Salaam wadau.
Naomba kujuzwa na yeyote kuhusiana na hizi Chipset za MediaTek, haswa ubora wake na kwa nini bidhaa zilizo na Chipset hii zinadharaulika, je ni kweli MediaTek ni hovyo au ni maoni tu ya mkumbo? Mfano simu za Tecno,Itel na Infinix ni mbovu na kiwango chake ni cha chini sababu ya MediaTek au kuna sababu nyingine?
Mtaalam
Chief-Mkwawa tunaomba mchango wako tafadhali.
Mediatek ni Soc ina Include vitu vingi sana ikiwemo Cpu, Gpu na mambo mengine kama Isp za camera, Wifi, Bluetooth, Controller za Memory etc
1. Cpu
Siku hizi hakuna anaetengeneza Custom Cpu Android, Wote wanatumia designs za Arm, arm core zake za Cpu zinaweza gawanywa makundi 3.
-Big Core
Hizi kuna Core kama X1, X2, X3 etc
-Middle Core
Cortex A715, A710, A78, A77, A76, A75, A73 etc
-Small core
Cortex A510, A55, A53 etc
Hapa Soc inayokupa Core nzuri ndio bora zaidi bila kujali jina,
Mfano Soc za mediatek kama Dimensity 900, 920, 1080, 8100 na 8200 zote zinatumia Cortex A78 ambazo ni za kisasa na zinakaa na Chaji
Lakini pia kuna Soc za Mediatek Helio P22, G35, G36 ambazo zinatumia cortex A53 ama A55 ni vimeo
Na zipo soc za kawaida kama G80, G99, Dimensity 700, Dimensity 810 ambazo ni za kawaida.
So kwenye Cpu inawezekana kabisa Mediatek ikawa bora kuliko snapdragon ama Exynos ikiwa Core ni Nzuri, ila Tatizo la hawa Ndugu zetu kina Tecno hata siku moja hawatumii Soc mpya za Mediatek, wao ni kusomba tu mabaki ya Soc za zamani, simu chache sana zina Soc nzuri toka kwao, hivyo tatizo hapa ni la Tecno na sio Mediatek.
2. Gpu
Snapdragon zinatumia custom Gpu za kwao wenyewe zinaitwa Adreno, Mediatek na Exynos nyingi wanatumia Mali Gpu za Arm, overall Adreni ni Gpu nzuri zaidi ni ipo adviced kama Gpu zina nguvu sawa Kuchukua ya Adreno sababu in real life itakua na nguvu zaidi.
3. Mambo mengine ya Soc kama Isp na Modems pia Snapdragon wapo vizuri zaidi, ila sio given inabidi uwe makini kuangalia bands, Aina ya camera iliotumika, version ya wifi na Bluetooth etc.
So mkuu Ku conclude Zipo Mediatek nzuri, sio Zote ni mbaya, na zipo pia Snapdragon mbaya, cha muhimu angalia specs husika.
Tecno na Infinix wanauza simu India pia, Tecno Pova 5G na Spark 11 5G india zinauzwa chini ya laki 5, na Zina Dimensity 900 soc nzuri ya 5G inayokaa na chaji na decent perfomance. Kwa Uelewa wangu mimi hizi simu hazipo Africa huku unaletewa spark 8 simu yenye soc ya zamani helio p22 inaweza kwenda shule kabisa.