Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
LG: Ahsante kwa mchango wako. Nia ya kuandika kitabu kile ni kuiweka sawa historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika kuwa Waislam ndiyo waliotoa mchango mkubwa hili sikulitaka mimi. Labda swali liwe kwa nini Waislam walilkuwa mbele katika kuupiga vita ukoloni? Msitishike na ukweli huu. Nachoshukuru ni kuwa waliokuwa hawatuelewi leo hii wanatuelewa. Vyuo vyote vinavyosomesha "African History" na "Islam and Politics" kitabu hiki ni mashuhuri na baadhi ya walimu wa vyuo hivyo ni marafiki zangu wakubwa na urafiki umekuja kwa sababu nimechangia katika dunia ya usomi, kitabu cha maana ambacho kimeongeza elimu. Jonathan Glassman, James Brenan, Brenan Mcsherry, Prof. Ali Mazrui ni watu ambao nisingewajua kama si kwa kitabu hicho. Hawa hawakupata kunikejeli wala kunizomea. Kwao wao nimepokea heshima, na mialiko. Ajabu naiona kwenu kila mkisoma hoja zangu hamaki zinapanda. Nimelipeleka hili jambo kwa mmoja wa maprofessa wa pyschology kutaka kujua ni nini hasa kinasababisha hali hii yenu na nimemuuliza kwa nini mimi sikasiriki kama hawa wenzangu. Kaniomba nimpelekee majibu yenu na hoja zangu. Nimefanya hivyo na sasa nasubiri jibu lake.
 

....kusema kwamba walimu wako WAKO WRONG haimaanishi MATUSI..........ni mtizamo.........ungejituliza wewe na kufanya FIKRA ungejua jinsi gani ya kujibu mtizamo wangu.........sasa kwa kuwa wewe umeachia moyo wako kutawala na kuondoa nafasi ya kichwa chako..................ndio kunasababisha kutukana MATUSI HAPO JUU...............

Walimu wetu..........both kwenye elimu dunia na elimu ya dini..........wanakuwa challenged................wao sio MWISHO WA FIKRA (na wao hukosea).............watu wanachallenge na hata kujibu AYA na JUMBE za vitabu depending on the facts............na huwezi kum-ignore mtu anayekuchallenge kwa facts eti kwakuwa hajakujibu kwa kutumia kitabu kama ulivyoandika wewe..........again hao WALIMU ARE WRONG.........kukuambia KITABU HUJIBIWA KWA KITABU..............

Kitabu chako cha kurasa say 200....chaweza kuwa na facts 10 (tena kumi ni nyingi) tu.........nyingine ni strories tu (kama kukunja miguu nyumba numba 36).......na si lazima kujibu facts 10 kwa kurasa 200!........wengine sio ma-story tellers.............
 
Ogah: Nakushukuru kwa mchango wako na nathamini sana juhudi zako. Tuendelee kujadiliana.
 
Safari: Ahsante kwa mchango wako. Nakuwekea kipande hiki kutoka kitabu changu kinachohusu Yanga na Sunderland ya miaka ya 1950. Soma kisha nipe fikra zako:

Baada ya vyama hivyo vya wanawake kuingizwa katika TANU ndipo iliamuliwa kuwa vilabu viwili maarufu vya mpira na vilivyokuwa na ushindani mkubwa mjini Dar es Salaam, Young Africans na Sunderland navyo vijumuishwe katika kuiunga mkono TANU. Young Africans ilikuwa kilabu isiyo na wafuasi wenye elimu sana. Wengi wa wanachama na mashabiki wake walikuwa watu wa kawaida kutoka mitaa ya Dar es Salaam. Yanga kama ilivyokuwa ikijulikana ilichukua wachezaji wake mashuhuri kutoka vijana waliozaliwa na kulelewa mjini Dar es Salaam na pembezoni mwake. Vijana waliokua na kucheza mpira pamoja katika viwanja vya tifutifu katika mitaa ya Kariakoo. Kandanda ndiyo iliwafanya watu wa Tanganyika na Zanzibar wakutane. Kulikuwa na uhusiano baina ya Yanga na chama cha African Association huko Zanzibar tangu miaka ya 1930. Wengi wa viongozi wa African Association walikuwa washabiki wa mpira na wengi wa viongozi wa Yanga walikuwa wapenzi wa taarabu na Zanzibar ndiyo walikuwa mabingwa wa muziki huo. Haya ndiyo mambo yaliyowakutanisha wananchi wa pande mbili hizi pamoja na mwamko wa siasa. Kama TANU, rangi za Yanga ilikuwa kijani na nyeusi. Mwaka 1954 TANU ilipopandisha bendera yake ya kijani na nyeusi mtu wa kawaida hakuwa na khiyari ila kuifunganisha TANU na Yanga. Kwa hiyo, kuwa mwanachama wa Yanga au shabiki wake kuwa mwananchama wa Yanga ilikuwa sawasawa na kuwa mwanachama wa TANU. Inaaminika kwamba ilikuwa wakati wa uongozi wa Mohamed Sultan kama rais wa Yanga ndipo Mohamed Sultan alimtambulisha Nyerere kwa Karume, Rais wa Afro-Shiraz Party ndani ya kilabu ya Yanga Mtaa wa Mafia na Sukuma, Kariakoo.
 
FM: Uchochezi si moja ya sifa zangu.
.......... ilikuwa wazi kuwa Pacha, kama Mkristo na kabila yake Mlulwa kutoka Mpanda, hawezi kukubalika na Wamanyema wa Tabora. Wamanyema walikuwa wanajulikana kwa tabia yao ya ukaidi.
Need we explain more?
I suppose I rest my case
 

BTW........Uzuri wa Walimu angalia products zao.............however products zilizozalishwa na product zao zaweza ku-deceive umma..........kwa kuamini uzuri wa Walimu hao.........my point is naheshimu sana mchango wa Walimu notwithstanding............
 
labda niwe tofauti kidogo katika kuchangia kwa kuuliza swali, kusema ni waislam ndio waliopigania uhuru na si nyerere kwa mfano unataka ku achieve nini regardless hoja yako ni kweli au si kweli? pili, sijui kama hata ushawai ku gogolise kujua sababu kubwa iliyowafanya waingereza watupe uhuru bila kumwaga damu, ni hoja za nyerere kwenye majukwaa ya kimataifa hadi akaonekana ni mtu anaweza ondoka, kuongoza mapambano ya uhuru wakati tungekua tunaonekana ni ma mbumbumbu sidhan kama huo uhuru tungeupata mkuu! kua na hoja jenga hasa ktk jamii kwani unakua kama unataka kuonyesha waislam wameonewa na wanaendelea kuonewa nchi hii bila sababu! unazungumzia vitu vilivyovunjwa vya waislam mbona huzungumzii mali za kanisa zilivyotaifishwa na zingine kulazimishwa kuwahudumia wananchi wote kiujumla bila kujali itikadi zao baada ya azimio la arusha! sera ya nchi ilikua ni kujenga mfumo usioruhusu dini kuingilia mifumo ambayo itawagawa watu kama nchi changa tulitaka umoja, je tunakoelekea sasa unakupenda, watu wanajali udini zaidi ktk siasa, michezo, ajira na karibu kila nyanja ya uchumi?
 

Mohamed Said,

..hapa umenichanganya kwelikweli.

..pamoja na kuelewa saikolojia ya wale wanaokupinga ungetafuta ushauri ili kuelewa saikolojia yako binafsi.

..hakikisha huyo mtaalamu wa psychology yuko independent, ili kupata ushauri wa uhakika na wenye msaada kwako.

..ktk video clip kuna mahali umejitambulisha kama Mmanyema, na zaidi ukadai hujawahi kukutana na Mkristo ktk kabila la Wamanyema. mimi kauli ile, na maneno mengine ya kuwazungumzia Wakristo kama "hawa," inanipa mashaka kama unaweza kuyaangalia masuala ya mahusiano kati ya dini hizi mbili with an "independent and unbiased" view.

..maadam umelileta mwenyewe suala la PSYCHOLOGIST, kwa heshima na taadhima, nashauri upeleke hizi video clips zako zikaangaliwe na wataalam na kupata maoni yao.
 
'

Tatizo si unachokiandika bali hizo hitimisho zako. Unamlaume Nyerere kwa kuwatenga waislamu lakini kila ulichoandika ni kuwa waislamu ndio waliowatenga wakristu wakina Pacha na Nyerere! Pamoja na Tabora kuwa na waislamu wengi, lakini bado tunaona mmisheni alikuwemo kwenye juhudi za kugombea uhuru! Hii yote inathibitisha msimamo wetu kuwa uhuru uliletwa kwa juhudi za kushirikiana wakristu na waislamu. Si waislamu peke yao kama unavyotaka kupindisha! Kwangu mimi huo ni uchochezi.

Amandla..........
 
duh huu mjadala unapoelekea sijui.

ila nnajua kwa haraka hakuna kitu ambacho kizito kukijadili kwa amani hadi mwisho kama masuali ya dini.

sasa tujadiliane bila ya kupambana kwa ngumi
 
Mtu wa Pwani: Ahsante kwa kuingia katika mjadala. Usiwe na hofu na mimi mie si mgomvi najibu hoja jwa hoja yenye mantiki wala sithubutu kutumia lugha isiyo ya kiungwana. Waamerika wana msemo: It takes two to Tango.
 
FM: Hakika umesema kweli. Nimekuwekea hiyo ili uone mambo yalivyokuwa wakati ule. Wabague uwatawale.
 
JK: Ahsante kwa ushauri. Huyu professor keshanipitia na moja katika taarifa yake alinambia: "You are a man of exceptional courage." Yapo mengi alisema kuhusu mimi na hadi leo namshukuru mtu aliyenijulisha kwake na mimi nimejitahidi sana kuwaeleza marafiki zangu kuhusu mtaalam huyu. Baadhi ya mabadilishano yetu yeye ametumia katika kusomesha. Hivi sasa anaandika kitabu ambacho Tanzania na woga wa viongozi wetu kuogopa vivuli utaelezwa. Yako mengi kanieleza kuhusu tabia yangu mazuri na mabaya. Insha Allah ikitokea nafasi ntakujuvya.
 
Mkuu hata hii story yako nashindwa kukubaliana nayo kwa sababu navyojua mimi Marehemu Sheikh Abeid Karume na African Sports ya Zanzibar ndio waanzilishi wa club ya Yanga ya Dar Es Salaam na ile Africa Sports ya Tanga zikiwa kama ni matawi la African Sports ya Zanzibar. Hii ilitokana na kuwa mzee yule (Baharia) baada ya kurudi Unguja alijiunga na wenzake kuunda team ya mpira kwa sababu jumuiya za kisiasa zilikuwa ni marufuku.

Nakuomba fanya utafiti kwa wana Yanga wenyewe utakuta historia hii na kama sikosei nilipokuwa Tanzania kabla sijaondoka (mwezi April) Yanga walimuenzi Marehemu Karume akahudhulia mkewe ktk maandimisho hayo, na nilimwona mke wa marehemu Abeid Karume akihutubia mkutano uloandaliwa na Yanga (on TV). Katika hotuba yake alisema wazi na kuwakumbusha wanachama mchango wa marehemu ktk Ujenzi wa team hiyo na akimalizia kwamba Karume was Assassinated na akiomba historia kamili ya kuawa kwake iandikwe na wahusika watajwe pasipo kuficha. Kwa hiyo sioni kabisa mahusiano ya Yanga na TANU hapa unatuongezea tu kwa sababu rangi zao zinafanana na ni ktk dhana hiyo hiyo unatumia kumlaumu Nyerere kwa sababu ni rangi ya Yanga, sii rangi ya Simba.
 
Originally Posted by Mohamed Said

FM: Uchochezi si moja ya sifa zangu. (kweli?)
.......... ilikuwa wazi kuwa Pacha, kama Mkristo na kabila yake Mlulwa kutoka Mpanda, hawezi kukubalika na Wamanyema wa Tabora. Wamanyema walikuwa wanajulikana kwa tabia yao ya ukaidi.
...........
harakati za pili za Waislam, safari hii kuchukua serikali kutoka kwa Wakristo. Harakati za kwanza zilikuwa zile za kumngíoa Mwingereza katika ardhi ya Tanganyika

.............
Katika miaka ya 1950, jiji la Dar-es-Salaam lilikua na la Waislamu. Hata mabibi wa Kikristo walikua wakivaa mabuibui, kivazi cha Waislamu.
.................

[/QUOTE]
Hizo ndio zake Mohammed Said,mwandishi who is basking in the sunshine of inconsequential foreigners and half cooked admirers.
Elewa tu muheshimiwa Mohammed kuwa siku ya siku , tutakapokula sahani moja hawa jamaa watakuwa wakila kuku huko makwao.


In general huyu ndugu yetu Mohammed Said is unstable upstairs.Nimejaribu kumuweka katika bahasha inayoeleweka lakini sipati anuani.

Kwa vile kwa mambo anayoandika anaomba msaada wa wataalam zaidi yake..PSYCHOLOGISTS mimi namshauri aende mbali zaidi apate ushauri wa PSYCHIATRISTS.
 
JK: Ahsante kwa ushauri wako. Insha Allah na tuendelee kujadiliana na kupeana nasaha kama hizi. Najifunza mengi. Wamanyema kama Warufiji na Wangazija huwezi kupata Mkristo. Huu ni ukweli ingawa huenda wengine wasiupende. Naitakia nchi yangu amani ya kweli ndiyo maana niliandika kitabu kile. Haiwezekani Wakristo wahodhi kila kitu halafu useme hivi ndivyo ilivyotakiwa na mtegemee Waislam waridhie na hali hiyo miaka nenda miaka rudi. Allah anawakataza Waislam kudhulumu na vilevile amewakataza kukubali kudhulumiwa. Wanaodhulumu hawathubutu kutoa majibu sana sana wameishia kupiga vitabu marufuku (Mwembechai Killings) na kukusanya magazeti (Africa Events).
 
Mkandara kwa hili wala sihitaji kumuuliza mtu. Yanga iko Mtaa wa Sukuma chuo chetu kwa Shariff Abdulrahman milango inatazamana. Nimuulize nani? Shariff Abdulrahman akicheza Yanga. Baba yangu kasoma Qur'an kwa Mwalimu Mzinga mtoto wake (Mambo Mzinga) alikuwa mchezaji wa Yanga hao wote ni wazee wangu. Mambo Mzinga na baba yangu wamesoma chuo kimoja hapo Mtaa wa Mafia na Chura. Sikuwa na haja ya kutafuta habari za Yanga kwa yeyote yule ni historia iliyokuwa ndani ya nyumba yetu. Hao watu wa magazeti masikini ya Mungu wanajiandikia tu bila ya hata kufanya utafiti. Ikiwa mtataka kujua historia yetu iko wazi tutaieleza na kama inakupeni shida haipendezi kwenu hiyo ni bahati mbaya. Mzee Kitwana Kondo wakati alipokuwa Mayor wa Dar es Salaam alilalamikiwa kwa kubadili baadhi ya majina ya mitaa ya Dar es Salaam na kuipa majina ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika. Katika mahojiano na Sarah Dumbah wa RTD Mzee Kondo alisema kama kuna mtu hajui Mshume Kiyate alikuwa nani katika TANU na aulize tutamwambia. Kwa hasad zao hadi leo wamekataa kubadili kibao cha Mtaa wa Tandamti na kuuita jina la Mshume Kiyate. Katika khutba niliyotoa Msikiti wa Idris bin Saad mwaka huu mwanzoni niliwaambia Waislam mara nyingine mkinialika hapa nataka nikione kibao cha Kiyate Mshume kimewekwa (Msikiti wa Idris bin Saad upo Mtaa wa Tandamiti na Donge. Tandamti ndiyo mtaa akiishi Mzee Mshume Kiyate.) Ukipenda naweza kukuwekea kipande cha mchango wake katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Mzee Mshume ni mmoja wa mashujaa wetu waliofutwa katika historia.
 
Mkuu wangu kuwa mchezaji wa Yanga haina maana ataajua historia ya Timu hiyo. Nakwambia wewe tafuta ukweli haiwezekani ukweli wako ndio pekee kwa sababu ulienda chuoni karibu na hapo.. Hii akili gani mkuu wangu. Nasema hivi, mimi nimeona ktk TV - Yanga wenyewe wakim enzi marehemu Karume live on TV April mwaka huu..na historia ikazungumzwa kwa kumpongeza Marehemu. Leo wewe unakuja na mambo ya Yanga na TANU hali havihusiani kabisa isipokuwa rangi zake. sasa utakuja sema hata haya nayoandika ni uongo tafuta ukweli mkuu wangu tafuta ukweli na sio wewe kufanya maamuzi ya mwisho.
 
Bona: Ahsante kwa mchango wako umechelewa kuingia katika mjadala. Swali lako nishalijibu huko nyuma. Nimeandika historia ya wazee wangu ili niweke kumbukumbu zao kwa faida ya kizazi kijacho. Historia rasmi ilikuwa inamtukuza Nyerere peke yake. Nikaona ni vyema nami niandike ili na ya wazee wetu ijulikane pia. Kwa bahati mbaya historia hii inawachoma watu wengine kwa kuwa waliokuwa mstari wa mbele kupambana na ukoloni walikuwa Waislam. Wao hawataki Waislam watajwe kwao wao ni kuingiza udini.
 
Mkandara: Mimi sina ugomvi na mawazo kama hayo uwanja ni wa kila mtu na mtu ana ruhusa ya kueleza lile analojua. Wanaotusoma watapima nani anasema kweli. Mwinyi Mangara mtoto wa Tabu Mangara mchezaji wa Yanga 1940s na Rais wa Yanga 1960/70 yu hai yuko pale Ilala waandishi wamfuate kwa mahojiano. Mtoto wa Kondo Kipwata aliekuwa kiongozi kabla ya Mangara Tabu wanae wapo na wawatafute kwa mahojiano. Captain Maliki aliecheza Yanga sisi bado wadogo sana yuko pale Club ya Pan African na akahojiwe. Hapana shaka ni hivi ndivyo inavyotakiwa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…