View attachment 638165
View attachment 638169
Kuna minong'ono na maneno ya wazi kwamba kuna viumbe wa ajabu wamekimbilia katika dunia na kusababisha hofu na wasiwasi wa maisha ya binadamu wa kawaida, kwa mujibu wa mwanasayansi wa fizikia na nyuklia raia wa Canada Bwana Stanton Friedman amesema dunia imekua ikitembelewa sana na viumbe wa ajabu maarufu kama Aliens kwa lengo la kuangalia mienendo kadhaa ya kitekinolojia na maisha ya kawaida na muda sio mrefu wataweka makaazi kabisa duniani, "Hakuna doa la mashaka kwamba viumbe wa ajabu wenye akili nyingi sana wanafanya safari zao kuja duniani"
Bwana Friedman mwenye umri wa miaka 82 alikua akichunguza ajali ya chombo cha anga za juu hususani ajali ya mwaka 1947 iliohusu chombo cha anga kilichopata ajali mbaya katika anga za juu na kueleza kilipotezwa na kitu kisicho cha kawaida kabisa kilichokua na viumbe wa ajabu,
aidha, amesema faili lenye taarifa za siri sana za CIA juu ya uwepo wa viumbe hao ni moja ya ushahidi wa uwepo wa viumbe hao, anasema anafikiri viumbe hao maarufu Aliens wanataka kulinda anga lao ambalo limekua likitembelewa sana na vyombo na binaadamu kutoka duniani, nae aliekua Waziri wa Ulinzi wa Canada Paul Hellyer amesema dunia imekua ikitembelewa na viumbe hao kwa miongo kadhaa sasa amesema mwaka 1995 viumbe hao walitembelea dunia amesema mwaka 1961 kulikua na vyombo vya anga vya ajabu 50 vilivyojulikana kama
UFO na visivyo vya kawaida kabisa vikiruka kutoka kusini ya dunia vikielekea Urusi na Ulaya.