Unajua Kitabu cha ufunuo kiliandikwa mwaka gani!? Na kwa nini kiliingizwa kwenye biblia!?
swali la kipuuzi, kitabu cha ufunuo kinatabiri hadi mwisho wa dunia, hadi muda huu
nakuletea mfano
Katika kitabu cha Ufunuo, Mungu anatufunuliwa wahusika au mawakala watano
ambao ni:
1—Mnyama mwekundu wa Ufunuo 12—Shetani mwenyewe
2—Mnyama mfano wa chui wa Ufunuo 13—Rumi ya kidini
3—Mnyama mfano wa mwana kondoo wa Ufunuo 13:11—Taifa la Marekani
4—Sanamu ya Mnyama Ufunuo 13—Umoja wa makanisa —WCC
5—Mnyama wa rangi nyekundu sana na mwanamke wa Ufunuo 17—-Illuminati,
freemason wakiwa wameungana na kanisa la Rumi..
Wengi hawakuwa wanatofautisha wanyama hao lakini utakapojifunza kwa undani
zaidi utagundua kwamba mnyama wa Ufunuo 17 ambaye ni mwekundu sana mwenye
pembe kumi na vichwa saba ambaye amembeba mwanamke inamaanisha muungano wa
Illuminati wakiwa wameunda majimbo kumi katika dunia nzima pamoja na kanisa la
Rumi likiwa na watawala saba tangu kuanza kazi yake baada ya kupata jeraha la mauti.
Biblia inapotumia neno mwanamke kiunabii humaanisha kanisa (Ufunuo 21:2) na neno
‘kichwa’ humaanisha kiongozi wa kanisa ambapo kwa kanisa la Mungu, kichwa ni Kristo
lakini kwa kanisa la uongo, kichwa ni mwanadamu aliyechukua nafasi ya Yesu duniani,
(Wakolosai 1:18; 2Wathesalonike 2:4). Biblia kamwe haijawahi kutumia neno ‘kichwa’
kumaanisha kiongozi wa kiserikali ila hutumia neno ‘watawala au wafalme’. Ndio maana
vichwa saba inamaanisha vipindi saba vya viongozi saba wa kanisa.
Ufunuo 17:8
anasema kwamba mnyama huyo yuko tayari kupanda kutoka kuzimu na
katika Ufunuo 9:11 tunasoma kwamba “Na juu yao wanaye mfalme, naye ni malaika wa
kuzimu…”. Mafungu yote hayo yanamaanisha umizimu (spiritualism) ambayo ni imani
ya Illuminati. Imani hii inamfanya muumini aamini kwamba hakuna kifo na mtu
anapokufa anakuwa amebadilisha mahali kwa kuhama duniani na kwenda mahali pengine
akiendelea kuishi na kwamba hiyo ndiyo mbingu yake maana hawaamini kama kuna
ufufuo. Chanzo cha fundisho hili ni Shetani alipomfundisha Hawa kwamba “Hakika
hamtakufa” Mwanzo 3:4. Hivyo tutajifunza na kuona ukweli huu wa Illuminati kwa
kujiunga na kanisa ili kutimiza malengo yao.
Je, kuna watu au kitu kinachoitwa Illuminati? Inaweza kuwa katika kizazi chetu hiki?
Baadhi wamekuwa wakidhihaki kuhusu swala zima la Illuminati. Hata hivyo katika
kitabu hiki unaweza kupata ufahamu wa kina kuhusu Illuminati na Freemason ndani ya
jamii tunayoishi. Je, maneno kama Illuminati au Freemason ni mapya kwako? Hilo
linawezekana maana maneno hayo hayafahamiki kwa watu wengi, hata kwa wasomi
wakubwa wa elimu ya duniani. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wahusika wa maneno
hayo wamekuwa wakifanya kazi zao kwa siri kubwa kiasi cha kuwafanya watu
mamilioni wasielewe kinachoendelea na hivyo maneno hayo kuendelea kuwa siri kubwa.
“The great strength of our order lies in its concealment,” yaani “nguvu kubwa ya
utaratibu wetu iko katika kuficha na kufanya kazi zetu kwa siri kubwa” ni maneno ya
Adam Weishaupt, mwanzilishi wa Illuminati mwaka 1776. Akaendelea kusema, “Let it
never appear in any place in its own name, but always covered by another name and
another occupation” yaani “Hebu isionekane mahali popote kwa jina lake, lakini daima
ifanyike kwa jina lingine na kwa namna nyingine.” (Kutoka kwa Robin’s Proofs of a
Conspiracy, p. 195.)
Kazi hizi za Illuminati zimekuwa zikifanyika duniani kote kwa karne nyingi kiasi
kwamba watu wengi hawajui hata kuwepo kwa watu kama hao. Njama hizi za siri
zinaweza kuwa na msingi wake tangu wakati wa Nimrodi, mtu yule muovu aliyeanza
kazi zake za uasi huko Mesopotamia. Wakati kila mwalimu wa dini anajua kuhusu mnara
wa Babeli, ni wachache wanaojua kwamba kanuni za mchakato huo wa zamani wa
kujenga mnara wa Babeli ndizo zinazofanya kazi hadi leo katika nyanja za Siasa na Dini.
Kitabu hiki kiitwacho ‘Illuminati na Freemason katika mnyama wa namba 666’,
kitakupa ukweli wa leo na wa ajabu na ukiondoa Biblia, ni vitabu vichache vinavyoweza
kukupatia habari za uhakika na muhimu kwa ajili ya wokovu wa maisha yako. Sio lengo
la mwandishi wa kitabu hiki kushabikia dini fulani au kuanzisha kanisa na kupata
waumini kama wafanyavyo walio wengi, bali lengo ni kutoa bila woga wala upendeleo
ukweli halisi kama ulivyotolewa na Mungu mwenyewe. Hivyo kama utakutana na habari
zinazopingana na imani yako ni vema basi kutulia na usikasirike maana hasira ya
mwanadamu haitendi haki ya Mungu (Yakobo 1:20), ni vema kumuuliza Mungu kwa
unyenyekevu ili akuhakikishie kama habari hizi zinatoka kwake na uwe tayari kupokea
lolote atakalokujibu. Mungu ni mwaminifu na hakika atakujibu kama utamwendea kwa
nia ya kutaka kufuata ukweli wake. Lengo la mwandishi wa kitabu hiki ni kuwapeleka
wasomaji kwa Mungu mwenyewe na sio kuwapeleka kwa mwandishi. Kabla ya kuanza
kujifunza kwa undani, hebu tuone vyanzo vya habari hizi nzito. Ninatoa shukrani kubwa
kwa ajili ya vitabu hata vile ambavyo hatuvikubali, maana vinatuonyesha mawazo ya
waandishi wengine. Vipo vitabu vingi ambavyo vimetumika katika kuandaa kitabu hiki,
vitabu hivyo baadhi ni pamoja na “The Illuminati 666” cha ndugu Roy Allan Anderson;
“The broken Cross” cha Padre Peirs Compton wa kanisa katoliki; “The Two
Babylonians” cha ndugu Alexander Hislop, “Freemasonry encyclopedia”, “Morals and
Dogma” cha Dr. Albert Pike; “To be God of One World” cha Robert Sessler; “The Keys
of this Blood” cha Padre Malachi Martin wa kanisa katoliki, “The Secrets of The
Illuminati” cha ndugu Mac Marquis aliyewahi kuwa freemason na akajitoa, mtandao wa
Wikipedia na mitandao mingine mingi ikiwa ni pamoja na vyanzo vya kuaminika kutoka
kwa Illuminati na Freemason wenyewe; pamoja na vitabu vingine vingi utakavyoviona
kama rejea ya kila nukuu utakayoisoma. Hata hivyo kitabu ambacho tumekitegemea sana
katika kuandika kitabu hiki, ni kitabu cha vitabu vyote, kitabu ambacho ni zaidi ya vitabu
vyote, kitabu ambacho ni tofauti na vitabu vingine vyote duniani kilichoandikwa na zaidi
ya watu 30 walioishi wakati na mahali tofauti tena kwa tofauti ya maelfu ya miaka, wengi
wao bila kukutana wala kufahamiana huku muasisi akiwa ni Mungu Mwenyewe, kitabu
hicho ni “Biblia Takatifu” ambayo pamoja na kuandikwa na watu zaidi ya 30,
hawakutofautina hata katika neno moja. Wakati tumetumia nukuu kutoka katika vitabu
vingine, lakini bado tumechukulia kwamba neno la Mungu ndani ya Biblia ndilo lenye
nuru na ukweli wa mwisho na hivyo limetumika hata kupima maandishi ya vitabu
vingine. Kwa muda wa miaka zaidi ya kumi na mbili sasa tangu nianze kufanya
uchunguzi kuhusu vyama vya siri, kamwe sijawahi kufundisha bila kupima mafundisho
ya vyama hivi kwa kutumia Biblia. Kila mipango na matukio yanayofanywa na Illuminati
nimekuwa nikiyapima kwa Biblia katika unabii ili niwe na uhakika kama mipango yao
iko sawa na unabii alioutoa Mungu kupitia Biblia.
Tunaweza kusoma katika Ufunuo 17:17 nabii Yohana anasema: “Maana Mungu
ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja na kumpa yule
mnyama ufalme wao, hata maneno ya Mungu yatimie” ikiwa na maana kwamba Mungu
ametia shauri lake mioyoni mwa Illuminati ili wapange mipango yao ya kumpa ufalme
wao mnyama wa namba 666 kusudi maneno ya Mungu—yaani unabii wa Mungu utimie.
Hapa tunaweza kutambua kwamba mipango ya Illuminati inakwenda sawa na unabii wa
Mungu. Kitabu hiki kitakupa habari za uhakika jinsi mipango ya Illuminati ilivyowekwa
kwa ajili ya kumpa utawala wao na nguvu zao mnyama wa namba 666 ili apate kutawala
dunia kama Mungu alivyotufunulia katika unabii wa Biblia. Mipango hiyo ni ya siri
ikiwa ni pamoja na kuweka ratiba ya vita kuu tatu (3) za dunia ambapo tayari vita kuu
mbili za dunia zimeshatekelezwa wakati vita kuu ya tatu ya dunia itatekelezwa muda si
mrefu.
Katika agano la kale na agano jipya ndani ya Biblia ndipo tumeweza kupata mwanga
wa kuelezea siri hizi za Illuminati na Freemason, ambalo ndilo kusudi la kitabu hiki ili
watu wajue ukweli na kisha wawe huru kutoka utumwani mwa shetani. Mtume Paulo
katika barua zake kwa kanisa ameelezea kuhusu “Siri ya Mungu” ambayo katika neno la
Mungu ni “Mungu kufunuliwa katika mwili,” na “Kristo ndani yetu, tumaini la utukufu
wetu” (1Timotheo 3:16; Wakolosai 1:26,27). Katika barua yake ya pili kwa
Wathesalonike anaelezea kuhusu “Siri ya kuasi” ambayo anaiita “Mtu wa dhambi,”
maana yake mnyama wa namba 666, anayejifanya kuwa ni Mungu akitaka aabudiwe
kama Mungu (2Wathesalonike 2:7; 3 na 4). Mtume anasema kwamba siri hiyo ilikuwa
inatenda kazi tangu wakati wake lakini akaelezea kwamba siri hiyo itafanya kazi kubwa
zaidi wakati wa mwisho kwa kutumia ishara na maajabu mengi. Hivyo tunakuta aina
mbili za siri, yaani “Siri ya Mungu” na Siri ya kuasi”. Siri ya kuasi inatokana na uasi wa
Shetani na kisha kuendelea kufanya kazi zake kwa siri kubwa ili kuwafanya watu
wasielewe kinachoendelea katika ulimwengu wa siasa, uchumi, elimu na dini na hivyo
watu wengi wanakuwa watumwa wa freemason bila wao kujua kama ni watumwa.
Kwa nini nimehusisha mnyama wa namba 666, Illuminati, freemason na maswala ya
ibada na imani? Ukweli ni kwamba unapoongelea Illuminati, Freemason na mnyama wa
namba 666 unaongelea kuhusu mambo ya imani, ibada na utawala kama anavyosema
mmoja wa Illuminati mwenye digrii 33 Bw. Albert Pike, namnukuu: “Every Masonic
Lodge is a temple of religion, and its teachings are instruction in religion” (Albert Pike,
Morals and Dogma, P. 213.) Kwamba “kila Loji (Jumba au kituo) ya Freemason ni
hekalu la mambo ya dini, na mafundisho yake ni maagizo katika dini.” Bw. Albert
anaendelea kusema kwamba: “Freemasonry is a search for Light. That search leads us
directly back, as you see, to the Kabalah.” [Albert Pike, Morals and Dogma, p. 741]
Kwamba “Freemason ni kutafuta nuru. Na kutafuta huko kunatufanya, kama unavyoona,
tujielekeze Kabalah.” Kama Freemason wana kazi ya kutafuta nuru, ambayo kwa kweli
siyo nuru ya kweli, basi watu wanaotafuta wokovu wanapaswa kutafuta nuru ya kweli.
Yesu alisema, “Ninyi ni nuru ya ulimwengu.” Mathayo 5:14 Hivyo tutakuwa
tukichunguza mambo ya imani, ibada na utawala ambavyo ni vitu muhimu zaidi kuliko
kitu kingine katika maisha ya mwanadamu maana ndivyo vitakavyotoa taswira ya hatima
ya kila mmoja wetu, ama ni uzima wa milele au kupotea milele.
Mibaraka ya kujifunza neno la Mungu ni kwamba unapoona dalili fulani zikitokea,
hazikustui wala kukutia hofu. Dalili hizo badala yake zinakufanya usonge mbele katika
kufanya kile ambacho Mungu amekiagiza ili kushiriki na wengine mibaraka hiyo ya
ukweli kadri wengi wanavyoweza kuwa na masikio na kusikia. Lakini pia kushiriki huku
kwa mibaraka na wengine si kwa lengo la kuwafanya wawe na hofu, bali kuwafanya
wajiandae kutokana na kile kitakachoupata ulimwengu kadri tunavyoishi. Kwa kufanya
hivyo mara kwa mara huwafanya wasikilizaji na wasomaji watafute kutembea na Mungu
kwa ukaribu zaidi ili kwamba wawe tayari kwa lolote atakalowaambia kulifanya katika
siku hizi za mwisho. “Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo
yatakayotendeka; wala hakuna jambo jipya chini ya jua.” Mhubiri 1:9.
Kujifunza unabii kunaweza kuwa ni jambo muhimu na zuri ambalo kamwe haliwezi
kushindwa katika kuamsha roho ya kumtafuta Mungu. Kila siku mtu anapojifunza ukweli
wa leo kutoka kwa Mungu, ndipo anapoanza kuona zaidi na zaidi unabii unavyotimia
mbele yake. Wakati watu wengi wanashindwa kuona hatari inayowakabili, msomaji wa
neno la Mungu anapata mbaraka wa kujua maonyo na hivyo kuweza kujiandaa yeye na
nyumba yake kwa ajili ya kurudi kwa Yesu mara ya pili. Na hii ndio sababu kwamba
Yesu hatakuja kama mwivi kwa yeye aaminiye, maana anaweza kujua unabii na
kujiweka tayari kwa ujio wa Yesu. Ndio maana Paulo anasema, “Bali ninyi ndugu,
hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.” 1 Wathesalonike 5:4.
Mara nyingi wahubiri huhubiri kuhusu mafungu mawili yanayofuatia katika nukuu
hiyo ya Paulo na kisha wanasimamia hapo tu. sababu ni kwamba, kama watalihubiri
fungu hilo hapo juu, kondoo wao watahitaji kufahamu ni jinsi gani Wakristo baadhi
watakutwa hawako tayari au wako gizani wakati Yesu anarudi. Lakini mhubiri huyo kwa
vile hajifunzi unabii na wala hajui unabii vya kutosha ili aweze kuwasaidia wasikilizaji
wake, hivyo anakwepa kusoma fungu hilo ili kuepuka maswali atakayoulizwa kutokana
na fungu hilo.
Kuna matukio mengi ya kiunabii ambayo yameshatimia katika siku zetu hizi kiasi
kwamba sina nafasi ya kuyaelezea maana kila mtu anaona hali ilivyo. Moja ya unabii
muhimu sana katika siku hizi za mwisho ni ule wa mnyama wa namba mia sita sitini na
sita. Baadhi ya matukio ya kiunabii hayaonekani kuwa ni unabii na watu wengi
wamechukulia kuwa ni hali ya kawaida ya asili kutokea. Wakati tunaamini kwamba Yesu
aliahidi kwamba atarudi tena kuwachukua walio wake, baadhi wameifanya hiyo ahadi
kuwa mzaha na hilo lilielezwa na mtume Petro, akasema,“…..Mkijua kwanza neno hili ya
kwamba katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu wenye kudhihaki, wafuatao
tamaa zao wenyewe, na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana tangu
hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa
kuumbwa.” “Watayakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe
watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao
watajiepusha wasisikie yaliyo ya kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” 2 Petro 3:3,4; 2
Timotheo 4:3,4. Hili nalo ni tukio la kiunabii maana limetimia. Utakuta ukimwambia mtu
akusubiri utarudi muda si mrefu, anakuambia “Umekuwa Yesu?” Akimaanisha kwamba
Yesu alisema atarudi lakini hajarudi na hatarudi hivi karibuni. Bahati mbaya wengi wa
watu hawa, wenye dhihaka, ni wale wanaodai kuamini mamlaka kuu ya Biblia.
Wanaamini kwamba Yesu atarudi lakini sio sasa ila ni miaka mamia ijayo. Sasa hapa
Mungu anatupatia unabii wa siku za mwisho kuhusu mnyama wa ajabu ambaye
anatambulika kwa hesabu ya kibinadamu. Wakati Mungu anatumia wanadamu kama
wakala wake katika kupeleka nuru ulimwenguni, Shetani naye anatumia wanadamu kama
wakala wake wa kueneza dini ya Shetani. Mungu anawaita mawakala wake kuwa ni
Wachungaji, Wainjilisti, Mitume, Manabii na watu mmoja mmoja kama washiriki wa
upande wa Mungu. Shetani amekuwa akiwaita mawakala wake kuwa ni Illuminati na
Freemason ambao hata hivyo hujigeuza na kujiita kama wachungaji, Wainjilisti, Mitume
Manabii kumbe kwa ndani ni mbwa mwitu wakali. Nitapaje kuwatambua Freemason na
Illuminati hata kama wanajiita majina ya wakala wa Mungu? kitabu hiki kitatoa majibu
mengi ya maswali yako. Napenda pia kuomba radhi mapema kwa kutokutafsiri baadhi ya
maneno yaliyoandikwa kwa lugha ya Kingereza; hii ni kutokana na umuhimu wa maneno
hayo kuwa katika lugha iliyotumika kuyaandika na pia kubana nafasi ili kitabu kisiwe
kikubwa. Naamini kwa wale wasiojua lugha ya Kingereza watapata watu wa kuwasaidia
kujua maana ya maandishi hayo kwa kuwa ni ya muhimu pia.
Baada ya kujifunza yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki utaweza kutambua yafuatayo:
1. Malengo na matukio ya Mpango Mpya wa Ulimwengu—-New World Order.
2. Madhara yatokanayo na mpango huo kwa kila mtu duniani.
3. Jinsi mpango huo unavyoathiri hata sasa kila mtu, kila familia na kila dini hata
kabla ya hitimisho la mpango huo.
Ukiwa umeshapata ujuzi na ukweli huu utaweza kujua jinsi ya:
1. Kujilinda wewe mwenyewe dhidi ya mpango huu, kuwalinda watoto wako,
kuilinda familia yako na wote uwapendao.
2. Kuishi maisha ya Kikristo huku ukiwa ni mshindi ndani ya ulimwengu huu wa
giza kuu la kiroho kwa sababu utaijua kweli nayo kweli itakuweka huru.
.