Ukweli kuhusu treni ni huu; Wengi Hawaujui

2. Mfano nchi kama Marekani na Canada mtu anayeendesha treni wanamuita Locomotive Engineer, India wao locomotive pilot, kwa nchi za Australia na common wealth wanaita locomotive driver hata hapa kwetu Tanzania.
HUO UTOFAUTI ni mbwembwe tu, Ukweli ni kwamba Dereva wa chombo chochote hupewa jina lake kutokana na aina ya chombo!
Msingi wa neno Dereva ni mlazimishaji, mswagaji au mpelekeshaji, Baadae neno hili ndipo likaanza kutumika kama mwongozaji!

Ndiyo maana kuna kiswahili watu huambizana, sitaki uniendeshe au unipelekeshe (Dont drive me crazy)

Treni haiendeshwi kama gari, maana yenyewe ni mtambo uko kwenye barabara yake, unalala hapo hapo, unateleza hapo, maisha yake ni hapo relini kama mitambo mingine ya viwandani, Hivyo inaongozwa na OPARETA au jina la kimtambo MACHINEST (fundi mitambo)
 
Sio treni pekee, vitu vingi sana vinetengenezwa kwa mfumo wa female & male zikiwemo cables, industrial plug, pipes, hose coupling, necklace, disconnector switch, USB, VGA, nk
Dah juzi nimenunua USB mpya inazingua, mwonekano mzuri ila kujaza simu masaa kibao.

Sasa nimeelewa, litakuwa demu hili puuzi!
 
Hii breaking system ya train kwann haiwi applied kwa magari ya kawaida hasa magari makubwa

Naona Kama itapunguza ajali sana
 
Sijajua kama ni mbwembwe ila naamini kuna maana yake nzuri tu ila tuachie hapo.
 
Hii breaking system ya train kwann haiwi applied kwa magari ya kawaida hasa magari makubwa

Naona Kama itapunguza ajali sana
Katika taaluma ya braking system ya railway,
ipo hivi katika mifumo ya breki za treni ina utofauti mkubwa kiasi na magari makubwa japo kuna baadhi ya valve zake zinaweza kuwa na majina na utendaji unaofanana utofauti ni kwamba katika service brake application ( yani breki ya kawaida tu kupunguza mwendo au kusimama) kwenye treni ni kupunguza kiwango cha pressure ya upepo katika mfumo unaoitwa Brake Pipe ambapo kuna kiwango maalumu kikiwekwa automatically brake inaachia magurudumu na endapo hicho kiwango kitapungua kwa sababu yoyote ile basi brake zitakamata kuna kifaa kinaitwa distributor katika locomotive na kila behewa ndiyo moyo wa brake system na ndicho kinafuatilia ongezeko au punguzo lolote la pressure ambalo dereva ataruhusu kupitia brake valve handle ili kufanya breki kukamata au kuachia gurudumu.

Tofauti kidogo na mfumo wa gari ambao dereva hukanyaga treadle valve ili kutoa control pressure iende kwenye relay valve ili kuruhusu upepo kwenda kwenye brake chamber na kusukuma pushrod na slack ili pad ikamate drum kupunguza au kusimamisha gurudumu.

Mfumo wa treni kidogo complicated kwasababu ya urefu wa treni na kuwa valve nyingi kwa kazi mbalimbali.
Japo kwa dunia ya sasa kwanzia kwenye treni hadi magari makubwa mifumo ya breki imekuwa ya kieletroniki sana mfano katika treni zenu za SGR si za full pneumatic ila ni Computer controlled braking.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ