroth [mwanamke aliyekuwa na marehemu Barlow] wanadai Doroth ni 'mjane'. Sijui hata niamini kipi.

Hujakosea. Na alipofiwa aliachwa na mt6oto mmoja, lakini sasa ana watoto wawili zaidi! Je kama hawakuwa wa Kamanda mama huyu alizaa na nani?
 
Usinambie kuwa alizaa na 'kamanda'!

Sio kuzaa na kamanda Barlow bali alizaa na kibopa mmoja wa kihaya aishiye Dar, na huenda ni huyo waliyemtia nguvuni na kumpeleka Mwanza, hiyo thread ipo humuhumu
 
Sio kuzaa na kamanda Barlow bali alizaa na kibopa mmoja wa kihaya aishiye Dar, na huenda ni huyo waliyemtia nguvuni na kumpeleka Mwanza, hiyo thread ipo humuhumu
Hii ndo JF, ungeniunganishia huo uzi ningefurahi saana
 
Hiyo sarakasi. Siamini kama kweli alikuwa anatoka kwenye kikao cha harusi. Lini polisi jamii wakabeba bunduki bila polisi? Au jamaa alikuwa amezoea kupigia polini?
 
Usinambie kuwa alizaa na 'kamanda'!

Ninachotaka kusema ni kwamba kama kamanda hakumzalisha huyu mama basi kuna aliyemzalisha! Kama huyo aliyemzalisha huwezi kumwita mume basi wajuvi wa lugha ya kiswahili telemkeni jamvini mtoe somo, mtu 'sampuli' hii anaitwaje?
 
Mtu ninayezaa naye pasipo kuoana namwita 'mzazi mwenzangu' na kamwe si 'mke wangu'. Labda huwa naikosea maana ya 'mume na mke'.
 
Kweli alifariki kwa presha na si ngoma kama wengine wanavyodai,

Ujane haumzuii mtu mwenye siha njema kubebwa na mwanaume mwingine na kumthamini kama mke wake. Ni kweli mume wa huyo mamaa alishadead lakini tangu mwaka huo sioni ajabu mama yule kuwa alishapata replacement. Hivyo mwamaume alokuwa akimtumia kukidhi haja zake za kimwili mda mrefu ndo anaaminika kama mume wake.
 
Back
Top Bottom