Zimesambaa picha za Darasa chakavu lililojengwa kwa udongo katika mitandao mbalimbali. Baadhi ya wanaharakati wakidai kuwa darasa hilo ni la Shule ya msingi Litingi, kijiji cha Litingi, kata ya Nyangao, jimbo la Mtama.
Ukweli upoje?
Picha iliyosambaa mitandaoni ikidai kuwa ni darasa la Shule ya msingi Litingi, kijiji cha Litingi, kata ya Nyangao, jimbo la Mtama
Ukweli upoje?
Picha iliyosambaa mitandaoni ikidai kuwa ni darasa la Shule ya msingi Litingi, kijiji cha Litingi, kata ya Nyangao, jimbo la Mtama
- Tunachokijua
- Aprili 26, 2022, Mtumiaji mmoja wa Mtandao wa Twitter (Sasa X) anayefahamika kwa jina la Martin Maranja Masese aliweka chapisho la picha inayodaiwa kuwa ni muonekano wa shule ya Msingi Litingi, jimbo la Mtama.
Picha hiyo iliambatana na ujumbe huu;
"Shule ya msingi Litingi, kijiji cha Litingi, kata ya Nyangao, jimbo la Mtama, mbunge wake ni Nape Nnauye (CCM) na alirithi mikoba ya Benard Membe. Nape Nnauye sasa ni waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Membe alikuwa waziri wa mambo ya nje"
Ufuatiliaji wa JamiiForums umebaini kuwa picha hiyo ni halisi lakini sio ya sasa kwa kuwa mamlaka husika zilishakuchukua hatua madhubuti za kurekebisha mazingira husika kwa Kujenga madarasa mengine Mapya Manne, matundu ya Choo, Ofisi za walimu na Matanki ya kuvunia maji katika shule inayotajwa tangu mwaka 2017.
Muonekano wa Shule hiyo kwa sasa ni kama inavyoonekana kwenye picha hizi hapo chini.
Picha hizo zinazosambaa wakati huu ni za zamani yaani mwaka 2015. Darasa hilo chakavu lilibomolewa tangu mwaka 2017.