Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
FM La kwanza ni kukubali kwa serikali kuwa imepitika dhulma. Kisha hapo ndiyo tutashauriana nini cha kufanya. Tusisubiri hadi unga uzidi maji tutakuwa tumechelewa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
FM La kwanza ni kukubali kwa serikali kuwa imepitika dhulma. Kisha hapo ndiyo tutashauriana nini cha kufanya. Tusisubiri hadi unga uzidi maji tutakuwa tumechelewa.
Mkuu Kiranga,
Unarudia kosa la wengine kufanya kuwa Dar ilikuwa ni kule palipoitwa uswahilini peke yake. Nyerere hakuambiwa asivae kaptula bali alifahamishwa kuwa anapokutana na wazee wa Dar es salaam ( ambao wengi walikuwa waislamu) asivae kaptula maana hawatapendezwa kuona kijana kavaa kaptula. Akiwa na wasomi wenzake Magomeni na kwenye klabu zao, kaptula ruksa. Hii ku-conflate Dar es Salaam na uislamu ndiyo uliotufikisha hapa. Hapa Dar es Salaam walikuwepo wanyasa kibao ( wakina Kambona n.k.) ambao vazi lao lilikuwa kaptula na kuweka "wei", Nyerere na kaptula yake asingeonekana mtu wa ajabu. Tatizo lilikuja pale alipotaka kukutana na watu ambao mila na desturi zao hazikukubali uvaaji huo. Hawa ingawa walikuwa wengi lakini hawakuwa ndiyo reflection ya Dar es salaam nzima ya wakati ule!
Kosa hili ndilo linalompelekea Mohamed kudhani kuwa Tanganyika ilikuwa Dar es Salaam na kidogo Tanga peke yao. Anasahau umati mkubwa wa watu wa bara ambao bila wao hamna kitu ambacho kingefanyika. TANU bila kukubalika kwa hao wengine, ingekosa legitimacy na hapo ndipo Nyerere alipomzidi Sykes., uwezo wa kukubalika nchi nzima na si mkoa wa Pwani peke yake!
Amandla........
Kukataa kwamba Dar ya early 50's ilikuwa mainly uswahilini ni kukataa ukweli tu.
Mkuu hapa sasa unakosea. Huwezi kusema kuna mkono wa Nyerere hjali hujawahi kuzungumza na Jumbe na ukamuuliza yeye kuhusika kwake wala kuandika ubaya wowote unaomhusu Jumbe. Hapa nikiwa na maana kama wewe umeweza kujua Nyerere ndiye alitoa order kwa Jumbe afenye vile kwa nini usianze na Jumbe, Kawawa au na wengine, bila shaka kitabu chako chote kinaepuka kutoa lawama kwa Waislaam.. ndivyo nilivyokuelewa mimi..Ahsante Mkandara kwa mchango wako. Mimi nimezungumza yote hayo Nyerere akiwa hai. Sikupata kumuogopa na yeye hilo alilijua fika. Hakuthubutu kunijibu hadi anaingia kaburini. Hapa unaona jina langu kamili sijajificha nyuma ya pazia kwa kuwa nakiamini ninachosema.
Ama ya Mzee Jumbe, Kawawa, Adam Nasibu na wengineo ningependa kama maswali hayo wangejibu wenyewe. Nyerere namlaumu kwa kuwa mkono wake ulikuwapo katika kuwahujumu Waislam na hili linaonekana katika maandiko yangu yote.
FM nimekujibu kwanza serikali ikubali lipo tatizo. Serikali haikubali kuwa kuna ubaguzi na ushahidi ulipotolewa na Prof. Hamza Njozi katika kitabu chake "Mwembecha Killings" ilichofanya serikali ya Benjamin Mkapa ni kupiga marufuku kitabu. Waliyoana mle yamewatisha sana.
FM Ahsante kwa mchango wako. Hilo linawezekana sana. Migonganon katika jamii ni jambo la kawaida. Kubadilishana fikra kama hivi ni jambo jema nami unanisomesha yale ambayo yamenipita au sikuyaona kama ulivyoyaona wewe.
Mkuu hapa sasa unakosea. Huwezi kusema kuna mkono wa Nyerere hjali hujawahi kuzungumza na Jumbe na ukamuuliza yeye kuhusika kwake wala kuandika ubaya wowote unaomhusu Jumbe. Hapa nikiwa na maana kama wewe umeweza kujua Nyerere ndiye alitoa order kwa Jumbe afenye vile kwa nini usianze na Jumbe, Kawawa au na wengine, bila shaka kitabu chako chote kinaepuka kutoa lawama kwa Waislaam.. ndivyo nilivyokuelewa mimi..
Ushahidi gani tena wautaka?...Waislam hawataki Apology, wanataka HAKI itendeke....na hii ndio misconception kubwa mliyonayo mnafikiri waislam wanataka favor..waislam wanataka Haki itendeke.Hamjatoa ushahidi wowote wa structural disrimination bali statistics zinazoonyesha kuwa waislamu hawafanyi vizuri shuleni kuliko wakristu. Ni ndoto za alinacha kutegemea serikali ikiri kitu ambacho hakipo. Na kukazania kuwa hamko tayari kuishauri serikali namna itakavyoweza kuwasaidia waislamu wenzemu ni kuwa irresponsible kuliko kifani maana wakati mkisubiri hiyo apology wenzenu wanasonga mbele na gap inazidi kuongezeka! Ndio maana nasema hamna nia ya kuwasaidia wenzenu bali kuhakikisha hata kile kidogo walichonacho hawatafaidi! Kama mnakataa kumshauri rais wenu ambaye ni muislamu mwenyenu kweli mtaweza kukaa meza moja na mkristu?
Amandla.........
...Fundi nafikiri unashindwa Kujua situation za wakati wa Mwalim na Hao unaowaita "Waislam"...hao wote unaosema walikuwa hawafuruki kwa Nyerere. Ikiwa Nyerere aliweza mficha Jumbe....hayo mengine madogo angeshindwaje? Hao walikuwa wapokea Order tu....!!!Hapana, Mkuu. Shida ni kuwa haukuwa na nia ya kutafuta ukweli bali ulitaka kuwamalaikisha waislamu na kuwaatupia lawama zote wakristu. Maandiko yako yenyewe yanakusuta. Hakuna mahali ambapo hao wazalendo hawakushirikiana wakristu kwa waislamu. Kama unyanyasaji na chuki, Nyerere hakuwaonea waislamu peke yao. Unalalamika kuwa wakina Sykes na wakina Mwapachu hawakuenziwa wakati humo humo unaelezea mchango mkubwa wa wakristu wakina John Rupia, Vedasto Kyaruzi, Mwanjisi na wengine. Unazungumziwa kuwekwa ndani viongozi wa vyama vya wafanyakazi na nyerere lakini humo humo unawataja wakristu walioswekwa ndani! Unakiri kuwa ni Jumbe ndiye aliyeuwa EAMSW lakini haumlaumu bali unamshupalia Julius.
Unasahau wakina waziri wa mambo ya ndani wa wakati huo ambaye aliyeandika na kusaini agizo la kuipiga marufuku EAMWS! Hauzungumzii mkutano uliofanyika 1968 ambapo Karume aliikemea EAMWS kuwa inapingana na sera ya ujamaa na ipo kwa ajili ya wageni! Hii ilikubalika kwa wengi wakati ule kwa sababu kila mtu alijua kuwa ingawa viongozi walikuwa Tewa na Bibi Titi lakini msukumo wa kipesa ulitoka kwa waislamu wa kihindi ambao walikuwa wafanya biashara ambao bila shaka hawakufurahia Azimio la Arusha. Yote haya huyaoni, unakimbilia kwenye hiyo myth ya Catholic Christian Movement.
Unatuambia kuwa ishara ya kuwa Nyerere kauupenda uislamu ni yeye kutofurahishwa ( bila kutuambia kama aliwakataza) kitabu kilichoandikwa na muislamu Sykes na mkristu Kleruu!
Hapana, Mkuu, ukivaa miwani ya udini inakuzuia kuona hata kilicho wazi. Sisi wakristu tunaamini kuwa kabla ya kutoa boriti katika jicho la mwenzako heri uanze na la kwako. Wewe umekazania kuonyesha makengeza ya wakristu wakati mwenyewe macho yako yanapofuka!
Amandla.....
Chuma,...Fundi nafikiri unashindwa Kujua situation za wakati wa Mwalim na Hao unaowaita "Waislam"...hao wote unaosema walikuwa hawafuruki kwa Nyerere. Ikiwa Nyerere aliweza mficha Jumbe....hayo mengine madogo angeshindwaje? Hao walikuwa wapokea Order tu....!!!
Mohammed Said kaandika tukio lingine la AGIP, Aziz...Nyerere alitoa order ya Kukamatwa Muft wa Tanganyika Shekh Hassan Bin Ameir...AGIP Aziz alikataa hio order...lkn nini kimefanyika...?Nyerere akafanya lake?
Ukisoma vema kitabu utajua Fitna za Nyerere...ilikuwa ukimpinga order zake anakutengenezea Zengwe...unatiwa ndani au kusahaulika kabisa....so hao unaowataja walikuwa Rubber Stamp.
Mzee Jumbe ameandika Kitabu..kitafute pia ukisome...!!!
Hivi waweza kunieleza kuwa Mahakama ya Kadhi na OIC ktk Utawala wa Jakaya umezuiwa na Jakaya?....!!!
Misamaha ya Kodi ya Makanisa imeruhusiwa kwa Serikali kupenda?.....Na hii ndio Christian Lobby anaiyozungumza Mohammed Said...!!!