Ukweli kuhusu viumbe wa ajabu wanaovamia dunia.

Ukweli kuhusu viumbe wa ajabu wanaovamia dunia.

comrade igwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2015
Posts
7,295
Reaction score
3,950
upload_2017-11-26_11-50-31.png


upload_2017-11-26_11-54-42.png



obama-meets-alien.png


Kuna minong'ono na maneno ya wazi kwamba kuna viumbe wa ajabu wamekimbilia katika dunia na kusababisha hofu na wasiwasi wa maisha ya binadamu wa kawaida, kwa mujibu wa mwanasayansi wa fizikia na nyuklia raia wa Canada Bwana Stanton Friedman amesema dunia imekua ikitembelewa sana na viumbe wa ajabu maarufu kama Aliens kwa lengo la kuangalia mienendo kadhaa ya kitekinolojia na maisha ya kawaida na muda sio mrefu wataweka makaazi kabisa duniani, "Hakuna doa la mashaka kwamba viumbe wa ajabu wenye akili nyingi sana wanafanya safari zao kuja duniani"

Bwana Friedman mwenye umri wa miaka 82 alikua akichunguza ajali ya chombo cha anga za juu hususani ajali ya mwaka 1947 iliohusu chombo cha anga kilichopata ajali mbaya katika anga za juu na kueleza kilipotezwa na kitu kisicho cha kawaida kabisa kilichokua na viumbe wa ajabu,

aidha, amesema faili lenye taarifa za siri sana za CIA juu ya uwepo wa viumbe hao ni moja ya ushahidi wa uwepo wa viumbe hao, anasema anafikiri viumbe hao maarufu Aliens wanataka kulinda anga lao ambalo limekua likitembelewa sana na vyombo na binaadamu kutoka duniani, nae aliekua Waziri wa Ulinzi wa Canada Paul Hellyer amesema dunia imekua ikitembelewa na viumbe hao kwa miongo kadhaa sasa amesema mwaka 1995 viumbe hao walitembelea dunia amesema mwaka 1961 kulikua na vyombo vya anga vya ajabu 50 vilivyojulikana kama UFO na visivyo vya kawaida kabisa vikiruka kutoka kusini ya dunia vikielekea Urusi na Ulaya.
 
Hili suala la aliens lina miaka mingi sana linaongelewa toka miaka mingi kabla ya kristo
 
Hakuna kitu kama hicho ni conspiracy game iliyokuwa inafanyika au inatumika katika jamii za wazungu koko ili kuwatenga baadhi ya wavumbuzi, watu wenye akili sana au hata mtu aliyeonekana kuwa atachukua uongozi wa nchi.

Basi , walimpakazia kuwa ana asili au mama yake mzazi alizaa na hao viumbe wa kusadikika ili watu wapate hofu ya kumchagua au kumkubali hata kufikia hatua ya kumtenga fulani hivi.

Siku hizi, za dini ya warabu pori na wazungu koko mnawaita hao viumbe wa kufikilika (aliens) kuwa ni mapepo au majini siju maruhani.

Mbona huku Afrika hawajawahi kuja!?

Kwa nini hawajawahi kuwakamata live.watuoneshe kwenye taarifa zao na aweke eneo tukamuone sote?

Je mahitaji yao hapa duniani yameisha kama ilivyokuwa hapo awali kuwa walikuwa wanakuja kuchukua mitambo na machine zao huku chini ya ardhi?

Wazungu koko ni wanafiki na watu wa fitina sana.

Any way, waafrika nao ni balaa tupu, wakiambiwa au kusikia tu chochote watazunguka nacho miaka Nenda rudi mwisho watajiaminisha kuwa ni ukweli.

Hata, Obama , mwaka 2008 walioanza kusema habari za ajabu juu yake kuwa naye anaongozwa na mara mapepo, oooh oooh ana alama Kichwani kama aliyeondolewa ubongo akawekewa mitambo ndani ya fuvu /Kichwa chake mara ana mkono wa kivuli.

Ila hali hizo zote ni kutaka kufanya mtu apoteze mvuto na kukubalika.
 
Back
Top Bottom