Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
FM: Ahsante kwa mchango wako: Kleist hawezi kuwa mnafik yeye ni mwanasiasa tu kama nilivyoeleza katika jibu langu. Juu ya hayo yote tuondoke hapo na tuangalie mengine. Nimeweka ukumbini vipande ambavyo mimi navipenda na hufurahi kila ninapovisoma. Tafadhali tuelekee huko na tuendelee na mjadala wa historia ya nchi yetu.

Mohammed Said , that is where you go wrong! Mjadala huu ni mkubwa na unapobanwa sehemu fulani usirudi kule unapopata unafuu.Na hii ni kwa vile umetengeneza serious allegations against Nyerere and Christianity kwa ujumla.
Wachangiaji kadha wa kadha wamejaribu kuonyesha kuwa kuyatazama matukio yote ya kupigania Uhuru kwa mtazamo wa udini si sahihi.
Hi kwa hakika halita saidia katika kutatua matatizo ya kimaendeleo katika sehemu kadhaa nchini.
Sisi sote ni watanzania na ni lazima tufaidike na matunda ya uhuru, lakini kama hujitayarishi kufaidi matunda haya nani atakulazimisha?
Huu ndio mtazamo wangu na pengine wengi pia.
 
Ami,
Shukran sana mkuu wangu kjwa maelezo yako kwani ndivyo unavyioniona mimi... na hakika na Ramadhan hii nasema mtu yeyote anayependa kujadili watu na hata kutoa hukumu zao ni Mjinga katika majinga waliopotea.

Ni kweli wala hujakosea wazazi wangu ni Waislaam na najiita Muislaam lakini sipendi kuudhi Upande wowote jambo ambalo sijui kama ningefanya kinyume ndio ningekuwa Muislaam wa kweli. Na pengine nikwambie mimi siwezi kujiita Muislaam kwa sababu sidhani kama nafanya ibada ipaswavyo ila na practice Islaam..Na siwezi chukia Ukristu kwa sababu ati Muislaam mmoja kaandika chuki zake kwa Nyerere kwa mabaya ambayo hayana Ushahidi isipokuwa hadithi ambazo hazina akili kabisa..

Nitarudia kusema siwezi kuamini Nyerere kuukandamiza Uislaam wakati woote kabla ya Uhuru na baada ya Uhuru ikiwa asilimia kubwa ya waanzilishi wa harakati hizo walikuwa Waislaam. Hiyo nguvu ya Kanisa kuliteka TAA au TANU sikuweza kuiona wakati wangu nikikua na hakuna ushahidi tosha nikiwa mdogo nisiyejua kitu kwani Ni walkristu waliopoteza shule, Zahanati ktk mfumo wa kutaifisha jambo ambalo liliweza kunipa Mkandara wa bara Elimu yangu..Nina hakika kama shule zile zingekuwa zetu Waislaam hapa pasingekalika hata kidogo..

Mkuu wangu siwezi kujiunga ktk Ujinga wako ama huo wa Mohamed Said kwani nimeishi ktk wakati wa Utawala wa Nyerere ambaye kwa wakati wote wa Utawala wake ameweza kujenga malengo ya kuwa na Taifa moja lenye kizazi cha Watanzania kwa sababu tu wewe na Waislaam wengine mnafikiria ilikuwa bora Waislaam kuwa na Upper hand katika uongozi wa nchi yetu kwa sababu tu wao ndio walikuwa waanzilishi wa TAA. Na kibaya zaidi ni pale mnapoona kuwa mtu napinga kuwepo kwa tabaka hizi kuwa ndiye mbaya kuliko yule mjenzi wa tabaka za Udini. Watu kama Sheikh Takadir leo ni hero wa Uislaam kwa sababu alimpinga Nyerere akijua fika kwamba Nyerere atakuja kuondoa itikadi inayoongozwa na imani ya dini (Islaam) ktk kuongoza chama cha siasa badala yake kukivika Itikadi za Utaifa ili kukiwezesha chama kupata umaarufu bara.

Sasa kwa wajinga kama nyie mtamwona Takadir ni hero wa Uislaam hali mmnashindwa kuelewa kwamba Tanzania haikutakiwa kuwa nchi ya Kiiislaam na wala haikuwa lengo la kina AbdulWahid, Mwapachu na wengineo kujenga taifa la Kiislaam kama manvyofikiria nyinyi ambao mabadiliko yoyote ya kuondoa itikadi za kidini yalikuwa pigo kubwa pigo la Uislaam wala msitake kujiuliza kwamba hao walimpinga Nyerere walitaka kitu gani tofauti na Nyerere. Kwa nini wanamlaumu Nyerere kwa kutumia Uislaam hali madai yao makubwa yanahusiana na nafsi zao wenyewe na sio kueneza ama kukuza kwa Uislaam nchini.

Sasa kama wewe unashindwa kutofautisha mtu anayetumia Uislaam kwa maslahi yake na yule anayepigania Uislaam, sijui mimi nikusaidie vipi..Yawezekana kabisa Mohamed Said yuko sawa (right) kama madai yake yatahusiana na AdulWahid kutopewa nafasi kubwa ktk historia ya nchi yetu kiasi kwamba amesahaulika.

Yawezekana pia kwamba sisi wananchi wote tuchukue lawama za kutoandika historia ya chama chetu cha TANU kwa kurudi nyuma zaidi ya mwaka 1954 jambo ambalo sijui tuanzie toka mwaka 1929 kuzaliwa kwa TAA ambapo Cecil Matola akiwa rais wa chama na Kleist katibu mkuu..lakini nako tunakuta wakristu kina Mark Makeja waliohamia Dodoma na kufungua tawi la kwanza la chama huko bara.

Kwa hiyo nachoweza kumwambia wewe ni kwamba Uislaam hauwezi kuwa sababu kabisa ya kutumiwa kulaumu Utawala wa Nyerere kwa aloyafanywa kwa baadhi ya watu kuwa ilikuwa njama zake against Uislaam. Mimi nakuomba nambie sheria yeyote aloiweka Nyerere kuhakikisha Uislaam unakufa au hauna nguvu nchini nitakusikiliza sana.. Na nitafanya uatafiti wangu na kujua zaidi Ubaya wa Nyerere kuhusiana na Uislaam na sio kunambia hadithi za watu (Waislaam jina) walioshiriki ktk jitihada ya kuutafuta Uhuru wa Tanzania hali hakuna historia ya chama wala nchi yeyote duniani imeweza ku cover kila mshiriki ktk Mapinduzi au mageuzi ya Utawala isipokuwa wale walioweza kukumbukwa ktk michango yao. Hata Marekani leo hii wanakumbukwa kina Abraham Lincorn kuliko waanzilishi wa upinzani ktk Utawala wa Muingereza.

Mimi siwezi kushiriki ktk Ujinga huu maanake nimefundishwa kujitegemea ktk kufikiri na hakika kufuata mafundisho ya kitabu ktk kujua haramu na mikapa ya kutumia ulimi wangu napozungumza..Siwezi kujingiza ktk dimbwi la ujinga kuyakubali mnaposisitiza na kumlaumu Nyerere na Ukristu kwa sababu tu ujenzi wa Nationalism ulikuwa pinzani na itikadi ya wazee wa Kiislaam waliofikiria kwamba wao ndio walitakiwa kuwa WATAWALA halali nchi yetu ama kulipwa fadhila fulani kwa sababu tu walikuwa members wa chama..

Siwezi pia kukubali ujinga unaosisitiza kumlaumu Nyerere kwa sababu hakuna Mtanzania aliyeandika historia ya nchi yetu na kuwataja hawa wazee wahusika hali sii kazi ya Nyerere kuandika vitabu wala historia ya chama. Ni kazi yetu sisi woote na ajabu ya Mungu ni pale unapofikiria kumpa Mohamed said hadhi ya Thiqqa kwamba kapokea hadithi kama wakati wa Mtume hali haya yote tunayozungumza ni mambo ambayo yametokea wakati wetu na sii hadithi ila sote ni washuhuda wa matukio ya utawala wa Nyerere. Kufananisha Mohamed Said na hadithi za mtume ni ufinyu wa kuelewa hata dini ya Kiislaam zaidi ya nukuu mnazo copy toka tafsiri ya vitabu badala ya kuelewa hizi hadithi zina malengo gani ktk jamii ya kiilsaam.

Kama unataka kuandika Biography ya Abdul Wahid hakuna mtu wala Nyerere aliyemzuia mtu yeyote kuandika. Kama ulitaka kuandika historia ya Tanzania na kuonyesha washiriki wake basi waandike wote na sii kuchagua majina ya Waislaam pekee hali unalaumu waliotangulia kwa kuandika majina ya Wakristu peke yake. Hii sii akili hata kidogo mwenye akili ataepuka kutumia naye majina ya Waislaam watupu na kuchanganya woote waliohusika kwa kuwapa sifa kila mmoja wao alipostahili bila kujali dini au dhehebu lake..

Maswala ya mahakama ya Kadhi na OIC yanamhusu vipi Nyerere..Na kweli kama JK na Shein wakishindwa kufanya wanayotakiwa kufanya mimi nadhani kwa jina la dini mnatakiwa kuwalaumu wao maanake mmumeweza kumlaumu Nyerere kwa kuwakwamisha watu fulani iweje iwe Taabu kuwalaumu JK na Shein kushindwa kuwezesha Uislaam nchini..

Kama mliweza kumlaumu Nyerere kwa makosa ambayo hayakuzuia Uislaam wala ibada yoyote ya kiislaam na kwamba yeye ndiye aliwalazimisha kina Jumbe, Kawawa na sijui waislaam kuusaliti Uislaam (nikiuliza like what - hamna jibu wala mfano) kwa nini JK na Shein iwe tofauti wakati ushahidi mnao mbele ya macho yenu kwamba kelele za mlangoni haziwezi kumzuia mwenye kutawala nchi kualala. Nyerere aliweza kuukandamiza Uislaam akiwa rais, huyu JK kwa nini anashindwa kuuneemesha Uislaam kwa nguvu ile ile ya Nyerere kimadaraka au ndio tuseme ndio Udhaifu wa viongozi hawa basi!

UMEMALIZA YOTE! Mpaka Cecil Matola? Iko kazi!

Amandla....
 
The origin of African's modern political activities lies in the Tanganyika Territory
African Civil Service Association (TTACSA), a trade union with welfare
functions established by African civil servants in Tanga as early as 1922. The
210 T. TSURUTA
Union had a branch in Dar es Salaam, but it lapsed during 1928, and most
of its known members transferred to the African Association (AA, Chama cha
Umoja wa Watu wa Africa in Swahili), founded in 1929 after the preceding
European Association and Indian Association in Dar es Salaam. AA's aim, one
of the founders stated in 1930, was "to safeguard the interests of Africans, not
only in this Territory but in the whole of Africa" (Iliffe, 1968: 2-3; Iliffe, 1979:
406-407).
AA recruited some 300 members by 1931 and began to build a clubhouse
in New Street, Kariakoo. Unlike the inclusive musical and sporting clubs,
members of AA in its early days appear to have been primarily educated or
well-off Africans who could afford to pay the rather expensive annual dues. Ten
AA branches were established during the 1930s, and by 1948, it claimed 39
branches and 1,780 members throughout the country (Iliffe, 1979: 408-409,
412-413, 426).
The AA leadership in the earliest days included the English-speaking staff of
the government such as Cecil Matola, educated in a Christian mission, together
with civil servants from the German times including Zibe Kidasi,(72) who had
deeper roots in the urban society. Added to this, the three leading groups of
Africans in Dar es Salaam in the 1920s - former mercenaries (Kleist Sykes),
the Manyema (Mzee Sudi), and the Zaramo (Ramadhani Ali) - were all
represented among the AA's fi rst leaders. Although TTACSA provided much of
its core members, AA was not simply a civil servants' trade union but "a deliberate
attempt to unite civil servants with the leaders of other social groups"
(Iliffe, 1979: 407-408).

Nimeitoa hapa:http://www.africa.kyoto-u.ac.jp/kiroku/asm_normal/abstracts/pdf/24-3/TSURUTA%20195-222.pdf

Mambo yalianza 1922, na si Dar bali Tanga. Nani anaikumbuka TTACSA ambako walitoka wengi wa waasisi wa AA? Conveniently, historian Mohamed Said amewasahau wote hawa na kumuona Kleist Sykes peke yake! Ukweli ni kuwa hakuwa peke yake. Walikuwepo wengi. Walikuwepo waislamu na walikuwepo wakristu. Uongozi ulikuwa na waislamu na wakristu. Mohamed Said anamlaumu Nyerere kwa kujifanya yeye peke yake ndiye aliyeanzisha TANU, sasa wajukuu wa wakina Matola, Mzee Bin Sui, Ramadhani Ali, Zibe Kidasi na wengine watasema nini wakimsikia? Msitake kutuharibia historia yetu kwa kuingiza uovu ambao haukuwepo.

Amandla......
 
Tatizo hapa kuna conflict of loyalty.

Kuna waislamu fulani wanajiona wanatakiwa kuwa loyal kwa uislamu zaidi kuliko utaifa. Na Nyerere hakutaka mambo kama haya akawakatilia mbali taasisi zao kwa sababu za usalama wa taifa. Waislamu hawa wanaona walionewa.

Kuna watu hawawezi kuangalia mambo bila kuweka miwani ya dini, wakiangalia historia ya ukombozi wa Tanganyika, hawawezi kuona Watanganyika tofauti walikaa na kuunganishwa na uafrika wao, wao wanaona dini za watu. Ndiyo maana kunatokea mvutano huu.
 
JK: Ahsante kwa mchango wako. Hiyo fikra yako nimekutananayo mara nyingi lakini nami nasisitiza kuwa ndani ya nafsi yake ilikuwapo chuki kubwa dhidi ya Waislam na aliifanyia khiyana kubwa historia yao. Kuna kitabu "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru" kilichoandikwa na Dr Harith Ghassany. Nyerere kawekwa vyema uwanjani. Kikitoka usikikose Insha Allah mna mengi yasiyifahamika kwa wengi.
 
FM: Ahsante ndiyo maana nasisitiza kuwa ingekuwa busara sana kama ungelisoma kitabu changu ndiyo uingie katika mjadala. Hayo uloandika nilmeyaeleza katika kitabu. Nakudondoshea kidogo hapa chini nilivyoiona TTACSA:


Tarehe 1 Februari, 1950, makuli walifanya mgomo mkali sana ambapo walipambana vilivyo na askari wa kuzuia fujo. Serikali ilichukulia kuwa migogoro ya mara kwa mara ya makuli ni siasa za vurugu na fujo dhidi ya serikali. Serikali iliwatuma askari wa kuzuia fujo (Kavirondoí kama walivyokuwa wakiitwa na watu wa Pwani) wakakomeshe mgomo. Hawa Kavirondo walikuwa askari toka bara waliojulikana kwa upofu na ukatili wao katika kutekeleza amri za kikoloni. Aghalabu walikuwa, kama kanuni, wakipelekwa kufanya kazi mbali na makwao ili wasipambane na watu wa kwao, endapo itabidi kuamriwa hivyo. Waislam wa mijini katika mapambano dhidi ya utawala wa Waingereza waliwaona Kavirondo kama vibaraka wa wakoloni na watu washenzi. Katika mapigano baina ya Kavirondo na makuli, Kavirondo kumi na tisa waliuawa.

Hali iliporudi kuwa shwari, Hamilton aliwekwa kizuizini nyumbani kwake na kimya kimya aliondolewa na kurudishwa Uingereza. Makuli wengi walikamatwa, wakatupwa rumande na mashitaka ya jinai yalifunguliwa dhidi yao. Serikali ilikuja kutambua kuwa Hamilton, mtaalamu wao wa vyama vya wafanyakazi waliyemleta Tanganyika, alikuwa mwanachama wa chama cha kikomunisiti cha Uingereza (British Communist Party) . Wakati wote alipokuwa akifanya kazi Idara ya Kazi, Hamilton alikuwa mara kwa mara akiwachochea makuli wazushe migogoro pale bandarini. Kama mfuasi kweli wa Marx, alikuwa akiamini kuwa wafanyakazi wastahili washike hatamu za juu za rasilimali. Aliamini kwamba mgogoro ule ungesambaa hadi kwenye sekta nyingine muhimu za uchumi kama ilivyokuwa katika mgomo wa mwaka 1947. Jambo hili linaeleza kwa kiasi fulani kwa nini Abdulwahid alijiuzulu wadhifa wake baada ya miezi sita tu na kwa nini kulikuwa na mabadiliko ya uongozi katika Dockworkers' Union mara tatu katika kipindi cha miaka miwili. Katika mwezi wa Juni, 1950, Dockworkersí Union ilivunjwa kwa amri ya mahakama na shughuli za vyama vya wafanyakazi hazikuibuka tena hadi mwaka 1955 baada ya kuasisiwa kwa TANU.

Harakati za makuli bandarini dhidi ya unyonyaji zilikuwa ndizo kichocheo kwa wafanyakazi wengi waliokuwa wakitumika chini ya hali ngumu za kazi. Mara baada ya mgomo wa mwaka 1947 vyama vitano vya wafanyakazi vilianzishwa: African Cooks, Washermen and House Servantsí Association, African Tailors Association, Morogoro Personal Servants Association na Dar es Salaam African Motor Driversí Association. Alipochukua ukatibu wa TAA mwaka1950 Abdulwahid alitumia uzoefu alioupata Dockworkersí Union kuwahamasisha watu kuingia TAA. Ni uzoefu huo huo wa bandarini ndiyo alioutumia katika kuibadili TAA na kuunda TANU mwaka wa 1954. Mapolu anasema kuwa harakati za vyama vya wafanyakazi vilienda pamoja na harakati za kudai uhuru:

Tanganyika African National Union iliundwa mwaka 1954. Siyo tu viongozi wake waliokuwa wale wale wa harakati za vyama vya wafanyakazi, lakini mara nyingi uongozi wa harakati mbili hizi zilifanana. Kwa hiyo ilikuwa rahisi kwa harakati za kudai uhuru kukita mizizi miongoni mwa wafanyakazi kupitia vyama vya wafanyakazi ambavyo vilikitumika kwa malengo yake ya siasa.

Vyama vilivyoonekana kama kwamba viliundwa kulinda maslahi ya wafanyakazi vilikuweko tangu miaka ya 1930. Serikali ya kikoloni, pamoja na kuanzisha sheria yaTrade Union Ordinance ya mwaka 1932, ilikuwa bado inapinga umoja wowote wa wafanyakazi ulioundwa kudai haki zao. Lakini jambo hili halikuwazuia wafanyakazi wasipiganie haki zao bila ya kujali kitisho cha wakoloni. Hakuna chama au jumuiya iliyoundwa iliyoamsha hamasa ya tabaka la wafanyakazi wa Tanganyika kama harakati zile za makuli wa mji wa Dar es Salaam. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Tanganyika Territory Civil Servants Association (TTCSA) iliyoundwa mwaka 1922 na Martin Kayamba na Chama cha Makuli, katika uongozi na mwelekeo. TTSCA kilikuwa chama halisi cha ustawi wa jamii ambacho hakikuwa na taathira yoyote dhidi ya ukoloni; TTCSA ilikuwa ëkilabu ya makarani na waalimu, ikiwa na magazeti na timu ya kandanda, ikisaidiwa na kuungwa mkono na serikalií. Chama hiki na vingine vya namna hii vilivyoundwa na kuongozwa na wasomi havikufanikiwa chochote.

Kama vile wanahistoria walivyowapuuza waanzilishi wa harakati za kudai uhuru kabla ya mwaka 1954, vivyo hivyo historia rasmi ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika inaanza baada ya mwaka 1955. Iliffe ameuona tena upungufu huu:

Fikra iliyozoeleka ya historia ya vyama vya wafanyakazi Tanzania ni kuwa vyama havikuanzishwa hadi miaka ya 1950. Bwana Tandau anasema kuwa chama cha wafanyakazi kiliundwa na vijana ambao mwaka 1955 waliunda Tanganyika Federation of Labour, ambacho baadaye kilisababisha wafanyakazi kujiunga pamoja. Harakati za vyama vya wafanyakazi Tanzania, zinaonekana kama zinavyoonekana harakati za kudai uhuru - kama kitu kilichoundwa kutoka juu kwa juhudi ya kundi dogo la wanaharakati wasomi.
 
Mkandara: Unaweza ukawa na hoja nzuri lakini ndani pakawa na tusi basi hoja yote inaporomoka. Neno kama "ujinga" halipendezi. Sikuweza kuendelea kukusoma.
 
FM: Cecil Matola nimemtaja katika kitabu changu. Msome hapa chini:


Mwaka wa 1929 Kleist na baadhi ya rafiki zake wa karibu kama Mzee bin Sudi, ambaye wazazi wake walikuwa Wamanyema kutoka Belgian Congo, Ibrahim Hamis - Mnubi ambaye baba yake alitoka Daffur nchini Sudan, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima - Mzaramo, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Rawson Watts na Cecil Matola - Myao kutoka Masasi walianzisha African Association, Kleist akiwa katibu muasisi. Wakati ule Gavana wa Tanganyika alikuwa Sir Donald Cameron ambae alitawala Tanganyika kuanzia mwaka wa 1925 ñ 1929. Cameron alikuwa gavana mliberali na alikuwa akifahamiana na Kleist. Cameron ndiye aliyeanzisha Baraza la Kutunga Sheria la kwanza na mfumo wa Indirect Rule katika Tanganyika. Msimamo wake huu ndiyo hasa uliochangia katika kuwezesha kunzishwa kwa African Association. Lakini juu ya haya yote, chama hiki kiliaswa kisijiingize kabisa katika siasa. Wakati chama hiki kinaanza tayari kulikuwepo na chama cha Wazungu na Waasia. Lakini katika Baraza la Kutunga Sheria Waafrika walikuwa wakiwakilishwa na padri wa Kikatoliki, Father Gibbons, ambae hakuwa hata anaishi na Waafrika bali akikaa Minaki Misheni nje ya Dar es Salaam. Abdulwahid anakumbuka baba yake akimwambia sababu ya kuanzishwa kwa African Association:

Wakati ule vilikuwepo vyama viwili. Kilikuwapo European Association na Indian Association. Vyote viwili vilishugulika na watu wao wenyewe. Lakini Waafrika hawakuwa na chama kama hicho kuwatetea. Katika Baraza la Kutunga Sheria Waafrika waliwakilishwa na mmishionari Mzungu jina lake Father Gibbons, aliyekuwa akifanya kazi Misheni ya Minaki maili kadhaa nje ya Dar es Salaam. Lakini kwa hakika mzungu huyu hakuwa na uhusiano wowote na Waafrika aliokuwa akiwawakilisha. Kwa ajili hii Waafrika walipohisi hawawakilishwi na hawana chama kama kile cha Wazungu na Waasia kutafuta haki zao, walikutana na kuamua kuunda chama chao wenyewe.

Kuanzishwa kwa African Association nje ya utaratibu uliokuwapo wa kuwa na vyama vya kidini na kikabila kilikuwa kitu dhidi ya mfumo uliozoeleka na uliojengeka katika utawala wa kikoloni. Ingawaje chama hicho kilikuwa kinaungwa mkono na Gavana Donald Cameroon na kikasajiliwa kama chama cha ustawi wa jamii, wamishionari waliwatahadharisha Wakristo wasijihusishe na chama: ëmara kwa mara Wakristo walikuwa wakitahadharishwa wasijihusishe na harakati zozote zitakazopingana na serikalií. Katika kuwatadharisha Wakristo wasijihusishe na siasa, wamishionari walikuwa wanayakini labda kutokana na uzoefu wao sehemu nyingine kuwa, vyama kama hivi vya ustawi wa jamii hatimae huwakilisha madai ya watu, hili likitokea basi watu huasi dhidi ya utawala. Bergen ameeleza utata huu unaowakabili Wakristo katika imani yao: ëKatika kufikiri kifalsafa na kiitikadi kwa Waislam ëimanií na ësiasaí ni kitu kimoja, wakati katika Ukristo mambo ya ëkirohoí na ëkiduniaí yametenganishwaí.

Kwa hakika uongozi wa African Association ndiyo ulikuwa hasa mwakilishi wa maslahi ya Waafrika wa Tanganyka, ingawa serikali ya kikoloni ilikuwa haitambui kama Waafrika ni watu ambao wangechukuliwa kuwa wana uwezo wa kushiriki siasa. Wakati ule Waafrika walikuwa wakipigania maslahi mazuri katika kazi kiasi cha vile zile sheria za kazi za kikoloni zilivyoruhusu.

Uongozi wa juu wa African Assocition ulikuwa ndiyo ule ule ulioshika madaraka katika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika. Ushawishi wa uongozi huu wa Waislam katika African Association unaweza kuonekana katika mwaka 1930 wakati African Association na siyo Al Jamitul Islamiyya iliyoandikia serikali ya kikoloni kudai kuchaguliwa kwa Waafrika kama kadhi ili kuhukumu kwa sharia ëÖwakati unakaribia au umesogea karibu kwa serikali hii kufikiria kuchaguliwa kwa Kadhi Mwafrika ambaye anajua sana sheria za Muhammad.
Pendekezo hilo halikukubaliwa na serikali.

Mapema mwaka wa 1930 katika juhudi za kuikiimarisha chama, Kleist akawa anasimamia ujenzi wa jengo la makao makuu ya African Association, New Street (sasa Mtaa wa Lumumba) ambalo wananchi walikuwa wakijenga ofisi yao kwa kujitolea nguvu zao wenyewe. Hili ndilo jengo ambalo TANU ilikuja kuzaliwa tarehe 7 Julai, 1954. Nyumba hii ipo hadi leo ingawa si kama ilivyojengwa hapo hapo mwanzo. Hivi sasa jengo hilo ni katika majengo ya hapo mwanzo makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hivi sasa ni ofisi yake ndogo. Ile nyumba ya zamani ilikuwa imejengwa kwa chokaa, udongo na mawe kama ilivyokuwa desturi ya ujenzi wa wakati ule. Chokaa ndiyo iliyokuwa ikitumika badala ya sementi. Akiwa bado mtoto mdogo, Abdulwahid anakumbuka kumuona baba yake na wenzake wakijenga nyumba hiyo kwa kujitolea siku za Jumapili. Vilevile alimuona baba yake akifanya mikutano na akishughulika na uongozi wa harakati za Kiislam na vyama vya wafanyakazi. Hakuna kiongozi nchini Tanganyika aliyekuwa na bahati ya kupata makuzi yaliyojaa harakati za siasa kumshinda Abdulwahid.
 
Mkandara: Unaweza ukawa na hoja nzuri lakini ndani pakawa na tusi basi hoja yote inaporomoka. Neno kama "ujinga" halipendezi. Sikuweza kuendelea kukusoma.
Mkuu wangu neno Ujinga haliwezi kupendeza kwa yule anayefikiria anajua hali hajui na hataki kujua. Na hili litakuwa neno zuri kwa yule anayejua kuwa hajui ila anataka kujifunza ili apate kujua asoyajua..Na maadam umeacha kunisoma basi nakuweka wewe katika fungu la wale wanafikiria wanajua kumbe hawajui na wala hawatakji kujua. Kwa hali hiyo ndio maana mjadala huu umechukua sura za kinyonga tusiweze kuelimishana.

Lawama zako hazina kichwa mkuu wangu. Utawalaumu Wakoloni kwa kutumia kudidimizwa jumuiya ya Watanzania lakini wewe pia ndio mwepesi wa kumlaumu Nyerere aliyekusomesha wewe toka shule ya msingi hadi chuo Kikuu ukiwa Muislaam na hata kufanya ibada katika shule ilojengwa na Nyerere ikiwa na msikiti ndani. Na hakika usingefika chuo kikuu kama kweli Nyerere alikuwa mbaguzi.. Ulizia sisi watu tulowahi kuishi nchi zenye Ubaguzi. Hiyo Saudia yenyewe wanatubagua sisi pamoja na kuwa Waislaam...

Unapokwenda kwao wanachukua hadi passport yako ya kusafiria na kukufanyisha kazi masaa 30 hadi 36 wasikupe hata muda wa kusali na huna mahala pa kwenda kuomba haki yako. Sana sana utafukuzwa nchini mwao.. acheni wakuu zangu hizi habari za kumlaumu Nyerere hali mimi na wewe tumeweza kusoma na hata tunayaandika haya mawazo yetu hapa pasipo kujihisi minority tena kama tulivyokuwa wakati wa mkoloni.

Hatushindani kwa hoja hapa hata kidogo isipokuwa kuzungumza ukweli ambao wewe na mimi tumeishi ktk mazingira ambayo hayakuwa na ubaguzi kiutawala isipokuwa leo hii Tanzania imekuwa na Ubaguzi ambao naweza kabisa kuuzungumzia kuliko wakati wowote ule. Hata ukisoma tu hapa JF utazikuta mada zinazoonyesha chuki na hasira za Udini ambazo hazikuwepo wakati wa Nyerere. Na hakika kwa mitazamo nayoiona hapa JF Nyerere alikuwa na kila haki ya kupiga vita watu wenye imani potovu kama wavyoona hapa JF ktk maswala ya dini.

Mkuu naweza kabisa kuwa extreme ktk Uislaam hasa pale mtu anapojaribu kuupaka Uislaam kwa kutumia matamanio yake kujenga hoja ya Udini.. Na hakika wewe mwenyewe unajua fika kwamba wakati wa Nyerere hata mihadhara ilokuwa ikifanyika Mnazimmoja na kina Ngariba na Mwirima ilikuwa na nguvu kubwa sana kiasi kwamba watu wengi waliweza kusilimu dini kuingia Uislaam kuliko wakati wowote wa historia ya nchi yetu. Tena basi Nyerere ndiye alikuwa na ushirikiano mkubwa na nchi za kiislaam kama Iraq, Libya, Iran na Misri wakati wa Nassar kuvunja hata Uhusiano na Israel kuliko leo hii mnapokumbatia Ukabaila kiasi kwamba mnanyenyekea mabwana (masters) wenu..

Mkuu acheni Unafik hii Ramadhan, kama kweli unataka kuandika Historia ya TANU vizuri fanya kama ulivyoagizwa na wengi hapa kijiweni. Nenda kawahoji woote waliohusika Waislaam kwa Wakristu na kutaja michango yao maanake historia ya tanzania haiwezi kuwa kamili kama utawaaacha Dr Vedasto Kyaruzi, MaChief Marealle, Mkwawa,Shangali, Lugusha, Wahindi pia kina karimjee na Vinran. Dr Mwanjisi, Mutahangarwa, stephen Mhando na wengine wengi ambao hakika hatujui michango yao kama Watanzania na wazalendo na sii kwa rangi au imani zao za dini..Hiyo title ya Kitabu chako tu inatosha kuzungumza mengi hasi yasiyokuwa na Uzalendo bali Udini.

Mkuu nimemaliza na wala sintaendelea kubishana na kujaribu kuandika kitu maadam wewe unaamini unayoandika ndio Ukweli mtupu. Na hakika imeniudhi zaidi kukusoma kwamba Kleist kukataa jitihada za baba yake na ndugu yake haikuhusiana na Uislaam ni kwa sababu ya siasa kama vile anajipendekeza kwa utawala uliopo. yaani maadam amekataa kukubaliana na dhana yako basi yeye ni mnafik.
 
Ishu si kutafuta uhuru wa waislamu au wakristo ndio maana akina bibi Titi walimkubali Nyerere wengine walipokuwa na mashaka nae ishu ni kwa nini historia iliyoandikwa na wanayofundishwa watoto haisemi ukweli juu ya jambo hili? Maana tunajua mawakala moja ya mawakala wa ukolono ni dini na pia tuambiwe basi hata katika kupigania uhuru dini pia ilitumika na ielezwe mchango wake maana inavyoonekana kuna kama vile kuna kundi fulani lilikuwa la wajinga na walikaa pembeni hawajui la kufanya, hawakupata elimu ndio maana mpaka leo wako nyuma na kundi lingine wao ndio walikuwa msitari wa mbele na wao ndio walikuwa wengi serikalini wakafanya ufisadi na kujiimarisha mpka leo familia zao zipo katika werevu na wengina awle katika ujinga. Tuichukulie mada kwa kuangalia taswira iliyipo na si kuwa fanatics

quote hiyo hapo ju inajibiwa vizuri na quote hii hapa chini..........

Mbona sijawahi kusoma mahali kokote kuwa uhuru wa nchi hii uliletwa na wakristo? Ama mbona sijawahi kusoma kokote kuwa waislamu hawakua na mchango wowote katika uhuru wa nchi hii? Ama katika wote waliotajwa, mbona sijawahi kusoma maamndiko yeyote yakisema hawakuwa na mchango wowote? Mbona hatusemi labda uhuru wa nchi umepiganiwa na watu wengi ila Nyerere ndo anaonekana kinara peke yake na badala yake tunaingiza hoja ya waislamu na mchango wao kwa uhuru? Kuna ajenda gani ya siri hapa? Acheni hizo bwana!
 
Kwa hakika naelewa hamaki za wengi hasa wasiokuwa Waislam wanaposoma kitabu changu The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Utold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press 1998, London. Naelewa shida wapatayo halikadhalika wasomapo makala zangu tofauti ninazojitahidi kueleza yale ambayo kwa hakika yamekosewa aidha kwa makusudi au kwa kutokujua kuhusu historia ya TANU.

Naelewa simanzi wanayopata Waislam wanaponisikia katika mihadhara na mazungumzo ya kawaida ninapowaenzi mashujaa wa uhuru wengi wao wakiwa Waislam ambao kwa hila wamefutwa katika vitabu na kumbukumbu za taifa letu.

Ukiachia mbali hayo mjadala huu ungekuwa na maana sana endapo wanaoamua kuzungumza suala hili wangejikita katika mada badala ya kuchanganya mada. Katika kufanya hivyo wangeweza kuhoji yake ambayo wanadhani ni uongo. Hii ingenipa mie nafasi ya kujibu na kusema kile ninachokijua.

Ama kuhusu Mwalimu Nyerere hapana hata mahali ambapo nimemvunjia heshima na wala siwezi kukosa adabu kiasi hicho ila ninalosema ni kuwa kuhusu TANU chama hicho hakuanzisha yeye na nimeeleza kwa kirefu sana jinsi chama kilivyoanza, kuchipua kwake hadi kuwa chama chenye nguvu kabisa. Kama kuna mtu anaona vibaya kwa kuelezwa ukweli huu ni bahati mbaya sana.

Ama kuhusu mambo ya elimu, kuwapo kwa Waislam Tanganyika na wingi wao, Bakwata nk. majibu Alhamdulilah yapo na kama itabidi nitayaeleza Insha Allah.


wamefutwa kutoka kwenye vitabu vipi hivyo?............
 
Ogah: Inaelekea umeingia katikati katika mjadala huu kwa hiyo mengi yamekupita. Fanya rejea nyuma. Kitabu "Historia ya TANU 1954 - 1977" hii ndiyo historia rasmi ya TANU kimewafuta mashujaa wa uhuru wa Tanganyika, kitabu cha Edward Barongo, "Mikiki Mikiki ya Siasa Tanzania" kimewafuta, Kimambo katika kitabu chake (jina sikumbuki) kawafuta, Abubakar Olotu "Historia ya TANU" halikadhalika. Soma vitabu hivyo utaona ukweli huu.
 
Mkandara: Ahsante kwa mchango wako hapana haja ya kujitoa na tuendelee na mjadala. Kama tumekwaruzana kidogo ni ubinadamu tu lakini naamini mimi na wewe heshima zetu bado ziko pale pale. Nataka nimzungumzie Kleist kwa kuwa naona kauli yake imepewa uzito kutokana na mahojiano yake na Gunze wa Radio Butiama. Bahati mbaya mimi Kleist ni ndugu yangu na ni mmoja wa watu ambao walionitia hima sana kufanya utafiti na kuandika historia ya waasisi wa TANU na historia ya babu na baba yake katika maendeleo ya siasa Tanganyika ya kikoloni kuanzia 1920s hadi 1950s. Kutokana na uhusiano huu mimi nina mengi nijuayo ambayo mtu mwingine hawezi kuyafahamu. Mathalan kulikuwako na ugomvi baina ya Nyerere na Ally Sykes kuhusu nyaraka za TANU. Nyerere alizitaka na Ally Sykes akakataa kuzitoa akidai kuwa hizo nyaraka lau kama ni historia ya Tanganyika lakini na mali ya ukoo wake. Hili ni moja. Ama kwa Kleist kuwa mnafiki hapana yeye anajua mengi sana na Kleist ni mtu wa tahadhari sana. Ngoja nikupe mfano mwingine. Kleist ana shajara (dairy) za baba yake za miaka ya 1950 ambazo alikuwa ameziandika katika hati mkato (short hand). Hizi shajara inasemekana zina siri na mambo mengi sana kuhusu juhudi zake za kuanzisha TANU na mikutano yake ya siri na akina Kenyatta Nairobi. Halikadhalika inasemekana ina hotuba za mwanzo za Nyerere ambazo alikuwa akizitoa pale Mnazi Mmoja miaka ya mwanzo ya TANU 1954/55. Kleist kakataa kabisa ku-transcribe hizi shajara na kagoma kabisa kuzitoa kwa mtafiti yoyote kuzisoma. Hivi karibuni Kleist kaona DVD niliyozungumza Msikiti wa wa Mtambani Ramadhani ya mwaka jana na mwanzo wa mazungumzo yangu nilihadithia kisa chetu mimi na Klest na Shariff Attas (mmoja wa babu zake Kleist) na jinsi Nyerere alivyomsahau Shariff Attas siku alipokutananae ofisi ya TANU juu ya kuwa walikuwa watu wa karibu sana wakati wa kuijenga TANU. Shariff Attas kwa zile adabu na misimamo ya kiungwana na yeye akamwambia Nyerere kuwa asiwe na wasiwasi wao hawakupata kujuana hata siku moja. Kleist alipomaliza kuangalia ile DVD akanipigia simu na kukiri kuwa DVD yangu imemliza.
 
Kutofautiana kuhusu kitu gani ni mali ya umma na kipi binafsi ni kitu cha kawaida. Mtu kukataa kuweka wazi diaries za mzazi wake inaeleweka. Wewe unahakika gani kuwa humo ndani kuna mambo yanayomhusu Nyerere peke yake? Diary ni personal na mara nyingi tunaandika mawazo yetu ya ndani na si yote yanayopendeza. Wangapi tunalizwa tunapokumbushwa kuhusu waliotutangulia? Mara ngapi tunawasahau wale tuliokuwa karibu nao hapo zamani? Ni kitu cha kawaida tu. Wewe kama kawaida, unataka kugeuza kichuguu kiwe mlima.

Amandla....
 
Mohamed Said,
Mkuu wangu hata sielewi unachotarajia kupata hapa. labda nikujibu wewe kwa kila hoja unayoanzisha ili tupate kuwa mstari mmoja maanake kila nayoandika toka nimeingia hapa hujanijibu hata moja isipokuwa kuchagua yale yaliyokuwa mepesi kwao kuyajibu.

Sasa ikiwa kweli Kleist anayo diary ya Baba yake ambayo amekataa kuitoa kwa mtu yeyote kiasi kwamba imebakia kuwa - INASEMEKANA, huoni kama yote uyasemayo ni udhanifu wa hoja yako mwenyewe kwani Kleist hajakwambia kilcihoandikwa!. Pili kama Kleist kafikia kukataa ku transcribe hizo nyaraka wala kufanyiwa Utafiti imekuwaje wewe upate habari kuwa zina mikutano ya siri ktk juhudi zake za kuanzisha TANU hali chama hicho kilianzishwa mwaka 1954 wakati Kenyatta akiwa jela toka mwaka 1952 na akatumika kifungo cha miaka saba 'til 1959. Ni wakati gani unapowaweka Abdul Wahid na Kenyatta meza moja na kwa maswala yapi muhimu kwetu?

Na kibaya zaidi ni kwamba umeshindwa kutuambia ni kitu gani walichokuwa wakijadiliana baina ya Abdul Wahid na Kenyatta hadi iwe siri kubwa na ya ukoo wa Skyes hali tunazungumzia nyaraka za chama na sii za maisha ya AbdulWahid na siri zake ambazo aliziweka ktk diary zisiwe mali ya Taifa ila yake binafsi.

Mkuu wangu nachojaribu kukuambia hapa ni kwamba yaliyokwisha tokea yametokea, unataka kuandika Historia ya Tanzania andika kama ni historia ya Tanzania lakini haya ya mchango wa Waislaam hali kila mtu anajua fika kwamba wapo wananchi wenye imani ya kiislaam walichangia sana Uhuru wetu ni kutaka kuonyesha tofauti baina ya dini hizi mbili. Ndio matatizo yanayowapata Kenya ambako Kenyatta amesifiwa sana hali wapo waasisi wa chama hicho kina Joseph Kang'ethe ambaye nina hakika Wakenya wengi hawamjui.

Na haikuwa swala la Ukabila isipokuwa Kenyatta ambaye muda mwingi wa harakati za Uhuru alikuwa jela ndiye akaja lamba dume na huyo tukamwona akiushamirisha Ukabila Kenya bila kificho. Sifa zote kapewa Kenyatta, na hata ukienda Zambia kwa Kaunda, South Africa kwa Mandela yaani kote historia ya nchi hizi imeandikwa na mwaandishi wetu waliochukua tu yale waliyoyaona mazuri kwao na kuyaandika wengine wakifikiria uandishi ni fedha hivyo waliweka chunvi za uuzaji.

Kasome historia ya Marekani, Canada au Uingereza kote utakuta wapo watu wengi sana wameachwa na sii kwa sababu ya dini. jinsia au rangi zao isipokuwa pengine michango yao haikuwa interest ya mwandishi ambaye somo kubwa kwake lilikuwa mhusika fulani na harakati za Uhuru wa nchi hiyo. Na kwa ujumla wa nchi ziku zote huwa haikusanyi kila mtu hata kidogo zaidi ya Utaifa wa wahusika ndani chombo chao kimoja yaani Chama. Hivyo ni historia ya chama ndiyo huvuta majina ya wahusika ktk kila tendo walofanya kukijenga chama au harakati zenyewe.

Nakuhakikishia kwamba hakuna mtu hapa JF wala Tanzania ambaye anasema Kina Sykes hawakuwa na mchango mkubwa ktk Uhuru wetu..Hawa watakuwa wendawazimu lakini haitokani na Uislaam wao ndio ulowasukuma kuunda chama kuutafuta Uhuru wa nchi yetu isipokuwa ni Uzalendo wao kwa nchi hii. Yawezekana pia wao walikuwa na mwamko wa harakati za Uhuru kabla ya Watanzania wengi kwani ukitazama list kubwa ya viongozi wa chama TANU waliokuwa juu ni wahamiaji zaidi ya makabila ya wazawa. Sasa hatuwezi kusema au kuandika Historia ya Tanzania kwa kuanza na mchango wa wahamiaji ktk Uhuru wa Tanzania iwe ndio historia inayokubalika hali wapo wazawa wengi tu pia walishiriki ktk kuundwa kwa harakati hizo.

We all played our part, dini makabila na hata race tofauti zilishiriki kwa njia moja ama nyingine na kwa vile sifa za ushindi wa Vita humfuata Jenerali sioni ubaya wowote Nyerere akibebeshwa joho la Baba wa Taifa kwa sababu tu askari wengi walikuwa mstari wa mbele wakipigana vita hiyo. Ila kama kweli wataka kuandika Biography ya AbdulWakil nadhani watu uliowafuata walikuwa tosha kabisa ya kukupa hadithi za maisha yake hata pasipo kuzipata zile nyaraka za siri. Unapozungumzia mchango wa Waislaam ktk Uhuru wa Tanzania ni kuanzisha tabaka za kimtazamo ktk harakati hizo kama wanavyodai Wakikuyu huko Kenya au kesho Wazuru waanzishe vagi la kusema ni wao waliokuwa wameanza harakati za Uhuru kabla ya kina Mandela na kabila la Nkosa..Na hapo ndipo vurugu itakapo anzia.

Ni muhimu sana kwako kuelewa kwamba leo hii tuna matatizo chungu nzima, iwe Waislaam au Watanzania na hakika utakuwa umewasaidia sana Watanzania kama utaweza kuandika habari zinazohusiana na dhulma inayofanyika leo hii. Na kama ni historia ni vizuri sana ukiandika watu wote wenye mchango mkubwa ktk harakati hizo badala ya kutumia majina yao na dini zao kama ndio mchango.

Kwa mfano Ukimzungumzia Mwapachu andika mchango wake, John Rupia, Dosa, Thomas Plantan na Kyaruzi ambao pia walikuwa muhimu sana sijawasoma wakiandikwa michango yao hali aalikuwa watu muhimu sana ndani ya chama. Ila kila naposoma ni jinsi gani hawa watu walimwezesha Nyerere kufikia pale alipofikia. It's all about Adaku, yaani kama vile mtu anakupa fadhila kisha inakuwa hadithi dunia nzima wajue umemsaidia vipi. Kama sii mimi huyu mtu asingekuwa chochote!...

Aaaah mkuu wangu huu Uislaam kweli au ni unafiki mtupu usiofaa ndani ya Uislaam. Ati Nyerere alimsahau Sharrif Attas ndio kimlize Kleist kana kwamba watu hawa sahauliani..Mimi kila naporudi Nyumbani hukutana na watu niliwasahau na wao hunikumbusha na isiwe jambo la kutoka machozi wala sababu kubwa ya kushangaa hata kama tulikuwa pamoja miaka ya nyuma. Sasa unapoona watu kama Kleist wanapoitazama DVD yako na kulia machozi kisha ukashindwa kutueleza kilichomliza hapo ndipo tunaposhindwa kuchukua mahitimisho yako. Nasema hivi kwa sababu hata mimi husimuliwa mambo ya marehemu baba yangu na hutokwa na machozi aidha kwa furaha ya kile alichoweza ku accomplish ama pasipo sababu maadam anayezungumziwa ni mzazi wangu..

Mkuu nimemaliza na sijui kama umeweza kuona upande wetu tunaitazama picha hii vipi kama wasomaji. Na hakuna kitu kibaya kwa mwandishi yeyote ambaye anataka kubishana na customers wake akifikiria yeye anajua zaidi yao. Sisi ndio wanunuzi na wapenzi wa historia ya nchi yetu na tuna haki ya kukwambia makosa yako kama mwandishi. Ukiweza kuwasikiliza wateja na ukaweza kuandika Historia ya Tanzania ikiwa na Mtazamo wa Uzalendo kwa nchi yetu utapata sifa na mauzo bora zaidi ya kutumia dini za wahusika kwa sababu HAIHUSU!.
 
Wakuu tunapoongelea suala la uhuru wa Tanganyika na TANU, mbona hatuzungumzii swala la ubaguzi lililokuwepo hata katika madhehebu tofauti ya kiislamu?
Ni ukweli kuwa mwafrika alikuwa 3rd class citizen katika Tanganyika na si waislamu wote walikuwa na umoja kama wengi tunavyoambiwa.
Misikiti kama ya Manyema ina historia yake kama misikiti ya watu wa bara, waislamu.
Kuna misikiti ambayo hata leo waislamu hawaingii.
Mizizi ya ubaguzi huu hadi leo ipo.
Sasa leo mwananchi wa Tanzania anapochukea a leaf, ukurasa mmoja tu katika historia ya Tanganyika na kuifanya ndio utetezi wake kwa waislamu wote, hapo napata wasi wasi wa hatima ya Tanzania na umoja wake.
 
Wakuu tunapoongelea suala la uhuru wa Tanganyika na TANU, mbona hatuzungumzii swala la ubaguzi lililokuwepo hata katika madhehebu tofauti ya kiislamu?
Ni ukweli kuwa mwafrika alikuwa 3rd class citizen katika Tanganyika na si waislamu wote walikuwa na umoja kama wengi tunavyoambiwa.
Misikiti kama ya Manyema ina historia yake kama misikiti ya watu wa bara, waislamu.
Kuna misikiti ambayo hata leo waislamu hawaingii.
Mizizi ya ubaguzi huu hadi leo ipo.
Sasa leo mwananchi wa Tanzania anapochukea a leaf, ukurasa mmoja tu katika historia ya Tanganyika na kuifanya ndio utetezi wake kwa waislamu wote, hapo napata wasi wasi wa hatima ya Tanzania na umoja wake.

Kweli bana...mimi sijawahi kuona Bohora mweusi....wote weupe na shurti ufuge ndevu kwa sayle ya ainayao tuu.....:focus:
 
Kutokana na hii mada kuwa moto, ilibidi nifanye kautafiti kidogo ili niweze kuelewa zaidi juu ya TANU na Uislamu kabla ya uhuru.
Mohammed Said anadai kuwa waislamu walikuwa marginalised baada ya uhuru.
Na kwamba hawa kuhusishwa katika matunda ya uhuru.
Ukweli ni kwamba hizi tofauti pamoja na kuwa zipo sasa , zilikuwepo hata kabla ya uhuru.
Kuna vikundi vya kislamu vilivyo dai kuwa aheri Tanganyika isipate uhuru wakati huo hadi na wao watakapo fika kuwa at par!!!
Mambo ya ajabu sana haya.
Nitanukuu utafiti uliofanywa na Dr Amos Mhina , Political Scientist ,UDSM katika paper yake:

Paper: Religions and Challenges of Development in Tanzania; Firefighters and Arsonists.
By: Dr. Amos Mhina, Associate Professor, Department of Political Science and Public Administration, University of Dar Es Salaam, Tanzania/ Visiting Scholar, Carleton University, Ottawa.​


Some Muslim groups were in a collision course with the coming nationalist government even before independence. As TANU and Nyerere were on course to independence in the late 1950s many Muslims supported the nationalist movement. There were however some conservative coastal Muslims who opposed TANU. According to Illife the most serious dissent came from the All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT) mostly based in Dar Es Salaam. In August 1959 its leaders went to the extent of proposing that Independence be delayed until Muslims achieved educational equality with Christians. (Illife 1979 pp.551-52). The nationalist party was able to calm moderate Muslims by promising to deal with the disparity after Independence.

Agitation started again after independence under the auspices of the East African Muslim Welfare Society (EAMWS). The EAMWS was banned by the government in 1968. the events which culminated into that ban are reflective of State-Muslim relations as well as intra-Muslim conflict and the divergent views of different sections of Muslims on how to engage the government. Different Muslim groups sought to wrest the power to control EAMWS from Asian Ismaili Muslims. It was difficult to do so because it the latter provided the funds for the organization. Up to 1968 the strategic posts of Secretary General and Education Secretary General were both held by Aziz Khaki an Ismaili. (Tambila 2006b. p. 181).

Sasa hiki kimbembe cha Ndugu yetu Mohammed Said bado ni mwendelezo ya yaleyale yaliyoonekana hata kabla ya uhuru!
Tupende tusipende wenzetu wana hulka ya kupendelea shari badala ya maendeleo.Sifanyi hivi kama uchokozi hapana lakini inabidi pawepo na mabadiliko ya kifikra ili wenzetu waweze kufaidika na fursa zilizopo za maendeleo.​
 
Gole Gwasika,
Sasa hiki kimbembe cha Ndugu yetu Mohammed Said bado ni mwendelezo ya yaleyale yaliyoonekana hata kabla ya uhuru!
Tupende tusipende wenzetu wana hulka ya kupendelea shari badala ya maendeleo.Sifanyi hivi kama uchokozi hapana lakini inabidi pawepo na mabadiliko ya kifikra ili wenzetu waweze kufaidika na fursa zilizopo za maendeleo.​
Mkuu hapa ndipo nisipokuwbaliana na wewe na watu kama wewe ndio Mohamed Said anawafananisha na Nyerere - Utanisamehe pia.

Ni lazima kwanza usome habari kisha fanya utafiti kujua kilichotokea na sio ku copy na ku paste hali hujui historia ya nchi. Kupingana na TANU wakati wowote au chama chochote haina maana unatokana na ubishi wa Waislaam bali ndio demokrasia ya kweli mtu kuchagua viongozi wako, kukubaliana na malengo ya chama na hata kuweza kuweka Upinzani kwani hakuna binadamu aliye kamili.

Sasa kama wewe unaamini wapo Miungu Watu ambao wanatakiwa kufuatwa tu kama sisi ni kondoo, hii haiwezi kuwa hoja kwa waumini wengine ambao wanaamini hakuna tena kondoo ila sote ni Umma mmoja.

Na Imani yako wewe haiwezi kuwa sifa kwa waumini wengine, la muhimu kwako amini unachoamini wewe kwa tafsiri yako na kaa pembeni kunywa maji ukisikia kiu. Hii habari ya WAO hivi na SISI ni hivi kisha unadai watu kupendana ndio Unafiki huu mkuu wangu. Na hakuna msikiti ambao Muislaam anakatazwa kuingia - HAKUNA kitu hiyo..samahani tena.
 
Huyu Mohamedi Said anazungumzia maoni yake na wala siyo fact. Historia gani anayoijua mtu mmoja tu? where is the documentation?
Kiumri anaonekana alikuwa mtoto mdogo sana mengi anayosimulia yalipotokea au hakuwepo kabisa duniani.. Ni yaleyale mambo yetu ya hadithi za kuhadithiwa na wazee wakati wakiota moto kumbe na hao wazee nao walikuwa wakitoa opinion zao. Kama anazungumza ukweli atoe ushahidi wa hayo mambo sio kutunga vitabu tuu kwa stori za kubuni ili zimtoe. Njaa mbaya sana. Kama ni historia historia ya nchi hii wanayo wakoloni kwani wao walikuwa wanafanya documentation wakati huo na wala sio waswahili ambao hawakuwa na utaratibu wa kuandika mambo yanayojili. Eti leo ndio unatunga kitabu cha historia ... yaani muda wote huo ulikuwa umelala tuu leo ndio unaona kuna haja hiyo? Hekaya za Abunuwasi zimerudi tena...!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom