Ukweli kuhusu pesa za kujikimu za walimu

Ukweli kuhusu pesa za kujikimu za walimu

Felicity

Member
Joined
Dec 2, 2011
Posts
21
Reaction score
3
Tunashangaa Tamisemi kwenye tangazo lao walisema pesa za kujikimu tutazikuta kwenye halmashauri zetu lakini cha ajabu watu wamefika kuripoti halmashauri wamejaza tu mikataba na vitu vingine vyote kisha wakatangaziwa warudi walipotoka kwa kuwa pesa za kujikimu hamna.

Hii serikali yetu vipi jamani?
 
We ulizani pesa IPO???? Piga kazi kijana ndo nchi yako hiyo
 
naomba kujua kutok kwenu niny mliokwxha ripot, hz fedha ni kwel zpo? na znatolewa baada ya muda gan? na kwa njia ip?
 
Naomba usishangae sana mkuu bado mapema sana.Hilo sio ajabu sana

More wonders to come!!!Utashangaa sana nchi hii!!!
 
Naomba usishangae sana mkuu bado mapema sana.Hilo sio ajabu sana

More wonders to come!!!Utashangaa sana nchi hii!!!

wanashangaa jambo dogo hivyo ndo kwanza masuprise yanakuja kibao looo watulie tu maana watataman wastaafu after 6 months
 
Eleweni hela ya kujikimu kwa mujiju wa kanuni za utumishi wa uma hulipwa na halmashauli husika hivyo inategemea na mapato yao, pia inategemea kama wana pesa kwa mda huo, hivyo unaweza kuanza kazi na dai kwa barua na endelea kufatilia na kukumbushia mara kwa mara watakulipa. ukiambiwa kurudi nyumbani mpaka salary isome ni sawa kwanza hapo nifeva kwani wengine huambiwa kuendelea na kazi wakati chambi hakuna. pia msiporuhusiwa mashureni muendako waambieni wakuu wawatunze mpaka bum litoke au mmbane ded awakopeshe ila huwa wanakopesha km mm kipindi naajiriwa ded alitukopesha, kila lahel . kumbuka sasa hivi unaitamani kazi hata usingizi hauji subiri miaka mitatu baada ya kuzoea utaanza kuijutia kwa nini niliajiliwa. maisha mema!
 
Huku meru hata vituo hatujapewa ni shida tuu tunahangaika mitaani,unashinda halmashauri na hupewi taarifa ya maana,mfano leo mpk saa hii tupo hapa na hatujaambiwa kitu.
 
Mfanyee makeke huko mwendako hayoo yote ni kutokana na udhaifu wa serikali yenu so msirudie kisa Oct
 
Sasa unambie nirudi, Geita kutoka Mtwara?

Pole jiran yangu kupangwa mbali, cha msingi mbaneni mkuu wa idala asipo eleweka bana ded asipo eleweka muoneni mwenyekiti wa council au mkuu wa wilaya mkiwa wote sio mmojammoja. tofaut na hapo ukiwa pekeyako ongea na mwl mkuu wako akutafutie hifadhi
 
Huku meru hata vituo hatujapewa ni shida tuu tunahangaika mitaani,unashinda halmashauri na hupewi taarifa ya maana,mfano leo mpk saa hii tupo hapa na hatujaambiwa kitu.

Daima jua kuhangaika kwako ndo neema yao yawezakua kuna vitu wanachelewesha maksudi ili wapate posho, muone mwenyekit wa council huyo atakachosema kinafanyiwa kaz tena haraka. pia mkuu wa wilaya, inategemea na nani kwenu ni muwajibikaji kat ya hao.
 
Tunashangaa Tamisemi kwenye tangazo lao walisema pesa za kujikimu tutazikuta kwenye halmashauri zetu lakini cha ajabu watu wamefika kuripoti halmashauri wamejaza tu mikataba na vitu vingine vyote kisha wakatangaziwa warudi walipotoka kwa kuwa pesa za kujikimu hamna.

Hii serikali yetu vipi jamani?

Kazi ya ualimu kimsingi ina changamoto nyingi toka siku unajaza mkataba wa ajira hadi unastaafu
 
Kazi ya ualimu kimsingi ina changamoto nyingi toka siku unajaza mkataba wa ajira hadi unastaafu

Nakushauri kuwa mvumilivu na yasome mazingira ulikopangwa kuharibu na kufanya shughuli za ujasiriamali kuongeza kipato, bila maarifa ya ziada hata kujenga hutoweza ndugu!
 
Wanaposema ualimu ni WITO si masikhara. Komaeni.
 
Da Hii Kali Sasa Hata Sisi Tumeripoti Kyela Hakuna Hela Za kujikimu Na Kwa Taarifa Za Chini Chini Kutoka Kwa Mmoja Wa Wakuu Wa Shule Kubwa Kasema Tujiandae Kisaikolojia, Kwan Hata Mshahara Inawezekana Tukaanza Kupata Mwezi Wa 6 Au 7 Maana Serikali Haina Hela
 
Hao wana hela waache uboya,wanazizungusha ktk biashara then watawapa waksha pata kafaida kdogo,dain hela zenu mkiwa wote na c mmoja mmoja,MADAI YA WATU WENG HUSIKILIZWA KULKN MTU MMOJA
 
Back
Top Bottom