Naona nianze na historia kwanza kwa faida ya wasomaji coz' naona hii ya kwako haija-expose vizuri chanzo cha uhasama kati ya Wahutu na Watusi!
HISTORIA FUPI: Hapo awali eneo ambalo hivi sasa ni Rwanda na Burundi hapakuwa na watu ambao wanafahamika kama Watusi hivi sasa; kwa maana hiyo, asili ya watu wa eneo hilo ni Wahutu!
Watusi walitokea Ethiopia, na kama ilivyokuwa enzi hizo, walipofika eneo ambalo sasa ni Rwanda na Burundi, Watutsi waliwavamia na kuwashinda vita wenyeji; Wahutu! Kimsingi, the guys(Tutsi) ni warriors since then kama yalivyo makabila mengi ya wafugaji....labda ni kwavile wameshazoea kufukuzana na wanyama wakali katika kulinda mifugo yao; tofauti na mkulima; yeye akimuona simba au chui atakimbia; by the way si simba wala chui anayekula mahindi lakini ukisusa mifugo kwa hao jamaa, imekula kwako (Hapo kwenye RED, tafsiri ni yangu kwahiyo msinidai ushahidi kwavile sina)!!!
Wakati wa ukoloni, Wakoloni waliwatumia sana Watusi kuwa-oppress Wahutu coz' Watutsi wao ndo walikuwa watawala. Inasemekana oppressing ya Watusi kwa Wahutu ilikuwa kubwa sana pengine kuliko sehemu zingine barani Afrika. Na wata Walipoingia Wabelgiji baada ya WWI, wakaendeleza hali hii, ya kuwatumia Watusi kuwa-opress Wahutu!
Lakini cha ajabu, wakati Wabelgiji wanakaribia kuondoka, wakaanza kuwaingiza baadhi ya Wahutu madarakani. Later on, kwa ushawishi wa kanisa Katoliki, Mchungaji wa Kihutu akatoa Waraka wa kuitaka Ubelgiji kukabidhi madaraka kwa Wahutu! Sujui kwanini RC waliwa-favor Wahutu, sina uhakika labda kwavile Wahutu walikuwa ni oppressed community or kutokana na ukweli kwamba kwa kawaida Wakulima walikuwa na muda wa kushiriki dini za wazungu kuliko Wafugaji na hivyo bila shaka Wakulima(Wahutu) wengi zaidi walikuwa wamempokea YESU kuliko Wafugaji Watutsi na hivyo RC kuamua kutoa upendeleo kwa waumini wao Na in fact, labda hapo ndipo unaweza kuona ni kwa vipi Kanisa lilihusika na mauaji ya kimbali kwa namna moja au nyingine!(Kwa mara nyingine, hapo kwenye RED, tafsiri ni yangu kwahiyo msinidai ushahidi kwavile sina)!!!!
Aidha, kufuatia Waraka huo, Wahutu wakaanzisha vyama vya kisiasa kama njia ya kujiandaa kutwaa mamlaka kutoka kwa Mkoloni Mbelgiji. Na historia inasema kwamba hata uanzishwaji wa vyama hivi ulisimamiwa na Kanisa!
Wakati Wabelgiji wamekaribia zaidi kuondoka, ukaitishwa uchaguzi ambapo (wengine wanasema wa kimagumashi) na chama cha Kihutu kikashinda! To make things even worse, pakapigwa kura ya kama Ufalme uendelee kuwapo au ufutwe! Tusisahau, ufalme ulikuwa unashikiliwa na Watusi wachache ambao ndo walikuwa wenye nguvu...this means that, mshindi huyu wa Kihutu alikuwa chini ya Ufalme wa Kitutsi! Hata hivyo, kama ilivyotarajiwa, wengi waka-vote against Monarch na hivyo Mhutu aliyechaguliwa akapata wasaa wa kujinafasi!! Na hivyo, mwanzoni tu mwa utawala wake akaanza kuwashighulikia Watutsi ambao walikuwa madarakani! Na katika kipindi kifupi, Watusi wakaonja joto ya jiwe kwani walishughulikiwa kila idara na wengi waliuawa na wengine wakaikimbia Rwanda! In short, ni kama walikuwa wanalipiza kisasi cha kuwa oppressed for centuries!
Hali hii ya uhasama iliendelea na kuja kuzalisha mauaji ya kimbali ya 1994 ambayo chanzo chake ni kutunguliwa kwa ndege ambayo ndani kulikuwa na Rais Habyarimana ambae alikuwa ni Mhutu!
SASA TURUDI KWENYE MADA:
Kwanza ni kweli kabisa uvamizi wa wageni ndani ya ardhi ya Tanzania unatokana na udhaifu ulio ndani ya uwezo wetu wenyewe! Hata hivyo, hilo hali-justify wageni kuingia na kutoka watakavyo! Huwezi kufika kwenye duka la mtu kisha ukaiba kwavile tu mwenyewe hajafunga! Ukikamatwa, utahukumiwa kwa wizi na wala hakuna atakayejali kwa utetezi kwamba ulikuta duka halijafungwa!!
Ni kweli pia kwamba mataifa uliyotaja ni ya watu wa mchanganyiko lakini kote huko kuna utaratibu wa mtu kuingia na sio tu kuingia utakavyo! Ukifanya hivyo na ukagundulika utawajibishwa! Na kama serikali imelala, raia wema wa nchi husika watapandisha sauti kulalamikia wahamiaji haramu! Labda tatizo la Mtikila ni aina ya lugha aliyotumia lakini kwa anayemfahamu hawezi kumshangaa!! Binafsi ningeshangaa endapo angetumia lugha ya kiungwana, lakini mtu ambae alipata kuita Mwili wa Baba wa Taifa kwamba ni mzoga sijui kama ni ajabu kuwaita Watusi ni nyoka! Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita Mtikila huyu huyu alipata kum-refer Mkapa kwamba ni Mmakonde wa Musumbiji ambae anatakiwa kutiwa kwenye lori na wamakonde wenzake kisha wakamwage mpakani! Lakini tukichuja maneno yake mabovu na ya kibaguzi, bado hoja yake inabaki kuwa ya msingi na katu uozo wa mipakani usiwe justification!
Mwisho ningependa kuzungumzia hilo la eti Kagame alikuwa tayari kufa kwa ajili ya Tanzania! Hebu jisikie aibu kwa hoja kama hiyo kwani hata kama ni kweli Kagame alishiriki kwenye vita vya Kagera, katu hakufanya hivyo kwa maslahi ya Tanzania bali alifanya hivyo kwa maslahi ya Museveni....ilikuwa ni lazima Museveni apate nchi ili nae (Kagame)apate nafasi ya kuendeleza harakati zake!