Ami,
MKANDARA
Huyu ndiye mpuuzi kabisa katika michango yake.Yeye anaonekana ana wazazi waislamu,na anajiita muislamu.Hataki kuudhi upande wowote kati ya hizo.
Usomi wake wote,kama alivyo Fundi Mchundo hataki Nyerere abebeshwe lawama za madhambi yake.Vile vile madhambi ya Christian lobyy anataka lazima lawama zake ziwaendee waislamu.
Akina Mwinyi,Kawawa na viongozi wengine waislamu walikuwa wakitumiwa na kushinikizwa,yale waliyoyafanya leo yanawatukanisha na kututukanishwa sote waislamu.Haya ni moja ya mafanikio ya wakristo kwa waislamu Tanzania,kuwafanya wasijiamini.Hata wakipewa nafasi huona ni fadhila tu,hivyo lazima wafanye kama wanavyoambiwa
Wakati huo huo leo akitokea kiongozi serikalini akitaka kitu cha halali kifanyike chenye mwelekeo wa kiislamu,basi huzushiwa mengi na kurudiwa katiba ili kishindikane kufanyika.Akiondoka tuambiwe kwa mfano "Nini kilimfanya Kikwete na Shein wote waislamu washindwe kuanzisha hiyo mahakama ya kadhi na kujiunga na OIC"
Hapo watasifiwa kuwa ni kwa vile wao ni wazalendo na walijuwa hivi vitu ni vya kibaguzi!.
Mkandara namfananisha sana na wanasiasa uchwara kama Richard Tambwe Hizza,Salim Msabah na Shaib Akwilombwe.Ni mjuzi sana wa kuuchonga lakini anaweza kupanda jukwaani na kusema lolote la kuudhuru upande mwengine.Uchongaji wake wa maneno una uwezo mkubwa wa kuwazuga watu.
Baba yake aliwahi kumpisha kitanda Nyerere apumzike katika juhudi za kuthamini uhuru sijui kwamba na yeye katajwa popote katika historia.Simlazimishi Mkandara kufikiri kama mimi,lakini nashangaa sana kutokuona ubaya wa historia ya TANU kuandikwa bila kutajwa waasisi wake,na jinsi gani asivyoona kuwa huo ni mkono wa Nyerere na wakristo wenzake.Ikiwa hili lina mjadala zaidi basi hakuna sababu ya kujadili chochote cha kihistoria.
Shukran sana mkuu wangu kjwa maelezo yako kwani ndivyo unavyioniona mimi... na hakika na Ramadhan hii nasema mtu yeyote anayependa kujadili watu na hata kutoa hukumu zao ni Mjinga katika wajinga waliopotea unachotakiwa ni kusoma na kuelimika..
Ni kweli wala hujakosea wazazi wangu ni Waislaam na najiita Muislaam lakini sipendi kuudhi Upande wowote jambo ambalo sijui kama ningefanya kinyume kuwalaumu wakristu ndio ningekuwa Muislaam wa kweli. Na pengine nikwambie mimi siwezi kujiita Muislaam kwa sababu sidhani kama nafanya ibada ipaswavyo ila na practice Islaam kama nilivyoagizwa na Kuran..Na siwezi chukia Ukristu kwa sababu ati Muislaam mmoja kaandika chuki zake kwa Nyerere kwa mabaya ambayo hayana Ushahidi isipokuwa hadithi ambazo hazina akili kabisa..
Nitarudia kusema siwezi kuamini Nyerere kuukandamiza Uislaam wakati woote kabla ya Uhuru na baada ya Uhuru ikiwa asilimia kubwa ya waanzilishi wa harakati hizo walikuwa Waislaam. Waislaam walikuwa minority kabla ya Uhuru leo hii ni hesabu kubwa sawa ama zaidi ya Wakristu..
Na kwa Ushuhuda wangu hiyo nguvu ya Kanisa kuteka chama cha TANU sikuweza kuiona wakati wangu nikikua na hakuna ushahidi tosha nikiwa mdogo nisiyejua kitu kwani Ni wakristu waliopoteza shule, Zahanati nyingi sana ktk mfumo wa kutaifisha jambo ambalo liliweza kunipa mimi Mkandara wa bara Elimu yangu ndogo ya madrasa..Nina hakika kama shule zile zingekuwa zetu Waislaam hapa pasingekalika hata kidogo kwa sababu ya watu wenye mtazamo kama wako.
Mkuu wangu siwezi kujiunga ktk Ujinga wako ama huo wa Mohamed Said kwani nimeishi ktk wakati wa Utawala wa Nyerere ambaye kwa wakati wote wa Utawala wake ameweza kujenga malengo ya kuwa na Taifa moja lenye kizazi cha Watanzania kwa sababu tu wewe na Waislaam wengine mnafikiria ilikuwa bora Waislaam kuwa na Upper hand katika uongozi wa nchi yetu kwa sababu tu wao ndio walikuwa waanzilishi wa TAA. Na kibaya zaidi ni pale mnapoona kuwa mtu napinga kuwepo kwa tabaka hizi kuwa ndiye mbaya kuliko yule mjenzi wa tabaka za Udini. Watu kama Sheikh Takadir leo ni hero wa Uislaam kwa sababu alimpinga Nyerere akijua fika kwamba Nyerere atakuja kuondoa itikadi inayoongozwa na imani ya dini (Islaam) ktk kuongoza chama cha siasa badala yake kukivika Itikadi za Utaifa ili kukiwezesha chama kupata umaarufu bara.
Sasa kwa wajinga kama nyie mtamwona Takadir ni hero wa Uislaam hali mmnashindwa kuelewa kwamba Tanzania haikutakiwa kuwa nchi ya Kiiislaam na wala haikuwa lengo la kina AbdulWahid, Mwapachu na wengineo kujenga taifa la Kiislaam kama manvyofikiria nyinyi ambao mabadiliko yoyote ya kuondoa itikadi za kidini yalikuwa pigo kubwa pigo la Uislaam wala msitake kujiuliza kwamba hao walimpinga Nyerere walitaka kitu gani tofauti na Nyerere. Kwa nini wanamlaumu Nyerere kwa kutumia Uislaam hali madai yao makubwa yanahusiana na nafsi zao wenyewe na sio kueneza ama kukuza kwa Uislaam nchini.
Sasa kama wewe unashindwa kutofautisha mtu anayetumia Uislaam kwa maslahi yake na yule anayepigania Uislaam, sijui mimi nikusaidie vipi..Yawezekana kabisa Mohamed Said yuko sawa (right) kama madai yake yanayo husiana na AbdulWahid kutopewa nafasi kubwa ktk historia ya nchi yetu kiasi kwamba amesahaulika. Lakini haikuwa kazi ya Nyerere kumuenzi Abdul Wakil bali sisi wote watanzania ambao tulimzika kwa heshima kubwa lakini tukamzika na mazuri yake yote..Ipo kila sababu ya kuandika Biography yake kama mwanzilishi wa harakati na pengine kumuenzi na sii lazima Nyerere afufuke ndio tukubali kwamba hili ni jukumu letu sisi Watanzania.
Yawezekana pia kwamba sisi wananchi wote tuchukue lawama za kutoandika historia ya chama chetu cha TANU kwa kurudi nyuma zaidi ya mwaka 1954 jambo ambalo sijui tuanzie toka mwaka 1929 kuzaliwa kwa TAA ambapo Cecil Matola akiwa rais wa chama na Kleist katibu mkuu..lakini nako tunakuta wakristu kina Mark Makeja waliohamia Dodoma na kufungua tawi la kwanza la chama huko bara.
Kwa hiyo nachoweza kukwambia wewe ni kwamba Uislaam hauwezi kuwa sababu kabisa ya kutumiwa kulaumu Utawala wa Nyerere kwa aloyafanya kwa baadhi ya watu kuwa ilikuwa njama zake against Uislaam. Mimi nakuomba nambie sheria yeyote aloiweka Nyerere kuhakikisha Uislaam unakufa au hauna nguvu ya kusambaa nchini nitakusikiliza sana.. Na nitafanya utafiti wangu kujua zaidi Ubaya wa Nyerere kuhusiana na Uislaam na sio kunambia hadithi za watu (Waislaam jina) walioshiriki ktk jitihada ya kuutafuta Uhuru wa Tanzania hali hakuna historia ya chama wala nchi yeyote duniani imeweza ku cover kila mshiriki ktk Mapinduzi au mageuzi ya Utawala isipokuwa wale walioweza kukumbukwa ktk michango yao. Hata Marekani leo hii wanakumbukwa kina Abraham Lincorn kuliko waanzilishi wa upinzani ktk Utawala wa Muingereza.
Mimi siwezi kushiriki ktk Ujinga huu maanake nimefundishwa kujitegemea ktk kufikiri na hakika kufuata mafundisho ya kitabu ktk kujua haramu na mipaka ya kutumia ulimi wangu napozungumza..Siwezi kujingiza ktk dimbwi la ujinga kuyakubali mnaposisitiza na kulaumu Nyerere na Ukristu kwa sababu tu ujenzi wa Nationalism ulikuwa pinzani na itikadi ya wazee wa Kiislaam waliofikiria kwamba wao ndio walitakiwa kuwa WATAWALA halali nchi yetu ama kulipwa fadhila fulani kwa sababu tu walikuwa waasisi au members wa chama..
Siwezi pia kukubali ujinga unaosisitiza kumlaumu Nyerere kwa sababu hakuna Mtanzania aliyeandika historia ya nchi yetu na kuwataja hawa wazee wahusika hali sii kazi ya Nyerere kuandika vitabu wala historia ya chama. Ni kazi yetu sisi woote na ajabu ya Mungu ni pale unapofikiria kumpa Mohamed Said hadhi ya Thiqqa kwamba kapokea hadithi kama wakati wa Mtume hali haya yote tunayozungumza ni mambo ambayo yametokea wakati wetu na sii hadithi ila sote ni washuhuda wa matukio ya utawala wa Nyerere. Kufananisha Mohamed Said na hadithi za mtume ni ufinyu wa kuelewa hata dini ya Kiislaam zaidi ya nukuu mnazo copy toka tafsiri ya vitabu badala ya kuelewa hizi hadithi zina malengo gani ktk jamii ya kiilsaam.
Kama unataka kuandika Biography ya AbdulWahid hakuna mtu wala Nyerere aliyemzuia mtu yeyote kuandika. Kama ulitaka kuandika historia ya Tanzania na kuonyesha washiriki wake basi waandike wote na sii kuchagua majina ya Waislaam pekee hali unalaumu waliotangulia kwa kuandika historia yenye majina ya Wakristu peke yake. Hii sii akili hata kidogo mwenye akili ataepuka kutumia naye majina ya Waislaam watupu na kuchanganya woote waliohusika kwa kuwapa sifa kila mmoja wao alipostahili bila kujali dini au dhehebu lake..
Maswala ya mahakama ya Kadhi na OIC yanamhusu vipi Nyerere?..Na kweli kama JK na Shein wakishindwa kufanya wanayotakiwa kufanya mimi nadhani kwa jina la dini mnatakiwa kuwalaumu wao maanake mmeweza kumlaumu Nyerere kwa kuwakwamisha waislaam ndani ya utawala wake iweje hii iwe tofauti? iweje iwe Taabu kuwalaumu JK na Shein kushindwa kuwezesha Uislaam nchini wakati wao ndio watawala!..
Kama mliweza kumlaumu Nyerere kwa makosa ambayo hayakuzuia Uislaam wala ibada yoyote ya kiislaam na kwamba yeye ndiye aliwalazimisha kina Jumbe, Kawawa na sijui waislaam kuusaliti Uislaam (nikiuliza like what - hamna jibu wala mfano) kwa nini JK na Shein iwe tofauti wakati ushahidi mnao mbele ya macho yenu kwamba kelele za mlangoni haziwezi kumzuia mwenye kutawala nchi kualala. Nyerere aliweza kuukandamiza Uislaam akiwa rais, huyu JK kwa nini anashindwa kuuneemesha Uislaam kwa nguvu ile ile ya Nyerere kimadaraka au ndio tuseme hawa ni dhaifu kwa sababu ya Nyerere.