MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Katika Hospitali na vituo vya afya vyote vya Mkoa wa Arusha hakuna majeruhi wa vurugu zilizojitokea wakati Wamasaai wakizuia zoezi la uwekaji wa mipaka katika Pori Tengefu la Loliondo,
Imeelezwa kuwa kama kuna watu waliojeruhiwa katika virugu hizo wajitokeze ili wapatiwe matibabu
Imebainika kuna kundi la Wamaasai kutoka nchi jirani (nchi hiyo nimehifadhi kwa jina) waliingia nchini kuzuia uwekaji wa mipaka katika pori hilo na baada ya kushindwa kutimiza azma hiyo walikimbia na kurudi katika nchi hiyo ya jirani wakiwa na majeraha
Ikukumbukwe kuwa zoezi la uwekaji mipaka ni kwa ajili ya kulinda uhai wa wa pori dhidi ya shughuli za binadamu kwa kuwa pori hilo ndilo uhai wa hifadhi za Serengeti na Ngorongoro.
Pia mipaka hiyo itasaidia kuzuia wawindaji haramu na wafugaji kuingiza mifugo katika pori hilo na katika hifadhi za Ngorongoro na Serengeti _ hususan kutoka nchi jirani ambao wamekuwa na mazoea na kujinuifaisha na maliasili zilizopo Nchini Tanzania
Wito kwa Watanzania kuiunga mkono Serikali kwa kuwa zoezi la uwekaji mipaka katika pori hilo linamanufaa makubwa kwa Taifa kwa linalinda maliasili kwa maslahi ya vizazi vya sasa na baadae
Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿