Ukweli kuhusu Mradi wa NSSF wa Dege Beach Kigamboni

Ukweli kuhusu Mradi wa NSSF wa Dege Beach Kigamboni

Samvulachole

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2006
Posts
413
Reaction score
118
Land for Equity (Ardhi Kwa Hisa) na Mradi wa NSSF Dege Beach Kigamboni


Jana Magazeti mengi yameandika kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Hasa Mradi wa Dege Beach Huko Kigamboni ambapo imeelezwa na magazeti yetu ambayo yana editors na waandishi wasomi kwa kuandika na kutoa

Tuhuma kuwa:



1. Katika Kila Kiwanja Kimoja kati ya Viwanja 300 vilivyoko Katika hatua ya kwanza ya Mradi thamani ya Kiwanja imezidishwa Kwa zaidi ya Shilingi Milioni 775.


2. Thamani ya Kila Kiwanja Ni Shilingi Milioni 25 Tofauti na Milioni 800 ambazo NSSF imenunua Kwa Kila Kiwanja Kimoja Kwa Mujibu wa Mkataba kati yake Na Kampuni ya Azimio.


Taarifa Hizi ni za Uongo.


Ukweli ni:

1. NSSF haikununua Ardhi eneo la Dege Beach, Kigamboni Kwa thamani ya Milioni 800 Kwa Kiwanja.

2. NSSF imepewa Ardhi Bure Ili iwekeze Kwa kuingia Ushirika wa Mradi Katika Ardhi ya Mtu Binafsi (Kampuni ya Azimio).


UFAFANUZI KUHUSU LAND FOR EQUITY au ARDHI KWA HISA:

Aina hiyo ya Ushirika hujulikana Kwa wataalam wa Sekta ya Majengo (Real Estate) Kama Utaratibu wa "Land for Equity" (Yaani Ardhi Kwa Hisa).

Ambapo Katika Makubaliano ya Mradi, Mbia Mmoja wa Mradi anatoa Ardhi Na Mbia mwengine anatoa Fedha za Uwekezaji.

Na kisha Hisa za Mradi hugawanywa kulingana Na mtaji wa Kila Mmoja (Ardhi Kwa Mbia wa kwanza, Na Fedha Kwa Mbia mwengine).

Na hili si Jambo jipya nchini.

Uchunguzi unathibitisha kuwa kilichofanywa na NSSF (Katika Mradi wa Dege Beach Kigamboni) ndicho kinachofanywa na taasisi mbalimbali nchini (wakiwemo NSSF wenyewe), katika Miradi mbalimbali ya Uwekezaji wa Ushirikiano kati sekta ya Majengo.


Baadhi ya mifano ya Miradi ya namna hiyo ni kama ifuatavyo:

1. NHC/TPDC MKAPA TOWER JOINT VENTURE

Miaka ya 90 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) liliingia makubaliano na Shirika la Mafuta la Taifa (TPDC) kujenga Jengo la Mafuta House kwenye ardhi inayomilikiwa na NHC katika eneo ambalo sasa pamejengwa Jengo la Banjamin Mkapa Towers.

(a) Katika Ujenzi Huo NHC walipewa asilimia 25 ya thamani ya mradi kwa kutoa ardhi (Land for Equity) ambayo mwaka 1995 ilikuwa ni Shilingi bilioni 19 bilioni.

(b) Kwa mujibu wa mkataba huo thamani ya ardhi ile mwaka huo ilikuwa shs 4.75 bilioni.

(c) Mwaka 1995 thamani ya ardhi katikati ya jiji la Dar es salaam ilikuwa ni shilingi 62,500 kwa kila mita ya mraba.

(d) Kiwanja kile kina mita za mraba 6,221 sawa na ekari moja na nusu.

(e) Kwa kutumia mahesabu ya kawaida thamani ya ardhi ya NHC ingekuwa shilingi 388 milioni na si hiyo 4.75 Bilioni ambayo inaonyesha bei kukuzwa Kwa nyongeza ya shilingi 4.35 bilioni.



2. NSSF MKURANGA POWER PROJECT


NSSF ni mfaidika wa Utaratibu wa "Land for Equity" Katika mradi Mpya wa Umeme Mkuranga.


(a) Mwaka 2014
NSSF ilinunua ardhi kwa thamani ya shilingi 100 milioni, ardhi hiyo ilikuwa Ni jumla ya ekari 100.

(b) Mwaka 2015 Wawekezaji waliingia ubia na Shirika la NSSF Ili kujenga Mtambo wa Umeme Katika ardhi Husika.

(c) Mchango wa NSSF Katika Mradi Huo ulikuwa ni ardhi yake ya Ekari 100 ambayo iliinunua Kwa Shilingi Milioni 100 Tu Mwaka Mmoja nyuma.

(d) Lakini Katika Mkataba wa Mradi Huo NSSF imepata asilimia 10 ya thamani ya Mradi Mzima wa Uwekezaji ambayo ni Dola za Kimarekani 450 Milioni Sawa na zaidi ya Shilingi 900 Bilioni.

(e) Katika Mradi huu wa Mkuranga NSSF ndani ya mwaka mmoja iliweza kupandisha thamani ya ardhi ile kutoka shilingi 100 milioni mpaka shilingi 90 Bilioni ambayo ni Asilimia 10 ya thamani ya Mradi Wote.

(f) Kama zingetumika Hesabu Za kawaida Tu thamani ya Uwekezaji wa NSSF kwenye Mradi Husika ilipaswa Kuwa Asilia 0.06 Tu Na Sio Asilimia 10 walizopewa.


3. PPF/NHC JOINT VENTURE MWANZA

Mradi mwengine uliofuata Utaratibu wa "Land for Equity" (Ardhi Kwa Hisa) ni Taarifa Juu ya makubaliano kati ya NHC na PPF Katika Ujenzi wa Jengo la PPF Tower Mwanza:

(a) NHC walitoa ardhi na kupewa Aslimia 25 ya hisa za mradi husika.

(b) Mradi huo una thamani ya Shilingi bilioni 258, Lakini Ukubwa wa ardhi waliyotoa NHC ni Kiwanja cha ekari moja tu.

- Kamwe huwezi kusikia ikisemwa kuwa PPF wamenunua Kiwanja Cha Ekari Moja Kwa thamani ya Shilingi Bilioni 64 Kwa Kuwa Ni Ushirika wa Pamoja.


3. NSSF RITA PROJECT

NSSF imejenga jengo RITA, eneo la Posta jirani Kabisa na Jengo la Klabu ya Billicanas Jijini Dar es salaam.

Katika Mradi Huo RITA iliyojengewa Jengo Husika, Na Kwa Kutoa ardhi hiyo wamepata hisa Asilimia 25 ya thamani ya mradi mzima wa Jengo Hilo, ambayo ni shilingi Bilioni 198.


Lakini Ukubwa wa Kiwanja cha RITA ni nusu ekari tu. Kamwe huwezi kusikia NSSF wamenunua nusu ekari kwa Shilingi bilioni 49 Katika Mradi wa Jengo la RITA.


4. LIST YA MIRADI MINGINE ILIYOFUATA UTARATIBU WA "LAND FOR EQUITY"



1. Mradi kati ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Fida-Hussein Katika Jengo lililoko Maeneo ya Jirani Na Hospitali ya Ocean Road.

2. Mradi wa Jengo la UVCCM eneo la Fire Jijini Dar es salaam.

3. Mradi wa Jengo la Mwalimu Nyerere Foundation eneo la Posta.

4. Mradi wa Jengo la UWT (Makao makuu ya Airtel) eneo la Morocco nk.



5. HITIMISHO




(a) NSSF iliingia ubia na kampuni ya Azimio Kwa ajili ya Uendelezwaji wa Ardhi Katika Mradi wa Dege Beach Kule Kigamboni.


(b) Kampuni ya Azimio Kwa Kutoa Ardhi ya Mradi Husika ilipewa asilimia 20 ya thamani ya mradi wa Dege Eco Village.


(c) Lakini Pia kwenye Mkataba wa Mradi Azimio wanapaswa Kutoa 35% ya Fedha za thamani ya Mradi.


(d) Hivyo kuwafanya wawe na 55% ya Mradi Husika Huku NSSF wakiwa na 45 ya Mradi Kwa Fedha watakazotoa.


(e) La kushangaza this time wameenda kwenye kamati ya bunge juzi na Mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) presented his report na amesema amewapa NSSF CLEAN REPORT and EVERYTHING IS OK (ripoti ya CAG inapatikana kwenye website yao hapa: National Audit Office of Tanzania » CAG reports )

(f) New management ya NSSF chini ya Mkurugenzi mkuu ndugu KYAHARAHARA wanasema HAPANA THINGS ARE NOT OK (bila kutoa ufafanuzi how) na kila akiulizwa kivipi majibu yake ni kuwa PAST management imeharibu mambo

(g) Kamati ya BUNGE ikaamua kuwa the report is ADOPTED na Mradi wa Dege uendelee. Management Ikae na the JV partner waangalie modalities za kuendelea na mradi.



Out of desperation Huyu Mkurugenzi mpya wa NSSF (KYAHARARA) fed the reporters with all lies (Tariff za uwongo). Na mbaya zaidi hakuna gazeti hata moja ambalo lilifanya investigative journalism na kuuliza basic questions kama vile:




1. Kama kuna ufisadi wa mabilioni kwenye mradi wa DEGE ECO VILLAGE why did CAG give clean report?


2. Kama kilichofanyika Dege ni ufisadi then why PPF NHC TBA TPDC etc are not taken to task? Why NSSF?


I'm sure wenye vichwa vilivyotulia Hapa Jamiiforums wataweza kulitazama hili kuala kwa jicho la tatu (3 dimension)


Hii inanifanya niamini kuwa huko NSSF kuna CIVIL WAR au VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE.

Theory yangu ni kuwa chini ya Mkurugenzi mpya, Management ilisimamishwa kazi na wale wanaokaimu wanawafanyia fitna wakiosimamishwa ili wafukuzwe then wao wawe confirmed.

Hiyo ndio vita inayoendelea kwa sasa na mbaya zaidi huyu mkurugenzi mpya naye amejiingiza kwenye hiii michezo michafu na kutoa taarifa za uwongo kwa vyombo vya habari.

Pia tusisahau kuwa huyu Mkurugenzi mpya aliwahi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa Mradi wa Daraja la Kigamboni ni mradi wa anasa na hauna tija kwa shirika.

Lakini wiki tatu zilizopita huyu huyu Mkurugenzi anawaambia waandishi wa habari kuwa Mradi wa Daraja la kigamboni ni mzuri sana kwa taifa na unaingizia Shirika Mabilioni

Nasubiri kwa ham kusoma Jinsi Paskal Mayala atakavyokuja kumjibia na kumtetea huyu Mkurugezi mpya.

Nawasilisha.

JAMIIFORUMS, WHERE WE DARE TALK OPENLY
 
na shangaa hadi mubunge wa kigamboni anasema kila kitu kipo sawa ukiona jambo linazungumziwa sana lazima ujue kuna kitu hakipo sawa ww umeelezea vizuri natumaini watu watakuelewa
 
Utetezi wako ni mzuri sana Ikiwa tu valuation/appraisal ilifanywa kwa kuzingatia share contribution ya parties. Ila ikiwa kilichofanyika ni appraisal for NSSF assets for accounting purpose where market value is the basis, then utetezi wako unakuwa null and void.
 
Hizo projects ulizotaja UVCCM, Rita, PPF, Benjamin tower ukiangalia utaona kuwa maeneo hayo yapo strategic na kutokana na location yake mwekezaji anakuwa hana option zaidi ya kukubaliana na mwenye ardhi. Unaweza ukaona kwa sasa Kariakoo wachaga na wakinga wanachukua ardhi na kujenga magorofa kisha jengo linakuwa jointly owned.

Pia taasisi za umma zikiingia mikataba zenyewe kwa zenyewe hata kama mmoja anagain zaidi hamna tatizo cuz zote ni public money na ni sawa na kuhamishia fedha zako toka mfuko huu na kupeleka kwenye mfuko mwingine.

Najiuliza bado kwanini NSSF hawakununua ardhi Kigamboni kisha waiendeleze wenyewe wakati maeneo kigamboni yapo wazi mengi tu? Kwanini waingie ubia na kampuni binafsi tena yeye ndio awe main shareholder? Mpaka hapo project ilipofikia, Azimio wameshatoa cash kiasi gani?
Hiyo Azimio ni ya nani? Who are the shareholders?
 
Wataumbuka tu mwaka huu. hapo umepangua wakajipange wtuletee mashudu mengine. Mwacheni DAU apumzike. hawa watu wanajistukia sana ofisi umepewa unaweweseka nini?
 
Wataumbuka tu mwaka huu. hapo umepangua wakajipange wtuletee mashudu mengine. Mwacheni DAU apumzike. hawa watu wanajistukia sana ofisi umepewa unaweweseka nini?
Hana ubunufu unategemea atatea vipi kibarua chake zaidi ya majungu na kutafta mchawi unafkiri alivojua anakabdhiwa nssf alijua anatoa lecture udsm
 
nasikia dk alikuwa bingwa wa kupiga madufu enzi za ujana wake na bado hajaacha
 
Land for Equity (Ardhi Kwa Hisa) na Mradi wa NSSF Dege Beach

Out of desperation Huyu Mkurugenzi mpya wa NSSF fed the reporters with all lies (Tariff za uwongo). Na mbaya zaidi hakuna gazeti hata moja ambalo lilifanya investigative journalism na kuuliza basic questions.

Nasubiri kwa hamu kusoma Jinsi Paskal Mayala atakavyokuja kumjibia na kumtetea huyu Mkurugezi mpya
Mkuu Samvu, kwanza asante kwa hii, kwa vile mimi sio insider wa NSSF, then utasubiri sana!.

Sifa Kuu ya JF ni kwa watu kusema ukweli daima no matter what, ombi langu kwako, kwa vile umekuja humu na facts, lets keep more facts to an open tukianzia na hii hoja ya kuna mtu yuko very desperate, ndipo tuje kwenye justification ya NSSF kufanya land acquisition kwa ubia katika eneo ambalo sio too demanding. Hiyo mifano mingine yote ni maeneo ya mjini kati, very prime na very demanding. Huko tutafika, tuanze na hii ya desperation.

Kwa vile kwenye hitimisho lako umesema nakuku quote
"Out of desperation Huyu Mkurugenzi mpya wa NSSF fed the reporters with all lies (Tariff za uwongo)", ili bandiko lako hili lisiwe ni kampeni maalum ya trying ya "saving the faces", utakuwa umelitendea haki jukwaa hili kama utaeleza huyo Mkurugenzi wa NSSF who fed the reporters with all lies out of desperation, yuko desperate for what? .

Tuanzie hapo.

Paskali
 
Land for Equity (Ardhi Kwa Hisa) na Mradi wa NSSF Dege Beach Kigamboni

Jana Magazeti mengi yameandika kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye miradi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF), Hasa Mradi wa Dege Beach Huko Kigamboni ambapo imeelezwa Kuwa Katika Kila Kiwanja Kimoja kati ya Viwanja 300 vilivyoko Katika hatua ya kwanza ya Mradi thamani ya Kiwanja imezidishwa Kwa zaidi ya Shilingi Milioni 775. Ikielezwa Kuwa thamani ya Kila Kiwanja Ni Shilingi Milioni 25 Tofauti na Milioni 800 ambazo NSSF imenunua Kwa Kila Kiwanja Kimoja Kwa Mujibu wa Mkataba kati yake Na Kampuni ya Azimio.

Taarifa Hizi ni za Uongo. Ukweli ni Kuwa NSSF haikununua Ardhi eneo la Dege Beach, Kigamboni Kwa thamani ya Milioni 800 Kwa Kiwanja, imepewa Ardhi Bure Ili iwekeze Kwa kuingia Ushirika wa Mradi Katika Ardhi ya Mtu Binafsi (Kampuni ya Azimio).

Aina hiyo ya Ushirika hujulikana Kwa wataalam wa Sekta ya Majengo (Real Estate) Kama Utaratibu wa "Land for Equity" (Yaani Ardhi Kwa Hisa). Ambapo Katika Makubaliano ya Mradi, Mbia Mmoja wa Mradi anatoa Ardhi Na Mbia mwengine anatoa Fedha za Uwekezaji. Na kisha Hisa za Mradi hugawanywa kulingana Na mtaji wa Kila Mmoja (Ardhi Kwa Mbia wa kwanza, Na Fedha Kwa Mbia mwengine).

Na hili si Jambo jipya nchini. Uchunguzi unathibitisha kuwa kilichofanywa na NSSF (Katika Mradi wa Dege Beach Kigamboni) ndicho kinachofanywa na taasisi mbalimbali nchini (wakiwemo NSSF wenyewe), katika Miradi mbalimbali ya Uwekezaji wa Ushirikiano kati sekta ya Majengo.

Baadhi ya mifano ya Miradi ya namna hiyo ni kama ifuatavyo:

Miaka ya 90 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) liliingia makubaliano na Shirika la Mafuta la Taifa (TPDC) kujenga Jengo la Mafuta House kwenye ardhi inayomilikiwa na NHC katika eneo ambalo sasa pamejengwa Jengo la Banjamin Mkapa Towers. Katika Ujenzi Huo NHC walipewa asilimia 25 ya thamani ya mradi kwa kutoa ardhi (Land for Equity) ambayo mwaka 1995 ilikuwa ni Shilingi bilioni 19 bilioni. Kwa mujibu wa mkataba huo thamani ya ardhi ile mwaka huo ilikuwa shs 4.75 bilioni.

Mwaka 1995 thamani ya ardhi katikati ya jiji la Dar es salaam ilikuwa ni shilingi 62,500 kwa kila mita ya mraba na kiwanja kile kina mita za mraba 6,221 sawa na ekari moja na nusu. Kwa kutumia mahesabu ya kawaida thamani ya ardhi ya NHC ingekuwa shilingi 388 milioni Na si hiyo 4.75 Bilioni ambayo inaonyesha bei kukuzwa Kwa nyongeza ya shilingi 4.35 bilioni.

• NSSF ni mfaidika wa Utaratibu wa "Land for Equity" Katika mradi Mpya wa Umeme Mkuranga. Mwaka 2014 NSSF ilinunua ardhi kwa thamani ya shilingi 100 milioni, ardhi hiyo ilikuwa Ni jumla ya ekari 100.

Mwaka 2015 Wawekezaji waliingia ubia na Shirika la NSSF Ili kujenga Mtambo wa Umeme Katika ardhi Husika. Mchango wa NSSF Katika Mradi Huo ulikuwa ni ardhi yake ya Ekari 100 ambayo iliinunua Kwa Shilingi Milioni 100 Tu Mwaka Mmoja nyuma. Lakini Katika Mkataba wa Mradi Huo NSSF imepata asilimia 10 ya thamani ya Mradi Mzima wa Uwekezaji ambayo ni Dola za Kimarekani 450 Milioni Sawa na zaidi ya Shilingi 900 Bilioni.

Katika Mradi huu wa Mkuranga NSSF ndani ya mwaka mmoja iliweza kupandisha thamani ya ardhi ile kutoka shilingi 100 milioni mpaka shilingi 90 Bilioni ambayo ni Asilimia 10 ya thamani ya Mradi Wote. Kama zingetumika Hesabu Za kawaida Tu thamani ya Uwekezaji wa NSSF kwenye Mradi Husika ilipaswa Kuwa Asilia 0.06 Tu Na Sio Asilimia 10 walizopewa.

• Mradi mwengine uliofuata Utaratibu wa "Land for Equity" (Ardhi Kwa Hisa) ni Taarifa Juu ya makubaliano kati ya NHC na PPF Katika Ujenzi wa Jengo la PPF Tower Mwanza, ambapo NHC walitoa ardhi na kupewa Aslimia 25 ya hisa za mradi husika. Mradi huo una thamani ya Shilingi bilioni 258, Lakini Ukubwa wa ardhi waliyotoa NHC ni Kiwanja cha ekari moja tu.

Kamwe huwezi kusikia ikisemwa kuwa PPF wamenunua Kiwanja Cha Ekari Moja Kwa thamani ya Shilingi Bilioni 64 Kwa Kuwa Ni Ushirika wa Pamoja.

NSSF imejenga jengo RITA, eneo la Posta jirani Kabisa na Jengo la Klabu ya Billicanas Jijini Dar es salaam. Katika Mradi Huo RITA iliyojengewa Jengo Husika, Na Kwa Kutoa ardhi hiyo wamepata hisa Asilimia 25 ya thamani ya mradi mzima wa Jengo Hilo, ambayo ni hilingi Bilioni 198.

Lakini Ukubwa wa Kiwanja cha RITA ni nusu ekari tu. Kamwe huwezi kusikia NSSF wamenunua nusu ekari kwa Shilingi bilioni 49 Katika Mradi wa Jengo la RITA.

• Miradi mengine iliyofuata Utaratibu huu wa "Land for Equity"
* Mradi kati ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Fida-Hussein Katika Jengo lililoko Maeneo ya Jirani Na Hospitali ya Ocean Road.
* Mradi wa Jengo la UVCCM eneo la Fire Jijini Dar es salaam.
* Mradi wa Jengo la Mwalimu Nyerere Foundation eneo la Posta.
* Mradi wa Jengo la UWT (Makao makuu ya Airtel) eneo la Morocco nk.

• Hitimisho:

NSSF iliingia ubia na kampuni ya Azimio Kwaajili ya Uendelezwaji wa Ardhi Katika Mradi wa Dege Beach Kule Kigamboni. Kampuni ya Azimio Kwa Kutoa Ardhi ya Mradi Husika ilipewa asilimia 20 ya thamani ya mradi wa Dege Eco Village.

Lakini Pia kwenye Mkataba wa Mradi Azimio wanapaswa Kutoa 35% ya Fedha za thamani ya Mradi, Hivyo kuwafanya wawe na 55% ya Mradi Husika Huku NSSF wakiwa na 45 ya Mradi Kwa Fedha watakazotoa.

La kushangaza this time wameenda kwenye kamati ya bunge juzi . CAG presented his report na amesema amewapa NSSF clean report and everything is ok.

NSSF wenyewe wanasema hapaana things are not ok. Past management imeharibu mambo.

Kamati ikaamua kuwa the report is ADOPTED na Mradi wa Dege uendelee. Management Ikae na the JV partner waangalie modalities za kuendelea na mradi.

Out of desperation Huyu Mkurugenzi mpya wa NSSF fed the reporters with all lies (Tariff za uwongo). Na maya zaidi hakuna gazeti hata moja ambalo lilifanya investigative journalism na kuuliza basic questions kama vile:


1. Kama kuna ufisadi wa mabilioni why did CAG give clean report?

2. Kama kilichofanyika Dege ni ufisadi then why PPF NHC TBA TPDC etc are not taken to task? Why NSSF?

I'm sure wenye vichwa vilivyotulia Hapa Jamiiforums wataweza kulitazama hili kuala kwa jicho la tatu

Hii inanifanya niacin kuwa huko NSSF kuna CIVIL WAR au VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE. Theory yangu ni kuwa wale wanaokaimu wanawafanyia fitna wakiosimamishwa ili wafukuzwe then wao wawe confirmed. Hiyo ndio vita inayoendelea kwa sasa na maya zaidi huyu mkurugenzi mpya naye amejiingiza kwenye hiii michezo michafu na kutoa taarifa za uwongo kwa vyombo vya habari

Pia tussah kuwa huyu Mkurugenzi mpya aliwahi kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa Mradi wa Daraja la Kigamboni ni mradi wa anasa na haunt tija kwa shirika. Lakini wiki tatu zilizopita huyu huyu Mkurugenzi anawaambia waandishi wa habari kuwa Mradi wa Daraja la kigamboni ni mzuri sana kwa taifa na unaingizia Shirika Mabilioni

Nasubiri kwa ham kusoma Jinsi Paskal Mayala atakavyokuja kumjibia na kumtetea huyu Mkurugezi mpya

Tunajua wewe ni mmojawapo wa wanufaika sasa majibu yako huku hata kusaidia nenda mbele ya kamati waeleze hayo,
 
Hizo projects ulizotaja UVCCM, Rita, PPF, Benjamin tower ukiangalia utaona kuwa maeneo hayo yapo strategic na kutokana na location yake mwekezaji anakuwa hana option zaidi ya kukubaliana na mwenye ardhi. Unaweza ukaona kwa sasa Kariakoo wachaga na wakinga wanachukua ardhi na kujenga magorofa kisha jengo linakuwa jointly owned.

Pia taasisi za umma zikiingia mikataba zenyewe kwa zenyewe hata kama mmoja anagain zaidi hamna tatizo cuz zote ni public money na ni sawa na kuhamishia fedha zako toka mfuko huu na kupeleka kwenye mfuko mwingine.

Najiuliza bado kwanini NSSF hawakununua ardhi Kigamboni kisha waiendeleze wenyewe wakati maeneo kigamboni yapo wazi mengi tu? Kwanini waingie ubia na kampuni binafsi tena yeye ndio awe main shareholder? Mpaka hapo project ilipofikia, Azimio wameshatoa cash kiasi gani?
Hiyo Azimio ni ya nani? Who are the shareholders?
Mkuu muanzisha hoja anajamba tu maanake ktk ripoti ya CAG walihoji kwanini wasitumie ardhi yao kujenga ambayo wanayo hukohuko kigamboni,ile ni njia ya kuiba waloitumia na kampuni yenyewe ni ya dau
 
Huu ni utetezi wa kijinga na umetokana na uandishi mbovu ambao wameripoti kana kwamba hiyo ardhi imenunuliwa na NSSF moja kwa moja badala ya kuripoti ardhi imetolewa na Azimio kama sehemu ya hisa ila kwa bei ya uongo.

Samvulachole wewe umetumwa, unajaribu kufanya spinning za kitoto, kwa awamu hii jua ni suala la muda tu wahusika watapewa get together pale Kisutu kabla ya kuhamishiwa mahakama ya mafisadi.

Mwisho, tusaidie wamilika au wadau wa Azimio ni kina nani, kwa nini walikuwa wanapata tenda nyingi za NSSF?
 
Nakuuliza mleta thread. Market value ya hiyo ardhi iliyoripotiwa kwenye books of accounts za NSSF ni ngapi? Pia kasome what is market value, share value, investment value, na potential value and. How they are used. Usidandie tu Real Estate bila kujua ina maaanisha nini.
 
Huu ni utetezi wa kijinga na umetokana na uandishi mbovu ambao wameripoti kana kwamba hiyo ardhi imenunuliwa na NSSF moja kwa moja badala ya kuripoti ardhi imetolewa na Azimio kama sehemu ya hisa ila kwa bei ya uongo.

Samvulachole wewe umetumwa, unajaribu kufanya spinning za kitoto, kwa awamu hii jua ni suala la muda tu wahusika watapewa get together pale Kisutu kabla ya kuhamishiwa mahakama ya mafisadi.

Mwisho, tusaidie wamilika au wadau wa Azimio ni kina nani, kwa nini walikuwa wanapata tenda nyingi za NSSF?

Huyu mtetezi ni mmoja wa waosha miguu ya ex DG na lazma atakuwa kati ya watu watatu waliondolewa ktk kile kitengo cha ufujaji pesa Nssf ie kitengo cha uwekezaji na miradi.
Jf syo sehemu sahihi kutetea hili swala Bali ni kujitokeza hadharani mbele ya PAC na kudadavua unachojua ili umuokoe huyo bwana wako,au toa nalala gazetini ukifafanua jinsi ardhi inavyoweza kuwa land equity na hapo tutakutambua kama mchumi mbobezi na ufungue ofisi ya consultation am sure utapata wateja wengi,kama huwezi funga domo lako wacha vyombo husika vifanye kazi,kumbuka pia DG MPYA ni mchumi tofauti na dau alikuwa marketer
 
CAG aliposema NSSF IS CLEAN alimaanisha nini na kama CAG report hiwezi kuaminika tena tumuamini nani tena , wakati bajeti yake ukaguzi ilikuwa 79b mwaka jana ikashuka hadi 40 mwaka huu sio haba hizo ni pesa nyingi sana kwa watanzania
 
Back
Top Bottom